16 March 2012
Elimu duni kwa wazazi chanzo ukatili kwa watoto
Wanafunzi wakiwa wamekaa chini kwa kukosa madawati,baadhi ya wazazi hugoma kuchangia michango ya vifaa shuleni (Picha naMtandao)
Na George Boniphace
AJENDA ya ulinzi kwa mtoto imekuwa ni jambo muhimu kote duniani, ikiwemo Tanzania kwa kuungana na Umoja wa Afrika na Jumuiya ya nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara
(SADC).
Pia, inaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuhakikisha kuwa mtoto wa tanzania anakuwa huru dhidi ya unyanyaswaji, ukatili, unyonywaji au utelekezwaji.
Shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa UNICEF, limetambua juhudi hizo na kulipatia kipaumbele kwa kuandaa mpango mkakati katika kumlinda mtoto popote alipo.
Imeanzisha sera ya 'Child protection Strategy' 2008 yenye lengo la kuhakikisha kuwa, watoto wanapata haki ya msingi ya kuishi, kuendelezwa na ustawi wa maisha yao ili watakapokuwa watu wazima waweze kuwa raia wema wenye kujua haki na wajibu wao wa
kizalendo kwa taifa lao.
Tanzania, kama nchi mwanachama wa umoja wa mataifa, imeridhia mikataba mbalimbali yenye lengo la kumlinda mtoto dhidi ya ukatili, unyanyaswaji, unyonywaji au utelekezwaji, miongoni mwa mikataba hiyo ni pamoja na fungamano la Afrika.
Tanzania imeridhia pia tamko la Shirika la Kazi Duniani (ILO) namba 182 linalowataka nchi wanachama kukomesha aina mbaya ya utumikishwaji wa watoto katika shughuli za uzalishaji mali au biashara ya ngono.
Katika kuifanya mikataba au matamko hayo kuwa na nguvu kisheria hapa nchini, imefanikiwa kuendesha mchakato uliolenga kupatikana kwa sheria ya mtoto kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali nchini.
Mwishoni mwaka 2009, Bunge la Tanzania lilitunga sheria ya mtoto ambayo pia Rais wa Kikwete ameridhia.
Kinachosubiliwa kwa sasa ni ukamilishwaji wa kanuni zitakazowaongoza watekelezaji wa sheria hii unaofanywa na Wizara ya Afya ustawi wa jamii.
Nchini, zaidi ya asilimia 50 ya watu wote ni watoto walio chini ya umri wa miaka 18, na ikiwa inapambana kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, ripoti ya sensa ya kitaifa ya watu na hali ya maisha iliyofanyika inatoa kadirio la asilimia 10 ya watoto wote kuwa ni wale waishio katika mazingira magumu wakiwemo yatima.
Hata hivyo, kamati maalumu ya haki kwa watoto, ya umoja wa mataifa kilichokaa mwaka 2006, kilionesha kutoridhika kwake na juhudi zilizokuwa zimechukuliwa na serikali ya Tanzania kumlinda mtoto dhidi ya unyanyaswaji, ukatili, unyonywaji na utelekezwaji.
Sehemu ya ripoti hiyo inaeleza kuwa "Bado watoto wa kike wanaolewa wakiwa na umri mdogo wengi wao chini ya miaka 18, uwepo wa adhabu kali ya viboko shuleni, vifo kwa watoto walio chini ya miaka 5, kuwepo kwa watoto wengi wanaotumikishwa kutoka sehemu za kazi na ongezeko la biashara ya ngono hasa katika miji
mikubwa.
Mbali jitihada mbalimbali zilizofanywa na serikali, wanaharakati, azaki na asasi mbalimbali nchini, bado ajenda ya ulinzi kwa mtoto haijapata msukumo unaotakikana kwa ngazi zote hapa Tanzania.
