11 January 2013
Kikwete afunga mjadala wa gesi *Awashukia wanasiasa wanaotafuta njia ya kujijenga *Ahofia nchi kupasuka vipande, wazee wampongeza
Na Mwandishi Wetu, Tabora
RAIS Jakaya Kikwete, ametangaza msimamo wa Serikali kuhusu madai ya wananchi mkoani Mtwara ambao Desemba 2012, walifanya maandamano makubwa ya kupinga ujenzi wa bomba
la gesi kutoka mkoani humo hadi Dar es Salaam.
Alisema kama kila Mkoa utazuia rasilimali waliyonayo isitoke katika mikoa yao, upo uwezekano Taifa kupasuka vipande.
Rais Kikwete aliyasema hayo mkoani Tabora baada ya kupokea risala ya wazee ambao alikutana nao Ikulu ndogo mjini humo na kuainisha athari za madai ya wananchi kama yatasikilizwa.
Aliongeza kuwa, kama kila Mkoa utataka kubaki na rasilimali
yake, Tanzania itapasuka vipande. “Sisi wanasiasa, baadhi yetu tumeharibikiwa, wengine wanatafuta namna ya kujijenga
upya kwa kutumia suala la gesi asilia,” alisema.
Wazee hao walidai kuwa, wao wanaunga mkono msimamo wa Serikali kuwa rasilimali zilizopo nchini ikiwemo gesi asilia ambayo imegunduliwa katika mikoa mitatu ya Tanzania ukiwemo Mtwara, itumike kwa manufaa ya nchi si kwa Mkoa husika pekee.
“Msimamo wa baadhi ya wananchi mkoani mkoani humo wakiongozwa na wanasiasa hasa kutoka upinzani, unashangaza kwani miaka yote tangu uhuru, msimamo wa nchi ni kuwa na rasilimali ambayo inapatikana sehemu yoyote nchini na kutumika kwa ajili ya Watanzania wote si kwa mikoa yenye rasilimali husika pekee.
Walisema Serikali inatumia mabilioni ya fedha kujenga bomba hilo kwenda Dar es Salaam ili umeme uweze kuzalishwa kwa wingi nchi nzima kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.
“Sisi tunaamini kuwa wenzetu wa Mtwara wamepotoka, msimamo wetu wa kihistoria nchini ni kwamba, rasilimali za nchi zitumike kwa ajili ya Tanzania na Watanzania wote,” walisema wazee hao.
Aliongeza kuwa, wana Mtwara walioshiriki maandamano hayo wamedandia ajenda ambayo hawaijui na hawakuianzisha wao kwa sababu kazi ya gesi asilia imefanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini wanaojaribu kuvuruga kazi hiyo ni wapinzani.
Katika hatua nyingine, wazee hao waliitaka Serikali kuanzisha
sera na utaratibu wa kutenga sehemu maalumu katika hospitali
zote nchini kwa ajili ya kuhudumia wazee ambao wanapata
shida ya kupanga foleni ili kupatiwa huduma za afya.
Waliupongeza msimamo wa Serikali kuhakikisha hakuna ardhi ya Mtanzania inayochukuliwa kwa matumizi ya umma bila wahusika kufidiwa fedha na kupewa muda wa kuachia ardhi hiyo.
Akizungumzia matibabu yao, Rais Kikwete alikubaliana na wazo
la kuanzisha sehemu maalumu za matibabu kwa wazee katika
hospitali mbalimbali nchini. “Hili ni wazo zuri, tutaangalia jinsi
ya kulitekeleza,” alisema Rais Kikwete.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hizi zote siasa tumechoka na huyu zuzu
ReplyDeleteRais hana jipya,anatakiwa aende mtwara akaongee na wananchi kuhusu gesi yeye kazi anayo fanya ni kupita kuongea pembeni.
DeleteMwambie aende mtwara akaongee na wananchi yeye anaogopa kwenda ndio maana akaenda Tabora.
kama umepewa pesa ili uandike kuhusu gesi kaka/dada umepotea gesi haitoki mtwara.
Mjadara haujafungwa kwani wewe unajua mjadala ulifunguliwa lini? mpaka useme umefungwa?
Hayo maneno ya Rais yanayoashiria kuwa mjadala wa gesi umefungwa sijayaona. Lbda kichwa cha habari kimekosewa!!!!!!!!
