29 January 2013

Wazee waliopigana Vita ya Dunia wailaumu Serikali



Na Darlin Said

CHAMA cha Wazee Waliopigana Vita vya Pili ya Dunia hapa nchini (TCL) wameilaumu serikali kwa kuwatelekeza na kuwaacha wakihujumiwa mali zao.

Akizungumza na gazeti hili Katibu Mkuu wa (TCL), Sylvester Lubala alisema tangu chama chao kiundwe mwaka 1996 kimekuwa na misukosuko pamoja na kukosa ushirikiano kutoka serikalini hasa utetezi wa maslahi yao.

Alisema, kutokana na hali hiyo imesababisha kukosa ruzuku zao zinazotumwa kutoka 'Royal Common Wealth Ex-service League' (RCEL) kutokana na Serikali kutotilia mkazo wowote katika kushughulikia kuhusu pesa zao badala yake zinaliwa na wajanja wachache.

Mbali na hilo, Lubala alivitaja vitu walivyodhulumiwa ni pamoja na kuchang'anywa kwa ofisi yao iliyopo maeneo ya Fire Kariakoo.

1 comment:

  1. Kuna walakini mkubwa kuhusu jengo lao la Tanganyika Legion (Fire), jinsi lilivyouzwa. Wananchi wanapaswa waambiwe jinsi lilivyouzwa na waonyeshwe mkataba. Nashangaa wabunge, NGO na wanasiasa wamenyamaza kimya wakati wazee hawa wanatapeliwa na wachache wenye nguvu. Hii ni skandali kubwa

    ReplyDelete