Vijijini kwa mfano, ukiukwaji wa haki za watoto umejikita zaidi katika baadhi ya mila zinazowalazimisha watoto kuolewa mapema ikiwa ni pamoja na kurithiwa pindi wenza wao wanapofariki, ukiukwaji wa haki za watoto wenye ulemavu, watoto wa kike dhidi ya wale wa kiume.
Mtafaruku katika familia ikiwa ni pamoja na talaka au utelekezwaji wa watoto, usafirishaji, mimba za utotoni, lakini kubwa zaidi ni ukosefu wa mifumo na miundo imara kwa
ngazi zote zitakazosaidia kuzuia au kuitikia maswala mbalimbali yanayowakandami.
Kuhusu msingi wa ajenda ya ulinzi kwa mtoto, Mei mwaka 2010 shirika la kuhudumia watoto la umoja wa mataifa (UNICEF) wakishirikiana na Taasisi ya ustawi wa jamii, Dar es Salaam walifanya utafiti kuhusu maono, tafasiri, uelewa na tabia za watu juu ya dhana nzima ya ulinzi kwa watoto nchini.
Utafiti huu ulilenga kufahamu ni kwa jinsi gani watoto wanalindwa na jamii ikiwa ni pamoja na kuangalia uimara wa mifumo na miundo iliyopo au inayopaswa kuwepo nchini kwa ajili ya ulinzi wake.
Utafiti huu ulifanywa katika wilaya tatu za kujifunzia, ikiwemo wilaya ya Magu (Mwanza), Hai (Kilimanjaro) na Temeke (Dar es Salaam).
Pia uliiwezesha UNICEF na Taasisi ya ustawi wa jamii kuibua mambo
mengi ambayo taifa na jamii inapaswa ikae chini na kujadili kwa
mapana na marefu ili ije na agenda mbadala na ya muda mrefu juu ya
matatizo sugu yanayowakabili watoto nchini.
Kupitia utafiti huo ilibainika kuwa, nchini ipo mifumo inayomlinda mtoto katika jamii, tatizo kubwa lililojitokeza ni kuwa
mifumo na miundo hiyo haipo imara katika kuzuia au kuitikia masuala
mbalimbali yanayowahusu watoto.
Kufuatia hali hiyo, UNICEF wakishirikiana na Taasisi ya Ustawi wa Jamii wameibua mradi wa Uimarishwaji wa Miundo na Mifumo kwa ajili ya ulinzi wa Mtoto Tanzania.
Mifumo na miundo inayokusudiwa kuimarishwa ni pamoja na familia, kutokana na kwamba ni jukumu la msingi la kila familia kuhakikisha kuwa ulinzi kwa mtoto ikifuatiwa na jamii pamoja na serikali kutoa ulinzi wa kisheri.
Akielezea uhalisia wa jambo hilo, mwakilishi wa UNICEF nchini, Bw.
Sunguya Francis anaeleza kwamba, wana imani kuwa mifumo hiyo ikiimarishwa kikamilifu itasaidia kuzuia au kuibua masuala
maalumu yanayowakumba watoto.
Anasema, utafiti huo ulilenga pia kupima uelewa wa wananchi kuhusu maswala ya ulinzi kwa mtoto, wilaya ya Magu ilionesha uelewa mkubwa, ambapo zaidi ya nusu asilimia 57 ya wahojiwa wote walionesha kufahamu.
Anasema kuwa,pamoja na uelewa huo bado kuna tatizo kubwa, kuwa ama jamii inapuuza jambo hili au tabia na mitazamo haijabadilika licha ya kuelewa.
Bw. Francis anasema kuwa, kimsingi tatizo la mitazamo ya wana jamii kuhusu ukatili, unyanywasaji, ukatili dhidi ya watoto halina budi lishughulikiwe mara moja.
Kutokana na tafsiri yake, ni kwamba juhudi zinahitajika ili kuweka mikakati ya maksudi kuanzia ngazi ya familia, kitongoji, kijiji, kata, tarafa wilaya, mkoa na hatimaye ngazi ya
Taifa.