ReplyDeleteKweli amekosea maana hafahamu kuwa mbunge wa mtwara mjini kwa tiketi ya ccm yuko pamoja na wananchi wake kupinga kusafirishwa kwa gesi kwenda DAR,Wakiwemo madiwani wote wa ccm pamoja na mwenyekiti wa wilaya ccm ndugu Ally Chinkawene.si kweli kuwa wapinzani bali ni wananchi wote wako pamoja kwa hili la gesi isipokuwa mwenyekiti wa ccm mkoa ndugu Sinani ambae ni kibaraka mwarabu aliyewekwa kwa maslai ya kinyonyaji kukandamiza wengi kwa maslai ya wachache ni huyu na Hawa Ghasi pamoja George Mkuchika ni mawaziri waliomposha Rais kwa kubembereza wasitolewe uwaziri maana hakuna wanachofanya kwa wapiga kura wao korosho zinakopwa hawasikiki wakisema chochote.
DeleteRais Kikwete anacho fanya ni kukurupuka tu
ReplyDelete1.Mtwara amepeleka mfumo mbovu wa kununua korosho stakabadhi gharani,wakulima wa korosho wanakopwa mpaka kilo 2 za korosho na vyama vya ushirika.
wakulima wanalima korosho zao kwa shida sana, alafu wakienda kuuza serikali inakopa korosho zao zote na ina anza kuwa zungusha,njoo kesho njoo kesho,njoo mwezi ujao utapata zenu,kila wakienda wanapigwa kalenda miezi 6 sasa hawajaripwa bado.
Rais anachukua gesi wakati anajua kabisa mtwara kuna watu wanataka maendeleo pia kama dar,yeye anashida na umeme kwa nini achukue gesi ghafi?
Mwambie huo mtambo wa kinyelezi unatakiwa ukajengwe mtwara alafu yeye atapata umeme kwa njia ya waya ambao utatoka mtwara plant na kugawa tanzania mzima kwa mikoa yote.
Mtwara wanajua anataka gesi ghafi akauze dar huo ndio ukweli ndio tabia ya viongozi wa CCM.Mwambie aende mtwara akaongee na wananchi sio kubabaisha tu.
mjadala umefungwa leo!!,lini alipofungua? aje mtwara aseme hayo maneno ingekuwa vema. hizo ni propaganda tu uwezi kuchezea upupu alafu usiwashwe kutoa gesi ghafi ni kuia mtwara na kusini kijumla imetosha mlipotoa reli kwa kigezo cha vita vya ukombozi wa africa leo hakuna kigezo zaidi ya mikataba ya kifisadi kama ni umeme weka nguzo tena very cheap na muda wa mwezi tu DAR umeme tunalilia gesi ghafi ibaki ili viwanda vijengwe watoto wetu wasiitwe tena wamachinga wewe unafikiri sisi inatunogea kuwaita watoto jina hilo? mkuu wa mkoa ametuita wapuuzi na waziri wa nishati anatuita wahaini na naibu katibu wa ccm taifa asema sisi ombaomba sasa tuachieni gesi ghafi kama tutamuomba vocha alizonadi ndugu mwigulu nchemba katika kauli yake kwenye chombo cha habari juzi
ReplyDeleteSINA UHAKIKA HATA KAMA KUNA UTANDAWAZI HAIBADILISHI KAULI KUWA UTAPOTEZA MUDA WAKO KUMPIGIA MBUZI ZEZE HATACHEZA NI VEMA MJADALA UFUNGWE KWA RASILIMALIWATU IKO KAULI KICHAA AKIKIMBIA NA NGUO ZAKO UKIWA UNAOGA UKAWA UNAMFUKUZA ILI UMNYANG'ANYE WATU WATAELEWA WAZI KICHAA NI ALIYENYANG'ANYWA NGUO
ReplyDeleteWATU WA MTWARA MSIJIDANGANYE KUHUSU KUKATAZA GESI,HII NI NCHI YETU SOTE.GESI NI YETU WOTE HATA KAMA SHIMO LA GESI LINGEKUA NYUMBANI KWA MMAKONDE MMOJA.TUNAUNGA MKONO UMEME UTENGENEZWE HUKO ILI MPATE AJIRA.LAKINI ACHENI RONGORONGO ZENU.HATA HIVYO GESI IPO KWENYE MAJI YA KINA KIREFU KTK MIPAKA YA KIMATAIFA,
ReplyDeleteWatu hawajawaelewa watu wa Mtwara,wao hawakatai gesi isinufaishe Watanzania wote wao wanadai kama ni kuzalisha umeme mitambo iwe Mtwara na miundombinu ya kusafirisha umeme ijengwe kwenda Dar.Gesi ya Mtwara ipo Msimbati ni pwani tu na sio wanavyodai
DeleteHakuna gesi iliyogundulika katika mipaka ya kimataifa gesi ipo mtwara na katika bahari ya mtwara TANZANIA. kwa usemi wako na usemi wa sospeter muhongo ni muhongo kama jina lake gesi ipo mtwara nchi kavu na baharini, na kwa usemi wako na wa waziri husika gesi itakuwa ya msumbiji au comoro maana jiografia hamkuisoma.hacha kupotosha ukweli.huku kuna mapoli mengi mbona twiga hawajaletwa badala yake wankamatwa airport wamezoea kupola mali za wananchi.
