27 June 2012

Kibanda, wenzake wasomewa maelezo ya awali




Na Grace Ndossa

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, jana iliwasomea maelezo ya awali Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Bw. Absalom Kibanda, mwandishi Bw. Samson Mwigamba na Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Bw. Theophil Makunga.


Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya kuchapisha makala ya uchochezi ambapo Wakili wa Serikali, Bi. Elizabeth Kaganda, ilidaiwa mbele ya Hakimu Bi. Waliarwande Lema, kuwa hazeti hilo toleo namba 2552, Novemba 30,2011, lilichapisha makala ya uchochezi kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Bw. Makunga anakabiliwa na shtaka la kuchapisha makala iliyoandikwa na Bw. Mwigamba katika safu yake ya Karamu ya Mwigamba iliyolenga kuwashawishi askari polisi na maofisa wa majeshi nchini kutoitii Serikali.

Bw. Kibanda anakabiliwa na shtaka la kupitisha makala hiyo ambapo Bw. Mwigamba akidaiwa kuiandika. Washtakiwa wote walikana mashtaka yao na kesi iliahirishwa hadi Agosti 7 mwaka huu.

Hakimu Lema alisema, washtakiwa wataendelea kuwa nje kwa dhamana kwa masharti yaliyotangulia.

No comments:

Post a Comment