*Wanaharakati wajiandaa kufungua kesi, waanza kuandaa vielelezo
*Wadai mgomo ulisababisha vifo vya watanzania wasiopungua 300
Na Mwandishi Wetu
SIKU chache tangu Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), kitangaze kusitisha mgomo na kurudi kazini kwa kile walichodai kumheshimu Rais Jakaya Kikwete, baadhi ya wanaharakati nchini wamepinga kitendo cha madaktari kufanya mgomo huo.
Wakionesha kukerwa na msimamo wa madaktari ili kuishinikiza Serikali iwaondoe madarakani Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda na Naibu wake Dkt. Lucy Nkya, kwa madai wao ndio chanzo cha migomo iliyofanyika kwa vipindi viwili tofauti, wanaharakati 36 wameazimia kuwafikisha mahakamani madaktari wote walioshiriki katika mgomo huo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwenyekiti wa kamati iliyoundwa na wanaharakati hao Bw. Godfrey Mosha, amesema mgomo wa madaktari umesababisha hasara kubwa kwa Taifa pamoja na vifo kwa Watanzania wengi wasio na hatia.
“Kimsingi mgomo huu haukufuaata taratibu hivyo si halali kama wanavyodai madaktari, kitendo walichofanya si cha kiungwana ambacho wanasheria hawawezi kukivumilia.
“Kamati yetu ipo katika hatua ya kuandaa vielelezo ili tuweze kufungua kesi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi ili wote waliogoma wawajibishwe iwe fundisho kwa makundi mengine ambayo hayana nia njema na Taifa lao,” alisema Bw. Mosha.
Aliongeza kuwa, Tanzania ni nchi ya amani na utulivu hivyo dhamira yao ni kudai haki iliyokiukwa na watu waliolewa madaraka kwa nafasi walizopewa na Taifa.
“Lazima haki hii ipiganiwe na wanaharakati wote wenye nia njema na nchi yao, kamati hii inaundwa na wadau wa mazingira, madaktari wastaafu na wanasheria.
“Tumegundua mgomo wa madaktari ulisabisha vifo vya watu wasiopungua 300, wenyewe wakiendelea kusaini vitabu vya mahudhurio na kupokea mishahara bila kufanya kazi,” alisema.
Aliongeza kuwa, mbali ya mgomo huo kutofuata taratibu, madaktari hao walikataa kukaa mezani ili kujadili maadai yao na Serikali wakiamini wao ni kundi muhimu kuliko wengine nchini kama jeshi, polisi na walimu.
Bw. Mosha alisema Watanzania wengi wanaamini kitendo cha madaktari kukataa mazungumzo na Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda kimeonesha dharau kwa kiongozi huyo kama watumishi wa umma na wasomi.
Alisema kamati hiyo inampongeza Rais Kikwete kwa kufikia muafaka na madaktari ambao wamerudi kazini kuendelea na kazi ili kuokoa maisha ya Watanzania.
Aliongeza kuwa, watumishi wa Serikali katika taasisi mbalimbali wanapaswa kuwa na uzalendo kwa nchi yao ili kuharakisha maendeleo ya sekta mbalimbali, kudumisha amani na utulivu.
Mgomo kama mgomo lazima uwe na matokeo. Sijui hawa waatalamu wa afya ya binadamu waliotaka matokeo gani kwani vifo ya watu 300 sio jambo la kujivunia hasa ukizingatia kuwa ni watu hawa hawa ndio walio kuwa na vipaji na ujuzi wa kuokoa au kuzuia vifo hivyo.
ReplyDeleteLakini pia kuna jambo jingine ambalo tusisahau kuwa kuna chimbiko au chanzo kingine ambayo itakuwa hawa wataalamu waliona kuwa ni bora kugoma na kuhatarisha maisha ya watu zaidi ya mishahara.
Najiuuliza kama sio mishahara basi ni nini?
Kwa hiyo natupia lawama serikali na wadau wake kwa kupunguza kasi katika kuhudumia na kusimamia sekta ya afya kwa ujumla.
Nahisi kama wange jaribu kuhakikisha kuwa hospitali na vituo vya afya nchini viko sawa na tayari kwa kutoa huduma ikiwa na pamoja kuweka vifaa na upatikanaji wa dawa. Naamini kuwa wadakatari wengi wamechafanya kazi bila kulipwa kila wanachostahaili kwa muda mrefu na huenda mazingira ya kazi nayo ndio chanzo cha hofu na huduma duni.
Naungana na mchangiaji hapo juu. La muhimu walichokuwa wanadai Madaktari ni heshima yao. Rais wetu alitumia busara zake akawaita Madaktari akaa nao. Mbonna walimsikiliza na uelewano ukatawala?
DeleteNyie Mawaziri wawili, tumieni ujasiri wa Rais wetu. Jishusheni hata muwatake radhi hawa Madaktari. Mkiomba msamaha kwa sababu ya matamshi yenu au dharau mliyowafanyia hamtapungukiwa na lolote. ondoeni kinyongo kati yenu (Mawaziri na Madaktari) Haitawezekana kuwatumikia hawa madaktari wetu ikiwa mnawadharau na kuwakejeli.
Madaktari wanafanya kazi zao kutumia mikono ya Mungu. Wanawacchana wagonjwa na wanapona! Hakuna yeyote ambaye haendi kwa Daktari. Awe Rais au Mchungaji.
Kama ni wakupelekwa Mahakamani ni hawa Mawaziri wawili na si vinginevyo.