29 June 2012

CHADEMA yajipanga kuandamana kupinga kupigwa Dkt.Ulimboka


Darlin Said na Tumaini Maduhu

CHAMA cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) kimejipanga kufanya maandamo makubwa kupinga kutekwa na kupigwa kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka.

Dkt. Ulimboka anadaiwa kutekwa usiku wa kumkia juzi na watu wasiojulikana.

Akizungumza na wananchi kwenye mkutano uliofanyika Karume Jijini Dar es Slaam juzi, aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbless Lema, alisema watu waliofanya kitendo hicho Serikali inawajua kutokana na kupigania haki za madaktari.

Alisema  kitendo hicho si cha kuvumiliwa, hivyo chama hicho kimeamua kuandaa maandamano ili kulaani kitendo hicho ambacho kimemsababishia majeraha makali.

"Utasema nchi yetu ni nchi ya amani huku wenzetu wakipata majeraha makali kwa kupigania haki za wenzao,tena kwa kukatwa kucha za mikono,"alisema, Bw Lema.

Alisema iwapo hali ya afya Dkt Ulimboka atabadilika, chama hicho kitafanya maandamano ya nchi nzima ili kuonesha umma kuwa kitendo kilichofanywa si cha kiungwana.

"Kwa kweli Dkt. Ulimboka alikuwa ni mpiganaji mzuri wa madai ya madaktari na maslahi ya wananchi, hivyo basi sisi kama wanaharakati tutahakikisha tunaonesha umma kuwa kitendo hicho si cha kiungwana," alisema Bw Lema.

Katika hatua nyingine Bw. Lema aliwahamasisha wananchi kuunga mkono mgomo wa madaktari kwa kile alichoeleza kuwa madai yao ni ya msingi.

"Hatuwezi kukaa kimya huku wabunge wakisaini posho nyingi bila yakuwa na huruma, hivyo basi sisi kama Chadema tutahakikisha tunaandaa maandano hayo ili kuishinikiza Serikali iwalipe madai yao, kwani kufanya hivyo ni kuwaogopesha wananchi wengine wasidai  haki zao," alisema,Bw. Lema.

6 comments:

  1. people's!!! Hongera sana CHADEMA. Ha2na wa2 wa kuikomboa nchi ye2 zaid ye2, naomba sana MUNGU awaumbue mafisadi katika nchi ye2! peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee's!............

    ReplyDelete
  2. Chaga Demonstration Movement (CHADEMA), sera yao ni Kumwaga damu, na hapatoshi na vurugu za kusababisha uharibifu wa mali na kupotea kwa maisha ya watu. Hawana kazi ingine ila kuzunguka mitaani kumwaga sumu kwa wananchi na kuwadanganya watu tunaandamna kupinga hiki, kupinga kile lazaidi hawana ni fujo tu.
    Huyu Godbless lema kavuliwa ubunge na mahakama kwa kosa la kutumia lugha chafu na kudhalilisha wagombea wa vyama vingine, pamoja na mambo mengine kufanya vurugu za kufa watu huko Arusha, sasa Arusha amepachafua kiasi hata watalii wanapewa onyo katika nchi zao kuwa Arusha si mahali salama, sasa badala ya yeye kubaki Arusha asafishe jina lake, ajitayarishe kukata rufaa au kugombea tena, anataka kuleta fujo zake Daresalaam.
    Yeye katika maandamano hayo anampinga nani? Au yeye na chama chake ndio waliomtumia watu Ulimboka wampige kisha wasingizie serikali? Maana inaelekea Chama chao kimefurahia sana Ulimboka kupigwa maana sasa wana ajenda za kupandia majukwaani na kuzungumza. Kuna kina Zitto walikuwa wanawaunga mkono madaktari kugoma, kapigwa kibaraka wao wanatoa wito madaktari upesi wakamhudumie Ulimboka, wameenda wakati wako kwenye mgomo huku wakiwapita wagonjwa wengine wakigumia na roho zao kama vile sio watu, kumtibia huyo Ulimboka ambaye ndio aliyekuwa akichochea migomo ya madaktari bila ya kujali ni athari gani zitawapata wananchi walalahoi, pamoja na juhudi zote zinazofanywa na Rais na serikali yake kuwapa upendeleo wa hali ya juu, hawana shukurani.
    Kwanza huyu Gobless Lema anajulikana kwa kuchangisha walalahoi kwenye mikutano yao, hana lolote kageuzi mikutano mradi.
    Ndugu zangu watanzania wenzangu msikubali kuzugwa hawana uzalendo wowote wapenda madaraka ya nguvu, wakotayari kutoa roho za watu wapeta madaraka, subirini 2015, na muombe Mungu huyo Ulimboka mlietaka kumtoa kafara apone, sivyo mtamla nyama.

