29 January 2013
Bilioni 8/- zatengwa kwa ajili ya mradi wa UMATA
Na Grace Ndossa
JUMLA ya sh. bilioni nane zimetengwa kwa ajili ya kuendesha mradi wa Usafi wa Mazingira Tanzania (UMATA) ambao utaanzia katika Mkoa wa Dodoma na jumla ya watu milioni moja watafaidika na mradi huo.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Usafi na Mazingira Prof.Anna Tibaijuka alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Prof. Tibaijuka alisema mradi huo unalenga kuhakikisha usafi wa mazingira unafanyika kikamilifu na upatikaniaji wa maji unakuwewpo katika vijiji hivyo ambao umefadhiliwa na Shirika la Kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Plan Intertional.
Alisema kuwa, mradi huo wa usafi utaenda sambamba na upatikaji wa maji utafanyika katika mikoa mitatu ambayo mkoa wa kwanza utaanzia Mkoa wa Dodoma na utafanyika kwa muda wa miaka mitano.
"Mradi wa maji ambayo utakuwa unaendelea hapa nchini utasaidia kupunguza tatizo la maji katika Mkoa wa Dodoma na wananchi wanaweza kuweka mazingira kuwa safi,"alisema Prof.Tibaijuka.
Naye Mkurugenzi wa Plan International kwa upande wa Tanzania, David Muthungu alisema mradi huo umeshaanza kufanyika na wanaendelea kutafuta wadau ambao watasaidia katika mradi huo ili waweze kufikia mikoa yote.
Pia alisema kuwa, kazi yao kubwa ni kusimamia mradi katika maeneo yaliyoanishwa kwa kujenga visima maeneo ambayo hayana maji na kutoa elimu jinsi ya kutumia maji ili waweze kuweka mazingira safi.
Muthungu alisema, watafanya tathimni katika mradi huo baada ya kukamilika na kutoa ripoti jinsi mradi huo unavyoendelea.
Hata hivyo alisema kuwa, mradi huo unahitaji uwezo mkubwa katika kuhakikisha unafanyika kwa usahihi ili waweze kumaliza kwa muda uliotakiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment