Na Patrick Mabula Kahama,
Wagonjwa walilazwa katika Hospatari ya Wilaya ya
Kahama wamenusulika kufa kwa tukio la
kupigwa na radi baada ya kutua
ndani ya hospitari hiyo .
Radi hiyo ilipiga katika hospitari hiyo juzi jioni mda
wa saa kumi na moja na kutua karibu na wodi namba moja
kwenye mti ambao iliupasua vipande vipande na kuzusha
hofu kwa wagonjwa waliokuwa wamelazwa.
Wakisimulia tukio hilo wagonjwa waliolazwa katika wodi namba
moja ya wanaume ,mzee Andrew Maganga alisema wakati
radi hiyo ikipiga walikutwa nje yeye na baadhi ya waliolazwa
hapo na ilitua kwenye mti na kuupasua pasua.
Bw.Peter Juma alisema wakiwa wamekaa mita chache kutoka
katika mti uliopigwa ghafla waliona mwanga mkali sana
mwekudu na bruu kisha radi ilitua sehemu hiyo na kuupasua
vipande vipande mti huo.
Bw.Juma alisema cha kushangaza baada ya radi hiyo
kupiga na kuupasua pasua mti huo cha kushangaza watu
mbalimbali wakiwemo watoto walianza kufika katika hospitari
hiyo na kuanza kugombania na kuchukua magome
yaliyokuwa yamechanwachamwa.
Wagonjwa hao walisema katika kugombania vipande vya
miti hiyo baadhi ya watu wengine walifika hapo na mashoka na
mapanga na kuanza kukata matawi na kuondoka nayo huku
wengine wakipiga magoti hapo na kuanza kuomba dua
Mganga mkuu wa Hospitari ya wilaya ya Kahama Dk. Andrew
Emmanuel aridhibitisha kupiga kwa radi hiyo na kusema
ilipasua mti mkubwa lakini hakuweza kuua wala
kusababisha kifa kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitari
hiyo
mmh mambo ya imani hayo
ReplyDeleteni ulozi tu .
ReplyDelete