DeleteNaiomba serikali ikubali kukosolewa, na inaposhauriwa izingatie ushauri husika.Kumekuwa na desturi ya serikali yetu kupenda kusifiwa tu hata kwa mambo dhaifu kuliko kukosolewa na kuongozwa ktk mambo ya msingi. Ukitaka upendeze mbele ya jicho la serikali huna budi kuipongeza vinginevyo utabatizwa majina mengi k.v. mchochezi, msaliti, mpenda umaarufu, mkaidi na mengine mengi yenye lengo la kukukatisha tamaa ili uache kuikosoa. Nawaomba wote waitakiayo Tz yetu maendeleo, wasiogope kuikosoa serikali inapopotoka lakini vilevile tuikumbushe na kuisifia yale mambo ambayo kwa kweli ilifanya vizuri. Mwisho navipongeza vyombo vya habari vingi kwa kuupa nafasi kubwa mjadala huu wa gesi, ingawa vimeshindwa kuonesha video ya maandamano hayo bali ni picha za kwenye mitandao tu. INAWEZEKANA IWAPO TU KILA MMOJA ATATIMIZA WAJIBU WAKE IPASAVYO.
ReplyDeleteserikali ya wapi isiyokuwa na mapenzi na wananchi wake?kwanini rais wa ccm akaongelee tabora wakati mtwara anapajua vizuri?kuna nini hapo,kwa nini plant isijengewe mtwara-wasikilizeni wapiga kura wenu na kulifanya suala kuwa la kisiasa zaidi,vyama pinzani kwa maoni yangu wako sahihi kwa kila hatua.maana wako bega kwa bega na wananchi wa mtwara,mfano mzuri angalia mikoa ya mwanza na shinyanga ina nn?madini yote kwisha hakuna chochote wala faida kwa wananchi wa eneo husika.ANYWAY CCM NI CHAMA CHA KIDIKTETA AMUENI MNAVYOAMUA-TZ YA KWENU MILELE
ReplyDeleteGesi ya watanzania wote? Hii serikali imeshikwa na wazimu, vipi kuhusu gesi na mafuta yanayotafutwa huko Zanzibar mbona inasemwa ni ya wazanzibari au wao si watanzania? Mbona gesi na mafuta ni yao na inatakiwa iwanufaishe wao, Haya mambo ya kufanya kila kitu Dar na Bagamoyo yatafanya nchi hii ipate matatizo. Hamna aibu mnaposema kila kitu kiwe dar....kwanini? Eti uchumi wa nchi upo asilimia 80, kwani mkifanya decentralization kuna shida gani? wa mtwara, walindi,waruvuma na wachagga, wapare, waarusha na wakigoma wakijitegemea kuna shida gani? au mnapenda kuwaona wakifukuzwa fukuzwa huko mitaani dar na polisi? Kwa nini mlitaka kuhamisha makao makuu Dodoma? Nadhani sababu kubwa ilikuwa kuondoa msongamamo na ujenzi holela Dar es salaam, lakini leo serikali hii ya CCM inaturudisha huko. Watu wa kusini komaeni na ninyi mnahitaji mikoa yenu iendelee, mmeshaonewa vya kutosha....msikubali tena.
