Na Amina Athumani
MCHAKATO wa Mchaguzi Mkuu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), unatarajia kuanza Oktoba mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHANETA, fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi zitaanza kutolewa mwanzoni mwa Oktoba, huku uchaguzi ukitarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.
Akizungumzia mchakato huo Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi alisema chama hicho kitapata viongozi wapya mwishoni mwa mwaka huu, hivyo wadau wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wajitokeze mara baada ya kutangazwa mchakato wa uchaguzi huo.
CHANETA ambayo Mwenyekiti wake Anna Bayi, anayemaliza muda wake, alitangaza dhamira kutogombea uongozi katika uchaguzi ujao ili kutoa nafasi kwa wadau wengine, wenye uchu wa maendeleo waweze kuongoza.
Viongozi wengine wanaomaliza muda wao katika chama hicho ni Makamu Mwenyekiti Shy-rose Banji, Katibu Mkisi, Mhazini Rose Kisiwa na Wajumbe ni Damian Chonya Marry Protus.
No comments:
Post a Comment