14 March 2012

Elimu kwa wananchi kikwazo upangaji miji

 Mkazi wa kijiji cha Homboza Wilaya ya kisarawe Mkoa wa Pwani Bw.Ally Mwinyimkuu, akichangia mada katika mkutano, wa wananchi na viongozi wa halimashauri, kuhusu majadiliano ya uanzishwaji wa mipango Miji kijijini hapo hivi karibuni.(Picha na Prona Mumwi)

Na David  John
UTARATIBU  mbovu katika upangaji wa miji barani Afrika ni miongoni mwa mambo yanayokwamisha kasi ya maendeleo barani humo.

Katika miji suala la upangaji miji limekuwa likipigiwa kengele siku nyingi hata pasipo kujua ni lini litaanza utekelezwaji wake.

Lakini wakati michakato ikiendelea serikalini kwa kushirikiana na mataifa mengine hali ya wananchi wa Tanzania kiafya, Elimu na hata maendeleo inazidi kudidimia.

Pamoja na madhara hayo wananchi wengi wamekuwa wakihofia utekelezwaji wa mpango huo kutokana na kukosa elimu juu ya faida ya upangaji miji.

Licha ya serikali kutaka nchi iwe katika  kupanga miundombinu mizuri katika mtiririko wa  mipango miji hali hiyo inaonekana kupokelewa kwa hisia tofauti na wananchi mbalimbali nchini huku wakihofia kunyang'anywa maeneo yao.

Pia wamekuwa wakihofia kupewa kipato kidogo ambacho hakikidhi haja ya eneo husika la mwananchi huyo.

Hali hiyo imezidi kujitokeza zaida katika baadhi ya mikoa huku viongozi husika wakikumbana na maswali mengi kutoka kwa wanakijiji kuhusu mchakato huo.

Hivi karibuni nilipata fursa ya kuhudhulia moja ya kikao cha wananchi wa kata ya Upanga Mashariki iliyopo katika mansipaa ya Ilala mkoani Dar es salaam.

Katika kikao kile palizuka hoja ya kuitaka serikali kuacha mala moja kuweka mpango miji na hasa katika ujenzi wa magolofa katika eneno hilo wakati wakzi wengi wako nanumba za chini.

Pia, ikiwaambiwa kwamba, mpango huo kwa Manispaa hiyo haufai kutokana na kukosekana kwa nafasi ya kufanya hivyo, wakashauri kutafuta njia nyingine ya kuboresha mazingira hayo.

Wakati wananchi hao wakidai hayo hali imekuwa tete kwa wananchi wa kijiji cha Homboza kilichopo Wilaya ya  Kisarawe, Mkoani Pwani   ambapo wameigomea halmashauri hiyo kuingiza mfumo huo katika kijiji chao.

Wananchi hao wanasema kuwa, wao hawana haja ya kuona kijiji hicho kinakuwa katika mpango mzuri na hata serikali ina lengo zuri.

Wanasema kuwa, kijiji hicho hakiwezi kuwa hivyo kwani wanatambua wakikubaliana na sera ya serikali watadhurumiwa haki zao kwa maana wanahistoria nzuri ya serikali yao.

Hivi karibuni, wataalamu wa ardhi walifika katika kijiji hicho kwa lengo la kupima viwanja, hali ilisababisha hofu kubwa baina yao na uongozi wa Wilaya hiyo.

Walidai kuwa, uvamizi wakuchukua maamuzi ya kufanya jambo hayakuwa na makubaliano wala elimu kwa wananchi kuhusu linalotaka kufanyika kijijini hapo.

Kutokana na hali hiyo wananchi walikosa imani na viongozi wao na kutaka kukutana na viongozi wa juu wa Wilaya ikiwa pamoja na Mkurugenzi,  Mbunge, Mkuu wa Wilaya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ili kupewa ufafanunuzi kuhusu uvamizi huo bila wao kushirishwa kwa zoezi liliotaka kufanyika.

Maswali mengi kwa Mwenyekiti Ng'mbi yalihusu kutoshirikishwa kwa wananchi hao katika mvhakato wa mpango huo na kutopewa taarifa mapema.

Wananchi wengi walihoi uhalali wa mapngo huo na ukimya wa viongozi hao ambapo, walitaka ufafanuzi ili kujua hatma yao.

Akitoa malalamiko, makazi wa kijiji hicho Bw. Ally Mwinyimkuu, anasema, hatua ambayo halmashauri wameifanya siyo sahihi ya kuvamia eneo ambalo linakaliwa na watu na kufanya kama halina watu kiasi cha kujichukuliwa maamuzi mkononi.