ReplyDeletewakianza kujitenga na gesi wakati hao wachinga kibao wapo dar asa nao waanze kufukuzwa dar?suala ni uwajibikaji.ukitaka kushangaa ujer kwemye barabara zinazokuja huku bulyanhulu gold mine uone zilivyo na mashimo na matope sehemu dhahabu inapotolewa na wananchi hao hawafaidiki .kama ni kiwanda sio ishu ila uwajibikaji na hiyo mikataba mibovu ndio ishu
DeleteHiyo ni kweli tunachotaka sisi sio gas isitoke ila plant ijengwe mtwara na utoke umeme uliozalishwa huku na hiyo gas iuzwe huku ili tujue kiasi kinachotoka ili mapato mengine yachangie maendeleo ya mkoa wetu.GAS KWANZA ....
ReplyDeleteMJADALA UMEFUNGWA MAGAZETINI SASA TUONE NI GAZETI GANI RONGORONGO SI WANAJIDAI NI MHIMILI WA NNE SIJUI NI KATIBA IPI????
ReplyDeleteNi kweli,kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo raslimali zilizogundulika popote ndani ya nchi ni mali ya serikali,kwani serikali nani?
ReplyDeleteKwa maoni yangu,hasa nikirejelea michango mingi mbalimbali iliyotolewa na wananchi wa kawaida pamoja na wachambuzi wa masuala ya uchumi,siasa na maendeleo ni kama vile hoja za serikali hazina mashiko katika uwanja wowote ule.
wananchi wa mikoa hiyo ya kusini,pamoja na watanzania wote wanaounga mkono hoja za wakazi wa Mtwara walioandamana kupinga uamuzi wa serikali wa kusafirisha gesi asilia kwa njia ya bomba kutoka Mtwara kwenda DSM wako sahihi zaidi na mantiki ya maelezo yao iko bayana ukilinganisha na maelezo ya serikali ambayo yanazusha maswali mengi kiasi cha mpango huo kutiliwa shaka siyo tu na wananchi wa kusini,bali pia na yeyote aliyeelimika,aliyekomaa kifikra,na mwenye upeo wa kutosha.
Wapo wanaowapinga wananchi wa kusini kwa kukosa moja au hata sifa zote tatu hapo juu,kwa kutoyaelewa maelezo ya wananchi wa mikoa hiyo, kwa mazoea ya kifikra dhidi ya mikoa ya kusini,na pengine kutokana na hulka za kukurupukia hoja pasi na kuzifanyia uchunguzi na kujipendekeza kunakolenga faida binafsi na siyo masilahi ya umma au taifa kama wanavyoonekana kuhubiri katika majukwaa.
Kinachoshadidiwa na serikali pamoja na wapambe wake wote ni kile ambacho kwa kiingereza huitwa "FALLACY"-a failure in reasoning which makes an argument invalid.yaani,ukosefu wa sababu za msingi na zinazokubalika kufanya walau hoja zake ziwe na mashiko.
Kuna hila katika hoja ya serikali ambayo huhitaji sifa nilizozitaja hapo juu kuelewa,vinginevyo ni rahisi kuamini kuwa wananchi wa kusini wamepotoka kama ambavyo wazee wa TABOBA na wengine wengi wanavyoelekea kuamini. BALI UKWELI NI KWAMBA, "UONGO UMEWASILISHWA KISANII"na hivi mbele za wanaokosa sifa nilizozitaja kuwa ukweli ambao unafanya wananchi wa kusini waonekane wabinafsi, lakini ukweli hauna mwisho na utabakia hivyo ulivyo siku zote kwamba wananchi wa mikoa ya lindi na Mtwara wako sahihi na hivi watanzania wote tunapaswa kuwaunga mkono.
Hoja kwamba mikoa hiyo imekuwa ikitumia mapato yaliyotokana na raslimali za mikoa mingine pasi na wao kuwa na mchango ni moja tu ya "FALLACY" inayotumika kusadikisha watanzania kuwaona wananchi wa mikoa ya kusini kuwa wabinafsi huku ikiwa haizungumzii kabisa michango mingi na mikubwa iliyotolewa na wakazi wa mikoa hiyo kwa taifa hilihili,pia serikali haisemi hujuma ilizozifanya na inazoendelea kuzifanya kwa mikoa hiyo ukiacha hii ya gesi asilia.Ukifuatilia kwa makini maelezo yanayotolewa na wananchi hawa utabaini kuwa wanastahili kufanya wanachokfanya, tena watanzania wote yatupasa kuwaunga mkono.
