- MASHTAKA YAKE TAYAI AMEANDALIWA
- KAULI YA KIKWETE YAKWAMA KUMUOKOA
Na Mariam Mziwanda
KITUO c h a S h e r i a n a H a k i z a
B i n a d a m u ( LHR C ) , k ime t a n g a z a kumburuta mahakamani
keshokutwa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa kile kinachodaiwa amekaidi kufuta
kauli yake ya kuruhusu vyombo vya usalama kupiga wananchi wanaokaidi amri za
vyombo hivyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi na mwanasheria wa LHRC, Harold Sungusia, alisema wanamfungulia shtaka Waziri Mkuu Pinda, kesi ya kimkakati itakayomlazimu ajibu mbele ya mahakama msimamo wa Serikali iliyosababisha atoe kauli hiyo.
Katika
kikao cha Bunge lililopita wakati wa maswali ya papo kwa papo Waziri Mkuu
alisema;“Ukifanya
fujo na umeambiwa usifanye hiki na wewe ukaamua ukakaidi utapigwa tu, maana
hakuna namna nyingine...ehee maana wote tukubaliane nchi inaongozwa kwa misingi
ya kisheria, sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona wewe ni imara zaidi, wewe
ndiyo jeuri zaidi watakupigwa tu na mimi nasema muwapige kwa sababu hakuna
namna nyingine maana tumechoka sasa.”
Sungusia
alisema kauli hiyo ya Waziri Pinda ni uvunjaji wa katiba ya nchi na haki za
binadamu, hivyo hawataikalia kimya. Alisema walishamtaka afute kauli yake,
lakini hakufanya hivyo.
Alisema
pamoja na bosi wake (Rais Jakaya Kikwete) kueleza umma kuwa Waziri Pinda,
aliteleza, lakini bado LHRC inaona anayo ya kujibu mbele ya mahakama.
Mwanasheria
huyo alifafanua kuwa kauli ya Waziri Pinda ni ukiukaji wa ibara ya 13 ya sheria
inayozungumzia usawa mbele ya sheria na ibara ya 30 ibara ndogo ya (3)
inayoeleza kama haki ya mtu inavunjwa, imeshavunjwa au inaelekea kuvunjwa
unaweza kupeleka shauri lako Mahakama Kuu.
“Kwa hiyo LHRC
hatutamvumilia na kuona haki za raia zinavunjwa... kauli ya Pinda
ametudhihirishia msimamo wa Serikali, hivyo hata waliokuwa wanafanya matukio na
kunyanyasa raia (polisi) kumbe walikuwa mgongoni mwake na walikuwa wakilindwa
na yeye,” alisema Singusia.
Kuhusu ripoti ya nusu
mwaka ya kituo hicho, LHRC iliainisha vifo vya wananchi vilivyosababishwa na
vyombo vya sheria. Kwa mujibu wa takwimu hizo, kwa mwaka huu kati ya Januari
hadi Juni watu 22 wamekufa kwenye mikono ya polisi, wanajeshi ama Sungusungu.
Kwa upande wa Katiba,
Singusia alisema vyama vya siasa vinatakiwa kukaa pembeni kuwaachia wananchi
suala zima la rasimu ya katiba ili kuepuka kuwa na Katiba iliyopatikana kwa
matakwa ya vyama hivyo ambayo yatakuwa si maamuzi ya wengi kwani idadi kubw ani
watu wasio na chama nchini.
Alisema kutokana na
umuhimu huo wa mchakato wa katiba ni vyema suala hilo likaendeshwa kwa umakini
ili ipatikane katiba itakayokidhi matakwa ya wengi, kwani bado maeneo ya vijijini
na pembezoni mwa nchi watu wengi hawakupata nafasi ya kutosha ya kutoa maoni
yao.
Kituo hicho pia
kimeishauri Serikali kuona umuhimu wa kuwepo kwa sera ili kuwa na sheria
itakayozungumzia suala la imani za ushirikina.
Alisema hiyo ni kwa sababu watu wengi wanakufa kutokana na
imani hizo. Alisema hadi Juni mwaka huu watu 300 waliuawa kwa imani za aina
hiyo.
Na akipatikana na hatia aachie madaraka ya uwaziri mkuu kwa kujiuzuru kama masharti ya utumishi wa umma yanavyotaka
ReplyDeleteUnataka apatikane na hatia gani? Akijiuzulu utafaidika kwa kitu gani?
ReplyDeletePinda ni shujaa. Anajua atastafu ama atabadilishwa uwaziri mkuu. Kwavile uwaziri mkuu sio cheo cha kudumu. Wako Wastaafu kibao kwa nafasi hiyo. Anajua atashtakiwa na watu wasioombea mema nchi hii. Lakini akakubali kujiweka mashakani tena kwa kurudia. Tunapenda mashujaa kama Pinda. Hatuwezi kubaki tumejikunyata wakati wahalifu wanatamba barabarani utadhani hatuna serikali.
ReplyDelete