Anasema uelewa huo ni muhimu kutokana na sababu ambazo anazitaja kuwa ni pamoja na kesi zinazohusiana na mtoto kutendewa ukatili zitolewe taarifa mapema katika vyombo husika na hivyo
mtoto aweze kupata msaada mapema na pia jamii yenyewe inakuwa inajengewa uwezo wa kukemea na kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Utafiti pia umebaini kuwa, penye uelewa kuhusu ukatili, unyanywasaji, unyonywaji na utelekezwaji wa watoto kumekuwa na mabadiliko katika utoaji wa taarifa kwa maana ya kutolewa kwa wingi zaidi.
Mradi unalenga, kuimarsha malezi yenye msingi wa kifamilia Kimsingi hii ndiyo shabaha kuu ya katika wilaya ya Magu. Ni ukweli usiopingika kuwa bado kuna tatizo kubwa la wazazi na walezi kuwatelekeza watoto na familia zao.
Hali hiyo imewafanya watotot wengi wajitumbukize katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zenye kuwaonya kama vile machimbo ya almasi, mashamba makubwa ya kilimo ambako hufanya kazi kama vibarua na pia katika sehemu ambako shughuli za uvuvi hufanyika ziwani.
Hii ni hatari zaidi kwa watoto wa kike ambao hujikuta wakijiingiza katika vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo, vitendo vinavyofanywa mara nyingi bila ya kinga kutokana na uelewa mdogo au masharti wanayopewa na wateja wao ikiwa ni sharti mojawapo la kupata ujira mkubwa).
Hali hii imekuwa chanzo cha mimba za utotoni, kuolewa katika umri mdogo, kupata magonjwa ya zinaa ikiwa ni pamoja na gonjwa hatari la UKIMWI.
Anasema, kuwa ongezeko la vitendo vya wazazi kuwatelekeza watoto wao linahitajii nia ya dhati itakayolenga kuimarisha familia kama
taasisi hasa zile zenye viashiria vyenye kupelekea viatarishi kwa watoto.
Pili, mradi huo unakusudia kuwaelimisha wana jamii kuhusu umuhimu wa kuwalea watoto katika familia, hii inatokana na matokeo ya utafiti yaliyobaini kuwa, wanaolelewa kwenye vituo vya kulelea watoto siyo yatima wanatakiwa katika kundi la watoto waishio kwenye mazingira magumu.
Vituo vingi vya kulelea watoto vimeanzishwa kibiashara, na kwamba watoto wamekuwa wakitumika kama chambo cha kujipatia fedha toka kwa wahisani.
Wazazi wanaodhani kuwa wanasaidiwa kulelewa watoto wao ikiwa ni pamoja na kuahidiwa kupatiwa elimu bure kwa ngazi
zote, wameichukulia hali hiyo kama msaada mkubwa kwao bila kujua madhara yanayowapata watoto hao.
Anasema kuwa vituo vingi wilaya ya hai kwa mfano inakadiriwa kuwa na vituo 22 vinavyojishughulisha na ulezi wa watoto bila kujali yatima au walio na wazazi.
Anasema kuwa, jamii ni sehemu mojawapo inayowajibika kwa sehemu kubwa kuhakikisha watoto wanakuwa salama, lakini vyombo vilivyoanzishwa kisheria, kama taasisi vina jukumu katika kusimamia haki za watoto.
Anasema, ukosefu wa elimu kwa wazazi ni moja ya kikwazo kumaliza unyanyasaji kwa watoto kwa kuwatumikisha na kuwanyima haki zao za msingi.
UNICEF/ISW, 2010 inaonesha kuwa, vyombo vinavyohusika katika kulea watoto hasa wale wanaohitaji kuwa na uangalizi wao ndio wanaokuwa katika hali ya hatari zaidi ya kutendewa ukatili huo hivyo serikali haina budi kulivalia njuga suala hili ili kukomesha ukatili huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment