Na Mwali Ibrahim
MKUU wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pambano
lisilo la ubingwa kati ya Francis Cheka na Karama Nyilawila, litakalofanyika katika Uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo linatarajia kuwa la uzito wa kg. 75 raundi 10, ambalo litafanyika Januari 28, mwaka huu.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa njiani kwenda Morogoro jana, Promota wa pambano hilo Philemon Kyando 'Don King' alisema tayari mabondia hao wameshapima afya zao kwa awamu ya kwanza.
"Niliwapeleka katika Hospitali ya Hindumandar, Dar es Salaam kabla sijapata dharura na hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya na kuangaliwa afya zao kwa ujumla na hii ni hatua ya kwanza, lakini nitawapima tena Januari 27 mwaka huu kabla ya kupanda ulingoni," alisem Kyando.
Alisema Januari 27 mwaka huu mabondia wote watapimwa na atakayeonekana afya yake si nzuri hatopanda ulingoni ili kulinda usalama wake.
Kyando alisema mabondia wote watatakiwa kufika Morogoro Januari 24 mwaka jana kwa ajili ya maandalizi ya mwisho, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika kikao cha pamoja.
No comments:
Post a Comment