Na Mwajabu Kigaza, Kigoma.
JESHI la Polisi Mkoa Kigoma kwa kushirikiana na SUMATRA katika uchunguzi wao wamebaini kuwa boti iliyosababisha vifo vya watu kumi na tatu na wengine 67 kuokolewa katika Ziwa Tanganyika mkoani hapa ilikuwa ni boti ya Mizigo na sio ya abiria.
Akitoa taarifa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kigoma Fraisser Kashai alisema kuwa tukio hilo la ajali ya kuzama majini lilitokea Januari 3, 2013 majira ya saa nne na nusu usiku katika eneo la mwambao mwa Ziwa Tanganyika eneo la Herembe Kata ya Sigunga Wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma ambapo lilikuwa likitokea Namansi Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa kuelekea nchini Burundi.
Kamanda Kashai alisema kuwa boti hiyo yenye namba za usajiri KST 0029 MV Yarabi Tunusuru iliyokuwa ikiendeshwa na nahodha bw Akilimali Seif (34) mkazi wa Kalungu Nkas na mmiliki wa boti ni Msiwa Omary (34) ambao walitenda kosa la walipakia abiria kwenye boti la mizigo huku usajiliwa wa boti hilo ukiwa ni kubeba mizigo tu.
Kashai alisema kuwa boti hilo lilipakia jumla ya abiria 85 na tani za mizigo 45 ambapo boti hilo lilizidiwa na mzigo na kuzama ndani ya Ziwa Tanganyika na kusababisha vifo na pamoja na uharibifu mkubwa wa mali.
Alisema kuwa hadi sasa Jeshi la Polisi limefanikiwa kupata maiti 13 ambapo wanaume ni wanne na wanawake tisa na kusema kuwa watuhumiwa wa tukio hilo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayo wakabili.
No comments:
Post a Comment