Anasema, mapungufu ya halmashauri kunyimwa ushirikianao na wananchi wa kijiji hicho ni kutokana na kukosa elimu ya suala hilo kabla ya kufanya uvamizi.

Anasema, unapotaka kufanya jambo lolote hasa linalolenga mazingira ya wananchi lazima pawepo na ushirikiano ili kunusuru hali ambayo inajitokeza katika maeneo mbalimbali nchini na kubwa katika eneo hili la ardhi.

Mwenyekiti wa halmashauri Bw. Adamu Ng'imbi  alikutana na changamoto za wananchi hao ambao walikuwa na jazba ya kutoona viwanja vyao vinachukuliwa bila utaratibu.

Bw. Ng'imba anasema kuwa, matatizo ya ardhi ndani ya nchi yamekuwa makubwa na bila kufanyika jitihada za makusudi serikali itaendelea kupata migogoro ya ardhi.

"Ni kweli kwamba halmashauri ya kisarawe iko katika mkakati wakuweka mji kuwa wa kisasa na tayari baadhi ya maeneo yamepimwa," anasema.

Anasema, kutokana na hatua hiyo vijiji karibia vitatu wameshafanya hivyo na lengo hasa ni kutaka kuwaboreshea wananchi mazingira ya kuingia katika soko zuri hata watakapo taka kuuza meneo yao wapate fedha nzuri.

Anasema, kilichotokea katika kijiji hicho kwamba, ilikuwa ni mapema kuendesha zoezi lolote kuhusiana na upimaji wa ardhi ya ambayo inamilikiwa na wananchi bila kuwashirikisha.

Hata hivyo hakuna hofu kwa wananchi kwani zoezi hilo halikuwa endelevu na halitaendelea tena mpaka pale utaratibu mwingine utakapo fanyika.

Bw. Ng'imba anasema kuwa, yalikuwa ni makosa ambayo yamefanyika kutoshirikisha wananchi kuhusu sakata hili , "Ninochoweza kusema ni kwamba wananchi wa homboza kuweni watulivu na msiwe na wasi wasi kuhusu hili litafanyiwa kazi," anasema.

Anaongeza kuwa lengo la halmashauri ni nzuri kwa maana inatakiwa wananchi wawe na faida ya ardhi yao kwa sababu, miaka ijayo bila viwanja kupimwa watu watauza kwabei ya kutupa lakini kama vitapimwa watapata faida kubwa.

"Mpango wetu ni kuweza kuwasaidia wananchi wetu hasa wa kijiji hiki, jamani bila kupima eneo hili litakuwa kama Majohe ilivyo sasa "anasema

Anasema, majohe kwa sababu ya kutoingia katika mpango miji leo imejegwa kiholela na kukosa kuifanya ionekane kama uchafu kwa kukosa baadhi ya huduma za jamii.

Anasisitizia wananchi hao kuwa, maeneo yao yako salama na hakuna atakaye vamia bila kuwepo na utaratibu wa muongozo wa halmashauri hiyo.

Amewahaidi kuwapa elimu zaidi wananchi hao mpango huo utakapo kamilika ili kuweza kuwa na imani nao ambapo itawezesha wananchi hao kuwa katika ramani bora , na hiyo nikutaka kuweka mazingira yaliyokuwa.

Anasema, ifike hatua wananchi waelewe adhma ya serikali siyo kwa faida ya jamii, na kuongeza kuwa mabadiliko hayana budi kufanyika kama taifa linahitaji maendeleo ya kweli.

Mbunge wa Jimbo hilo Bw. Selemani Jafu, aliwahakikishia wananchi kutokuwa na hofu kwani hakuna jambo na hasa kubwa kama la ardhi kufanyika bila kushirikisha wananchi.

Amewataka wananchi kusaidia na kushiriki kufanya mabadiliko ya katika kushiriki kikamilifi ili kuweza kupata katiba inayohitaj maoni yao.

Mpango miji ni hatua nzuri ya kuleta maendeleo nchini, wahusika wanatakiwa kutoa elimu kwa wananchi ili kurahisisha kazi hiyo na kuepusha migogoro.

Sheria ya Mipango miji kifungu cha 24 (2) kinamtaka Mkurugenzi wa Mipango miji kutangaza eneo la mradi kutokuendelezwa kwa miaka miwili hadi mpango kamili utakaporidhiwa.






















No comments:

Post a Comment