Ninapenda hatimaye kuwashauri viongozi wetu ambao wengi wao walizaliwa,kukuzwa,kusoma na kuanza utumishi wa umma katika karne iliyopita kutambua kuwa wanaiongoza jamii ya leo isiyofahamu wala kuhitaji kufahamu hayo yaliyopita hata kama yanaweza kuhitajika katika nyakati fulani,hivyo wao ndio wanapaswa kubadilika na kuongoza wakizingatia mahitaji na matarajio ya wananchi waliowapa dhamana hiyo.
Wakazi wa mikoa ya kusini wako sahihi,serikali ikubali huo ndio ukweli,wao (viongozi)ni binadamu wenye hulka ya kukosea kama binadamu wengine,hiyo ni kawaida,cha msingi sasa warudi kwenye njia sahihi ili tuendelee kuijenga nchi yetu kwa amani,iachane na kutafuta mchawi,na kutumia lugha zinazobeza wakazi wa mikoa hiyo kwa kuwa hizo sizo sifa za viongozi makini,wajibu wao ni kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi kwa kutumia taratibu sahihi,kwa uwazi na ukweli. MUNGU AWPE HEKIMA KATIKA KUFANYA MAAMUZI,EPUKENI KUWA CHANZO CHA KUIVURUGA TANZANIA,MUWE NA KIASI,MUTOSHEWE.
Ukweli ni kwamba serikali inafahamu fika madai ya wananchi wa Mtwara ya kutaka kituo cha kufua gesi asilia kijengwe Mtwara ili kiwe kichocheo chamaendeleo ila serikali inapotosha makusudi kwa kuwa wamezoea kuona kila wanapowadhulumu wananchi wa Mtwara wanakaa kimya. Pia serikali ilishajipanga kuhujumu neema hii ndio maana haina mpango wa kuigusa HOJA ya wananchi kwa sababu ukifanya hivyo utakosa sababu ya kuhalalisha kuisafirisha gesi kwenda Dar. Ila serikali ISUBIRI machafuko na kwa taarifa yao wananchi wa Mtwara hawatanii katika suoam la gesi wako DETERMINED na hiki ndio kishiko chao cha mwisho wameamua kufa na GESI. Raisi kikwete asiseme kuwa amefunga mjadala wa gesi wananchi wa Mtwara hawana muda wa kujadili suala la gesi wao wameweka msimamo kuwa GESI KWANZA kwa hiyo kama serikali inajifanya kichwa maji basi waandae jeshi la kuja kuwauwa wananchi wa Mtwara kwa sababu hilo ndio chaguo lao endapo madai yao yatapuuzwa. Narudia tena serikali isijidangaye katika hili na kwa taarifa tu James Mbatia imeshaanza kuonja joto ya jiwe jana jioni bila kujali ni wa chama pinzani kwa sababu huku gesi kwanza vyma baadaye. Na kama serikali inadhani ni masikhara basi imtume Waziri wa nishati na madini akasisitize msimamo wa serikali mbele ya wananchi kama atarudi hai.Sio mchezo watamuua. Serikali achane ujanja ujanja hii ngoma ni nzito. Hilo bomba kwa sasa hamuwezi kujenga na kama munadhani ni utani basi wapelekeni hao wachine muone watakavyotobolewa matumbo yao kwa mishale. niye munacheza na watu wa kusini. Wamechoka kudhalilishwa rudini katika HOJA yao au acheni ianze VITA.
ReplyDeleteSerikali waachie hao gesi yao.
Deletepelekeni nguvu za utafiti na ujenzi wa miundombinu maeneo mengine yenye watu wapenda maendeleo. Mkiendelea kubishana tutaharibikiwa. waende na vijembe na visururu vyao wakacimbe gesi yao alafu witunze kwenye vibuyu watengeneze umeme wao! Fullstop. Kujitia kupenda maendeleo leo wakati mlikua mnanufaika na nguve na rasilimal za wengine. HAMNA SHUKRANI KABISA!!
Nyrere angekua hai angewachapa viboko vya makalio ili muwe na chmbe za soni. Yeye alijenga kiwanda cha kusifisha alimasi Iringa wakati almasi inachibwa Shinyanga.
mnafikiri mzee alikua mjinga?
