Na Ester Maongezi
MTIHANI wa uwakala wa wachezaji na
uwakala wa mechi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA),
unatarajia kufanyika Septemba 26 mwaka huu kwenye ofisi za Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania
(TFF)
.Akizungumza Dar es Salaam jana Ofisa Habari wa TFF,
Boniface Wambura alisema katika mtihani huo, kutakuwa na jumla ya maswali 20.Alisema 15 kati ya hayo yanatoka FIFA
kuhusiana na kanuni za kimataifa za mpira wa miguu na matano yatatoka TFF,
kuhusiana na kanuni mbalimbali zinazotawala mchezo huo nchini.
Wambura alisema kwa ambao wangependa
kufanya mtihani huo, utakaokuwa katika lugha ya Kiingereza ambayo ni moja kati
ya lugha nne rasmi za FIFA, wanatakiwa kujisajili TFF kwa ada ya dola 50 za
Marekani, ambapo watapewa utaratibu na maeneo ambayo mtihani huo unalenga.“Mtihani huo utafanyika saa 4 kamili
asubuhi na muda wa kufanya mtihani hautazidi dakika 90.“Mpaka sasa Tanzania
ina mawakala watano wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni John
Ndumbaro, Mehdi Remtulla, Ally Saleh, Yusuf Bakhresa na Said Tully,” alisema
Wambura.
No comments:
Post a Comment