- NI MFANYABISAHARA WA MADINI ARUSHA
Na Omary
Moyo, Arusha
MFANYABIASHARA wa madini ya tanzanite,
Bw. Steven Alex, amepigwa risasi jana jioni na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi
eneo la Pangani, jijini Arusha na kuporwa zaidi ya sh. milioni 60.Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,
walisema mfanyabiashara huyo alikuwa ndani ya gari lake akiwa
amepaki eneo la Pangani ili aweze kulipa madeni kwa watu waliokuwa wamemuuzia
madin
Walisema ndani ya gari hilo ambalo lilifungwa
vioo, alikuwa na wenzake wawili ambapo ghafla walitokea vijana watatu waliokuwa
na pikipiki aina ya Toyo ambazo namba zake hazikufahamika wakiwa
wameifunika na mifuko ya nailoni.“Walimgongea dirishani wakitaka afungue
mlango, huyu mfanyabiashara hakufungua ndipo vijana hao walichomoa bastola na
kuanza kugonga tena kwenye dirisha la gari.
“Walipoona hafungui, kijana mmoja
alimimina risasi kwenye mlango wa mfanyabiashara huyo na zilimpata ubavuni,
miguuni na tumboni...risasi nyingine ilimjeheruhi mwenzake Bw. Abel Musa,
mwingine aliinama hivyo zilimkosa,” alisema.Waliongeza kuwa, baada ya vijana hao
kufanya unyama huo, walifungua mlango na kuchukua mfuko wa rambo uliokuwa na
zaidi ya sh. milioni 60 na kutoweka nazo kila mmoja akielekea upande wake.
Walisema baada ya tukio hilo, wananchi
walikusanyika na kumchukua mfanyabiashara huyo ambaye alikuwa amejeruhiwa
vibaya na kumkimbiza hospitalini.“Inasemekana njama hizo zilipangwa na
wafanyabiashara wenzake ambao waliwasiliana na majambazi na kuwaeleza mwenzao
analipa madeni kwani alianza kuzunguka maeneo mbalimbali.Kamanda wa Polisi mkoani Arusha,
Liberatus Sabas alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alikiri kulisikia lakini hakuwa na
maelezo hivyo aliahidi kulifuatilia zaidi
No comments:
Post a Comment