ACHA USHENZI WA KUZITETEA HOJA ZA KUWAKANDAMIZA WATU WA KUSIN BWEGE WEWE...SERIKALI IMEUA BANDARI:RELI:KOROSHO: NA SASA WANATAKA KUIONDOA GESI KUDADADEKI TUNASEMA LAZIMA PACHIMBIKE NA SERIKALI YENU FISADI.TUPO TAYARI KUMWAGA DAMU KUTETEA RASILIMALI ZETU. ALUNTA CONTINUA
DeleteNdio. Amekusaidia hata kuweza kutumia mtandao! Utumie kwa busara. Ungeweza kuzuia utafiti usifanywe na serikali fisadi ukafanya mwenyewe ukagundua tungekusifu sana.Kama wewe mwana Mtwara wa ukweli huna haja ya jazba maanake utafaidika tu iweiweje. Kama mwana siasa tu damu ni mtaji wako katika biashara yako ya siasa na kuuza sura hivyo hatukushaingai.
DeleteFaida ya gesi ni pale inapotumika, kama haina matumizi haina faida yoyote. Gesi ilikuwepo Mtwara chini ya ardhi kwa miaka mingi, haikuwa na manufaa yoyote kwao. Ni kipindi sasa gesi imenguduliwa huko. Nafikiri ingekuwa imekwisha wanufaisha wananchi wa huko,lakini matumizi yake ni kidogo sana. Ndio maana wananchi wa huko hawaoni manufaa yake mpaka sasa, hapa kuna tatizo la msingi. Mimi nafikiri watafakari zaidi. Kama wanaona kuendelea kukaa na gesi yao bila kutumika ndio faida, inawezekana wamefungia mawazo yao kwenye boksi. Mimi nawashauri wafikirie nje ya boksi, wanaweza wakapata majibu ya busara zaidi.
ReplyDeletekama mwanza nao wakisema samaki wa mwanza hakuna kutoka, shinyanga nao na dhahabu yao , mbeya na makaaa yao ,nk , sizani kama tungefika hapa tulipo naoNA sasa siasa inatutawala kulIKO ekima na kuheshimu na kueshimu wa taaLAmu . we mbatiA KAFATA NINI UKO ALIKUWA WAPI , MBONA TUNA KURUPUKA. . KUMBUKENI TAFTI AZIJAISHA NAAMBIWA KUNA SEHEMU KUNA URANIAM . NAYO IBAKI UKO AU IENDE DAR .NAWAACHI WATAALAMU NA SIO NYIE WANA SIASA . BASI KAMA VIP SERIKALI WAOONDOE WATU WAO MTWARA WARUDI NA TEAM YAO YA WAATAALAMU TUOINE KAMA WATABEBA BABANGO AU KINA MBATIA WATAPANGA KUJA UKO SWALA LA MAENDELEOO KUSINI NI LA KIISTORIA ENZI ZA MKOLONI KWA SASA NAIPONGEZA SERIKALI KWA HATUA INAZO CHUKUA KIDOGO KIDOGO TUTAFIKA TU LAKIN TUKIEBDEKEZA KUONGEA NA WANASIADSA NA SIASA ZA MAGAZETI TUTA KWISHA JAMANI . TUESHIMU MAMLAKA TULIYO JIWEKEA
ReplyDeleteACHA MANENO YA KIFISADI WEWE KIBARAKA WA CCM,WE INAONEKANA WAZI KUWA NI SEHEMU YA MAFISADI TUNAOHANGANAO KTK NCHI HII.HOJA YA WATU WA MTWARA UNAIJUA KABLA YA KUKURUPUKA NA KUITETEA SERIKALI YAKO YA WALA RUSHWA NA MAFISADI WAKUBWA. KWA TAARIFA YAKO,HOJA YA WANANCHI NI KWAMBA GESI IINUFAISHE TAIFA IKIWA MTWARA,KWA NINI IAMISHWE KWENDA DAR KWANI MTWARA SIO TANZANIA? ELEWA HOJA,FISADI MKUBWA WEWE.
DeleteBasi tunshauri serikali ya kifisadi ya ccm ijitoe. Wawekezaji waende sehemu nyingine. Mbaki na chadema yenu na jazba zenu. Hasira za mkizi ijara ya mvuvi!! Serikali simamisheni mara moja mradi huo.
Delete