Na Amina Athumani
BAADA ya kukithiri vurugu katika mechi mbalimbali za soka katika wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, serikali imeongeza faini kutoka sh. milioni tano hadi sh. milioni 10 kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), endapo kutatokea uharibufu wowote utakaosababishwa na mashabiki.
Hatua hiyo ya serikali, imekuja baada ya hivi karibuni kutokea vurugu katika mechi ya Kombe la shirikisho katika Simba na Kiyovu ya Rwanda na nyingine ya Ligi Kuu Bara, kati ya Yanga dhidi ya Azam FC, ambapo mashabiki walivunja viti vya uwanja huo na kusababisha hasara.
Akizungumza Dar es Salaam jana, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara hiyo, Leonard Thadeo alisema adhabu hiyo imepandishwa kwa TFF na itawajibika kulipa sh. milioni 10 kwa ajili ya matengenezo na gharama ya ununuzi wa mali itakayopotea au kuharibika.
Alisema katika mara zote uharibifu ulipokuwa ukijitokeza katikia uwanja huo, serikali imekuwa ikichukua hatua ya kufanya matengenezo bila kulazimika kuwahusisha wadau wengine.
Thadeo alisema kwa sasa inaonekana uharibufu huo unajengeka kuwa tabia, miongoni mwa baadi ya mashabiki wa soka nchini.
"Hatua hii haiwezi kuvumilika, kwani inasikitisha zaidi kuona kuwa hata baadhi ya viongozi wa klabu hawatambui kuwa kuna wajibu wa msingi kama viongozi, kuwaelimisha wanachama na wapenzi wa klabu zao kuacha uharibifu na badala yake ndiyo wanaosema kuna viti vingi vimeharibika, kaharibu nani?
"Viongozi tutambue wajibu wetu kwa wale tunaowaongoza, kwani wizara haitasita kuufunga uwanja endapo tabia hiyo ya uharibifu itaendelea," alisisitiza Thadeo.
Thadeo alisema, ili serikali isifikie hatua hiyo amewataka wapenzi wa soka kutoa ushirikiano wa kuhamasishana na kuelimishana, kushabikia na kushangilia timu kwa amani na utulivu, ili kuimarisha uzalendo na kuthamini rasilimali za taifa kwa faida ya kizazi kijacho.
Alisema ni dhahiri vurugu zinazoendelea kujitokeza, zitaweza kuwakatisha tamaa kwa kuwa uwanja huo umejengwa na serikali kwa msaada wa Serikali ya Watu wa China na kwamba kwa sasa kuna wataalamu, wanaoendelea kusaidia uendeshaji wa kazi uwanjani hapo.
Mtu akikutwa anaharibu kiti apigwe risasiharadhani, wengine hawatarudia ustaabu ni kitu cha bure hivi kwanini mijitu bado mishamba tu tutandelea lini TANZANIA?
ReplyDelete