Na Mwali Ibrahim
BONDIA Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' amesema kuwa pambano lake kati ya Nasib Ismail litakalokuwa miongoni mwa mapambano ya utangulizi katika Francis Cheka na Kalama Nyilawila ndio litatumika kuwa mazoezi ya kumuadhibu Rashid Matumla.
Maneno na Matumla wanatarajia kupanda ulingoni Februari 25 katika pambano la marudiano litakalofanyika katika ukumbi wa PTA, Saba saba Dar es Salaam.
Mabondia hao wanarudiana baada ya kushindwa kutambiana katika pambano lao lisilo la ubingwa lilofanyika sikukuu ya Krismas, Mtonikijichi ambapo Maneno hakuridhishwa na matokeo hayo ya Droo ambapo pambano hilo litakuwa ni pambano lao la nne.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno alisema pambano hilo la Janurai 28 litakuwa ni sehemu ya kuonyesha kiwango chake kwani hata bondia huyo atahakikisha anamtwanga vilivyo.
Alisema, kwa sasa anaendelea na mazoezi katika kambi yake iliyopo katika ukumbi wa kwa Rich uliopo Kongowe chini ya kocha wake Chaurembo Palasa ambaye nae atakuwa ni mmoja kati ya mabondia watakao wasindikiza Cheka na Nyilawila.
Mapambano ya utangulizi katika pambano lao hilo yatakuwa ni kati ya Mikidadi Abdalah na Shomari Mirundi, Abdalah Mohamed akiwa na Salehe Mkalekwa.
No comments:
Post a Comment