    ReplyDelete
  3. naungana na msemaji aliyepita. hivi we Lema wakati ulipokuwa Bungeni hukujua kama ulikuwa unasaini posho nyingi? mbona hukukoma kuzisaini?
    leo umepigwa chini ndo unajifanya unaleta kauli za uchochezi mbona huku pigania haki za madaktari
    kipindi unasaini hiyo mihela? leo ndo unajifanya unahuruma.kwa taarifa yako hata mkiandamana haisaidii kitu mwishowe mtakubaliwenyewe kukameza moja na serikali kama vipi hata wote waache kazi serikali yetu inamkono mrefu inauwezo wa kufanya chochote na huduma zikaendelea kama kawa. ndo muwaajiri sasa hao madaktari mliowa ingiza mkenge.
    na nyie madaktari kwani ni mkubali kuendeshwa na chadema mwishowe mtaumia!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. KAMA SERIKALI ITAACHIA UCHOCHEZI HUU NITAISHANGAA NI MUDA MUAFAKA WAGONJWA WOTE WATOKE HOSPITALINI WAANDAMANE MABARABARANI KUPINGA MADAKTARI NA CHADEMA KUWATUMIA KAMA NGAZI YA KUPINDUA NA KULETE MAASI KATIKA NCHI HAPO NDIPO WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU WATAKAPOONEKANA NI WANASIASA AU WANATETEA HAKI ZA BINADAMU HAPA NDIO SERIKALI IWAONYESHE KUWA IPO KIHALALI IWAPO MAHAKAMA KUU HAITACHUKUA HATUA KUKOMESHA YA KICHOCHEZI BUNGENI NA SERIKALI INAPUUZIA KITAKACHOTOKEA TANZANIA HISTORIA ITAWAHUKUMU KUWAACHIA FREEMASON WANYWE DAMU ZA WATANZANIA

    ReplyDelete
  5. Namsifia mchangaji wa kwanza, mliofuatia nina wasi wasi na nyie na sijui kama ni raia wa Tanzania, au kama mlienda shule basi mlikuwa mnasikia mnachofundishwa lakini mlikuwa hamelewi!!! Basi kama mlikuwa mnaelewa nafikiri mlielewa kwamba kama HERUFI A=B=C basi hamkuelwea kama kumbe A=C na C=A na B=A na A=B!!!!
    Basi tujibu watanzania 1+1-1+0=0+1-1+1=? Jibu mtakalopata basi ninyi mtakuwa wamoja na serikali.

    ReplyDelete
  6. wote mlioongea hapo juu ni vibaraka wa ccm maana hamjui haki zenuau ni miongoni mwa mafisadi wa nchi hii ndiyo maana hamuelewi. Msiwe kama akina Mgwelu bungeni kazi yake kusema wapinzani hawana shule. Hilo sio kweli wana shule nzuri hata kushinda ya ccm. Hicho ni kilio cha samaki ukweli utajulikana 2015. Freemason ni CCM ndio wanaopiga wanachi risasi bila sababu wakati wanadai haki. Hata raisi alishatamka wakigoma damu itamwagika, wengine virungu

    ReplyDelete