- WAIBANA SERIKALI VIGOGO DAWA ZA KULEVYA
Na Darlin Said
CHAMA c h a Wa n a n c h i (CUF),
kimemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi, kukomesha
biashara, matumizi ya dawa za kulevya na utoroshaji wa nyara za Serikali.Mwenyekiti wa
chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba, aliyasema hayo katika taarifa yake kwa
vyombo vya habari jana wakati akizungumzia maazimio ya Baraza Kuu la CUF Taifa,
ambalo liliazimia mambo mbalimbali.
Alisema jukumu
la kukomesha vitendo hivyo nchini, halipaswi kufanywa na Waziri wa Uchukuzi
Dkt. Harrison Mwakyembe ili kuwalinda vijana na heshima ya Taifa.A l i o n g e z a k u w a , D k t .
Mwakyembe ana majukumu mazito ya kusimamia reli, bandari, viwanja vyndege,
usafirishaji pamoja na suala zima la uchukuzi.
Prof. Lipumba alisema, umefika wakati
wa Serikali kupambana na wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya ambao ndiyo
wanaoharibu sura ya nchi kimataifa badala ya kuelekeza nguvu zao kwa
wafanyabiashara wadogo.
"CUF inasikitishwa na biashara ya
dawa za kulevya kushika kasi nchini na kutoroshwa kwa nyaraka za Serikali bila
vyombo vya dola kuchukua hatua stahiki badala yake nguvu kubwa inatumika kuzima
uhuru wa vyama vya siasa, waandishi wa habari, wanaharakati na viongozi wa
dini."Nguvu hizi zingetumika kupambana
na majanga ya ujambazi, wizi wa rasilimali, ubadhirifu serikalini na madhambi
mengine,
Watanzania wangekuwa na uchumi imara na
kungejenga Taifa lenye nguvu kubwa kidemokrasia siku za usoni," alisema.Wakati huo huo,
baraza hilo limedai kusikitishwa na mgogoro wa kiuchumi uliotangazwa na nchi za
Rwanda na Uganda juu ya kutumia Bandari ya Dar es Salaam kutokana na urasimu
uliopo pamoja na miundombinu mibovu ya barabara, bandari.
"Baraza limeitaka Serikali
kulitazama jambo hili katika sura ya kiuchumi badala ya mtazamo wa kisiasa ili
kuweka mkakati wa kulinusuru Taifa," alisema Prof. Lipumba.Alitoa wito kwa Rais Jakaya Kikwete,
kuendelea kutumia njia za kidiplomasia kutatua mgogoro uliopo kati ya Tanzania
na Rwanda ili kuleta maelewano ambayo yatadumisha usalama wa nchi hizo.
Katika hatua nyingine, CUF imeitaka
Serikali itoe taarifa zinazohusu ripoti za uchunguzi uliowasilishwa na tume
zilizokuwa zikichunguza matukio mbalimbali ili wananchi waweze kujua ukweli.Alizitaja tume hizo kuwa ni pamoja na ile ya kuchunguza mauaji ya Padre
Mushi, Mwandishi Daudi Mwangosi, kutekwa na kuteswa kwa Dkt. Ulimboka, Mhariri
Absalom Kibanda na kuitaka iunde tume huru ya kuchunguza tukio la kupigwa
risasi kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shekhe Ponda Issa
Ponda
No comments:
Post a Comment