Na Kassim
Mahege
RAIS Jakaya Kikwete, amefanya mabadiliko
ya makatibu wakuu 13 na manaibu 14 katika wizara mbalimbali nchini, hatua
ambayo inalenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi Serikali.Mabadiliko hayo
yalitangazwa Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Sefue Ombeni,
alipozungumza na waandishi wa habari.
Katika mabadiliko
hayo mapya waliokuwa makatibu wakuu wa wizara tatu watapangiwa kazi maalum.
Alisema miongoni mwa makatibu wakuu wapya na manaibu wao miongoni mwao wametoka
serikalini na wengine sekta binafsi na wengine kutoka wizara moja kwenda
nyingine
Walioteuliwa na
wizara zao kwenye mabano ni Florence Turuka (Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu),
Joyce Mapunjo (Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki), Sihaba Mkinga (Katibu
Mkuu, Habari, Michezo na Utamaduni) na Sofia Kaduma (Katibu Mkuu Kilimo na
Ushirika)
Wengine, Dkt. Deo
Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Afya), Uredi Mussa (Viwanda na
Biashara), Dkt. Servacious Likwelile (Katibu Mkuu Wizara Fedha).Watakaopangiwa kazi
nyingine baada ya kuondolewa kwenye nafasi zao ni Seth Kamuhanda, Kijakazi
Mtengwa, Omary Chambo.
Manaibu Makatibu
Wakuu wapya na ofisi zao kwenye mabano ni kama ifuatavyo, Angelina Madete
(Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira), Regina Kikuli (Ofisi ya Waziri Mkuu),
Zuber Samataba (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),
Edwin Kiriba (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) na
Deodatus Mtasiwa (Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa
-(Afya).
Wengine ni Dkt.
Yamungu Kayandabila (Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika) Prof. Adolf Mkenda
(Wizara ya Afya-Sera) Dorothy Mwanyika (Wizara ya Fedha- Fedha za Nje na
Madeni), Rose Shelukindo (Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) Dkt.
Selassie Mayunga (Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) Monica
Mwamunyange (Wizara ya Uchukuzi) na Consolata Mgimba (Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi)
Aliwataja wengine
kuwa ni Elisante Ole- Lazer (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo),
Armantius Msole (Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki).Kwa upande wa waliohamishwa ni John Mngodo ambaye amehamishiwa Wizara ya
Mawasiliano, Selestine Gesimba, amepangiwa Wizara ya Maliasili na Utalii,
Mhandisi Ngosi Mwihava amehamishiwa Wizara ya Nishati na Madini.
No comments:
Post a Comment