Na Ester Maongezi
WASHIRIKI 20 waliopita katika mashindano ya kuimba ya Epiq Bongo
Star Search (EBSS), wanatarajia kuingia kambini wiki ijayo kwa ajili ya
kujiandaa na fainali ya michuano hiyo.Akizungumza Dar
es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoandaa
mashindano hayo, Rita Poulsen alisema wameamua kuwaingiza kambini washiriki
hao, ili kujifunza mambo mengi zaidi
.Rita alisema amefurahi kupata idadi nzuri ya vijana na wenye ubora waliojitokeza kwenye usaili na anaamini kwa mwaka huu kutakuwa na ushindani mkubwa."Tumepata washiriki makini kutoka mikoa mbalimbali, hivyo mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani mkubwa tofauti na miaka iliyopita na nina imani tutapata wasanii bora zaidi," alisema Rita

Rita alisema
mashindano hayo kwa mwaka huu yatarushwa kupitia kituo cha TBC Taifa kila
Jumapili.
Alisema wameamua kuitumia TBC kwa
sababu za kibiashara na hiyo ni kutokana na tafiti alizozifanya, kabla ya
kufikia uamuzi huo."Hakuna sababu nyingine
iliyosababisha kuyahamishia matangazo ya EBSS kutoka ITV, kama uvumi
unavyoenezwa na baadhi ya watu ila nilijaribu kufanya uchunguzi na kugundua TBC
inatazamwa karibu mikoa yote ya Tanzania.
"Hiyo kwangu nikaona ni fursa kwa
Watanzania kupata burudani na kutambua vipaji vilipo nchini," alisema
Rita.Naye mshindi wa mwaka jana wa EBSS,
Walter Chilambo alisema vijana wajitokeze kwa wingi katika mashindano hayo na
kwa wale waliokosa nafasi ya kujisajili kwa mwaka huu nafasi bado ipo kwa
mwakani, hivyo wasikate tamaa.Usaili wa EBSS mwaka huu, ulifanyika katika Mikoa sita ya Arusha,
Mbeya, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na Dar es Salaam. Washiriki 50 walipatikana
lakini walichujwa na kubaki 20.
No comments:
Post a Comment