NAIROBI,Kenya
WAKATI wananchi katika kila pembe ya dunia jana waliadhimisha siku ya wapendao maarufu kama Valentine Day, kwa stahili mbalimbali,hali hiyo ilikuwa tofauti nchini kwa wanaume nchini Kenya, baada ya kulalamika kuhusu kunyanyaswa na wake zao.
Kulingana na Mwenyekiti wa Chama cha kutetea Haki za Wanaume nchini humo,Bw. Nderitu Njogu, idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka mno.
Bw Nderitu alisema juzi kuwa utafiti wa chama chake umeonesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwasabibisha kuwadharau wanaume.
Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawake wengi sasa wana kipato kikubwa kuliko waume zao.
Mwishoni mwa wiki Polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri mkoani kati, baada ya kumshambulia mumewe na kumjeruhi vibaya kwa panga.
Mwanamume huyo bado anapata matibabu hospitalini baada ya kukatwa katwa usoni na uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.
Bw. Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwaka jana na kwamba utafiti wa shirika lake unaonesha kesi nyingi za wanaume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika Mkoa wa Kati.
"Siku hii ya Valentine na washauri wanaume wasikubali kunyanyaswa na wake zao, kwa kufanya matumizi makubwa kuliko na wanayoweza kumudu" alisema Bw. Nderitu.(BBC).
No comments:
Post a Comment