Na Pendo Mtibuche, Dodoma
SERIKALI mkoani Dodoma imesema suala la upandaji holela huduma za matibabu ya afya chini ya mifuko ya afya ya jamii NHIF na CHF limekuwa likiathiri utendaji wa mifuko hiyo.
Hali hiyo imedaiwa kutokana na wauzaji wa dawa na watoa huduma kubadilisha
bei ya dawa wanavyotaka na kwa wakati wowote.
Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Rehema Nchimbi wakati akifungua kongamano la siku moja la wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Dodoma.
Alisema, sekta hiyo ya afya imekuwa ikikabiliwa na changamoto nyingi ambazo ambazo zimekuwa kuongeza malalamiko mengi kuhusu ukosefu wa dawa katika vituo vingi vya Serikali na hasa vilivyopo ndani ya Manispaa ya Dodoma na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa.
Alisema, kutokana na suala hilo kuwa nyeti basi ipo haja ya Serikali
kulitazama kwa makini suala hilo na kulitafutia ufumbuzi.
Mbali na changamoto hiyo ya kupanda kwa bei ya matibabu, lakini pia Mkuu huyo wa mkoa alibainisha kuwa pia kumekuwepo na vituo vya afya ambavyo vina uhaba wa watoa huduma wenye sifa hasa vijijini, hivyo suala hilo linasababisha utoaji huduma hafifu zisizokidhi kiwango kinachotakiwa kwa wanachama.
Alisema, hali ya afya katika Mkoa wa Dodoma inahitaji kufanyiwa tathimini ya uhakika ili kuona ni njia zipi zitakazoinua mifuko hiyo miwili ya afya ya jamii yaani NHIF na CHF ili iweze kufanya vizuri.
No comments:
Post a Comment