Na Rehema Maigala
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam, jana
imetupilia mbali ombi la Bi. Aurelia Ngowi, aliyekuwa mke wa Mkurugenzi wa
Utawala na Fedha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Amatus Liyumba
.
Bi. Ngowi
alifungua kesi mahakamani hapo akitaka aruhusiwe kuishi katika nyumba iliyopo
Mbezi Beach ambapo ombi hilo lilitupwa baada ya mahakama kwenda kujiridhisha
katika nyumba hiyo na kukuta ni ya biashara si ya kuishi familia kama alivyodai
katika maombi yake.Hata hivyo,
mahakama hiyo imemtaka Bi. Ngowi ahame katika nyumba hiyo ili mdaiwa Bw.
Liyumba aendelee na shughuli zake za kibiashara.
Kesi hiyo
ilikuwa mbele ya Hakimu Jackline Rugemalila, ambaye alidai kuwa, hayo ni ma omb
i ma d o g o amb a y o yalipelekwa na mdai mahakamani hapo.Mahakama hiyo
ilikwenda hadi katika nyumba husika ambapo baadhi ya majirani walisema nyumba
hiyo tangu ijengwe, haijawahi kuishi watu bali ni nyumba ya biashara Amjen
Excutive Hotel.
Bi. Ngowi
alipeleka maombi saba mahakamani hapo ambayo ni kuiomba mahakama hiyo imzuie
Bw. Liyumba aache kutawanya mali za familia pamoja na kutaka kuuza nyumba
inayokaa familia.
Katika kesi
hiyo ya madai, Bi. Ngowi alidai kufunga ndoa na Bw. Liyumba mwaka 1978. Kesi ya
msingi ya madai ya talaka, itatajwa Septemba 16 mwaka huu.Bw. Liyumba anatetewa na wakili
Sweetbert Nkuba wa kampuni ya Austin and Wilson, wakili wa mdai ni Margaret
Ringo
No comments:
Post a Comment