Na Zourha
Malisa
MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar
es Salaam kwa tiketi ya CCM, Idi Azzan, amejipeleka polisi na kutaka jeshi
hilo, kufanyia uchunguzi tuhuma za kuhusishwa na biashara za dawa za kulevya na
iwapo itabainika anahusika, hatua za kisheria zichukue mkondo wake
.Mbunge
huyo alifikia hatua hiyo jijini Dar es Salaam jana baada ya barua zilizoandikwa
na watu wanaodai ni wafungwa wa Tanzania wanaotumikia adhabu zao mjini Hong
Khong, nchini China, kusambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimhusisha yeye
(Azzan) kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo akiwatumia vijana hao. Wafungwa hao
wanadaiwa kuwa wanatumikia adhabu zao baada ya kupatikana na makosa ya dawa za
kulevya.
Mbunge huyo alisema
alienda kutoa taarifa hizo mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es
Salaam.“Nimeamua kwenda
kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo
hilo na ukweli ubainike na hatua za kisheria zifuate juu yangu,” alisema Azzan,
wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana.
Azzan alibainisha
kuwa ameamua kwenda kutoa taarifa polisi ili waanze uchunguzi wao. Alisema
barua hizo ambazo hazina anuani ya eneo zilipotoka wala majina ya waandishi
wake zina lengo baya dhidi yake na kutaka kuposha umma.
“Mimi sipo juu ya
sheria itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja,
na nitajiuzulu ubunge wangu,” alisisitiza Azzan na kuongeza;
“Wapigakura wangu wa
Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina
nia mbaya yenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja
majina yao.”
Mwishoni wiki hii
katika mitandao mbalimbali ya kijamii ziliwekwa barua zinazodaiwa k u a n d i
kwa n a wa f u n gwa waliokamatwa na dawa za kulevya nchini China zikimhusisha
mbunge huyo na biashara hiyo.
Barua hizo pia
zinawataja baadhi ya viongozi wa serikalini kuwa wanajihusisha na mtandao
wadawa za kulevya, lakini hazikuainisha majina yao.
No comments:
Post a Comment