09 January 2013

Wanaume epukeni unyanyasaji wa kijinsia

Na Steven William,
Muheza

WANAUME wilayani Muheza wametakiwa kufahamu kwamba hawapaswi kupewa
tendo la ndoa na wake zao kila siku ndani ya siku 30 kwani watambue
huo ni unyanyasaji wa kijinsia.


Hayo yalisemwa na mwezeshaji kutoka jeshi la polisi wilayani Muheza
Amina Ngonyani katika mafunzo ya siku moja na kuratibiwa na kikundi
cha ujasiliamali cha Inuka yalifanyika katika ofisi ya kata ya
Masuguru juzi.

Alisema kuwa haipaswi kila siku mwanaume kupewa tendo la ndoa na mke
wake ndani ya mwezi mzima huo ni unyanyasaji mkubwa katika ndoa.

Ngonyani alisema kuwa hata kama mke wako hataki amechoka mwanaume
anamlazimisha afanye tendo la ndoa hata kwa nguvu kwa kisingizio
amemuoa ni haki yake.

Alisema kuwa sheria hiyo ya kupinga unyanyasaji ilianza mwaka 2007
ambapo kuna baadhi ya wanaume wamekuwa makatili kwa kuwapiga wake zao
wanaporudi nyumbani kisa chakula hamna na kwamba mwanaume hajaacha
chochote nyumbani.

Ngonyani alisema kuwa pia mwanaume kumuolea mwanamke mwingine mke wake
ni unyanyasaji ambapo inasababisha ndoa kuvunjika kutokana kwamba
upendo utazidi kwa wanawake wengine.

Alisema kuwa katika unyanyasaji mwingine ni ule mwanaume anamuomba
tendo la ndoa mke wake kinyume na maumbile kwa kuwa amezoea kufanya
hivyo kwa mwanamke mwingine wa nje.

Ngonyani alisema kuwa upo unyanyasaji mwingine wa watoto utakuta mama
wa kambo anampiga mtoto kwa kuwa sio wake huku nao wanaume wanawabaka
watoto kitu ambacho sio kizuri.

Alisema kuwa tayari ameshapokea kesi nne za wakina baba kuwabaka
watoto kinyume na maumbile ambapo huo ni unyanyasaji mkubwa.

Ngonyani alisema kuwa upo unyanyasaji mwingine katika taasisi za kutoa
huduma watu wananyanyaswa sana wanapofika hususani polisi na huduma za
Afya.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kukundi cha ujasiliamali cha Inuka David Msuya aliwataka wananchi kujua haki zao za kimsingi kuhusu unyanyasaji wa kijinsia na kupinga ukatili wanaofanyiwa kwani ni haki yao wasiogope.

Kwa upande wao Afisa mtendaji wa kata ya Kwemkabara Imani Mtumbi na
Afisa mikopo kikundi cha ujasiliamali cha Inuka wilayani Muheza Jemes
Msuya Vipepeo kwa nykati tofauti walishukuru sana kupata elimu hiyo
wataifanyia kazi.

1 comment:

  1. mmh kweli unakuta mwanaume anaambiwa na mkewe kwamba amechoka yeye anataka tu tena kwa lazima

    ReplyDelete