Na Mwali Ibrahim
CHAMA cha Riadha Tanzania (RT), kimeitaka mikoa kuharakisha kufanya uchaguzi mdogo ili kutoa wawakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa chama hicho, unaotarajia kufanyika Februari mwakani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT Suleiman Nyambui alisema hadi sasa kuna mikoa ambayo haijafanya chaguzi zake, ingawa ilishapewa taarifa.
Alisema miongoni mwa mikoa ambayo haijafanya chaguzi hizo ni Dar es Salaam, Mbeya, Mtwara, Morogoro na Rukwa.
"Kushindwa kufanyika kwa chaguzi hizo kunatokana na vyama hivyo, kutokuwa na ushirikiano na maofisa utamaduni wa mikoa yao ambao ndiyo wenye jukumu la kuwasimamia, hivyo wanapaswa kuwashirikisha maofisa hao," alisema Nyambui.
Aliongeza chaguzi hizo zinasaidia hasa katika uchaguzi Mkuu wa RT, kwa kuwa ili kufanikisha uchaguzi huo inapaswa kila mkoa utoe washiriki.
No comments:
Post a Comment