TEGUCIGALPA,Hondura
WAFUNGWA wapatao 272 wameripotiwa kufa nchini Hondura,baada ya moto mkubwa kuzuka ghafla gerezani.
Habari kutoka nchini humo zilieleza kuwa moto huo ulizuka ghafla juzi katika mji wa Comayagua,uliopo katikati mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo baadhi ya wafungwa walijinusuru baada ya kuvunja dari na kujirusha kutoka juu ya paa la nyumba.
Taarifa hizo zilieleza kuwa moto huo ulizuka Juamnne jioni na iliuchukua zaidi ya saa moja kuudhibiti.
Msemaji wa kikosi cha zima moto katika mji huo wa Comayagua,Bw.Josue Garcia,alisema kuwa hakli ilikuwa taharuki katika gereza na baadhi ya askari magereza walilazimika kutimua mbio ili kujinusuru.
"Tusingerweza kuwatoa nje kwa sababau tulikuwa hatuna funguo na hatukuweza kumpata askari aliyekuwa nao,"alisema.
Naye Bi.Lucy Marder,ambaye ni mkuu wa kitengo cha maafa katika mji wa Comayagua, alisema kuwa taarifa zinaonesha kuwa watu 272 wamekufa.
Gereza hilo la mji wa Comayagua, lipo umbali wa kilometa 100 Kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Tegucigalpa,na lina uwezo wa kuchukua wafubngwa zaidi ya 800.(BBC)
No comments:
Post a Comment