13 December 2011

Askofu aionya serikali ya JK

*Ataka iache kudhoofisha upinzani, kulinda amani iliyopo
*Asema CHADEMA inaongoza kwa umaarufu nchini
*Adai kutoridhishwa na matokeo yanayotangazwa na NEC


Na Gladness Mboma, Moshi

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt.Thomas Laizer, amesema Serikali ya Rais Jakaya Kikwete isifanye kazi ya
kudhoofisha nguvu ya vyama vya upinzani hasa wakati wa kupiga kura na kama hali hiyo itaendelea, wananchi watashindwa kuvumilia hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na utulivu uliopo nchini.

Alisema Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), kina umaarufu mkubwa kuliko vyama vingine vya siasa nchini hivyo umefika wakati wa Serikali kuviheshimu na kuvipa nafasi vyama vya upinzani ili viweze kufanya shughuli zao bila vikwazo hasa katika chaguzi mbalimbali.

Askofu Laizer aliyasema hayo juzi katika harambee ya kuchangia ukarabati na upanuzi wa kanisa la KKKT Nshara, lililopo Machame, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi.

Katika harambee hiyo ambayo ilikwenda sambamba na Jubilee ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Hai, Bw.Freeman Mbowe, zaidi ya sh.milioni 200 zilichangwa.

“Kuna watu wanashindwa kutamka wazi kuwa CHADEMA ni chama maarufu hapa nchini, rushwa za kununuliana kanga wakati wa uchaguzi haziwezi kuwafikisha Watanzania popote, miaka 50 ya Uhuru itakuwa na maana kwetu kama tutaondoa chuki kandamizi.

“Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo na kukubaliwa hata kama hayana ukweli binafsi sikubaliani nacho, naomba tujirekebishe katika kipindi kingine cha miaka 50, tusipofanya hivyo amani tuliyonayo itatoweka,” alisema.

Aliwasihi Watanzania kudumisha amani na utulivu uliopo sio katika mambo yanayohusu siasa pekee bali hata katika madhehebu ya dini kwa kuhakikisha jambo lolote ambalo litaonekana kufanywa kinyume, litatuliwe kwa mazungumzo.

Alisema Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema kuwa, “Mficha maradhi kilio kitamuumbua” hivyo amani iliyopo nchini itadumu kama haki itatendeka.

Askofu Laizer aliongeza kuwa ni jambo la kumshukuru Mungu kwa Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru bila ya mapigano wala umwagaji damu na kusisitiza kuwa, kila Mtanzania awajibike kumuomba Mungu ili aendelee kusimamia amani miaka 50 ijayo.

Alisema maandamano yoyote yanayofanywa na wananchi au vyama vya upinzani kupinga mambo mbalimbali, lazima Serikali ikae chini, ijiulize na kutafuta ufumbuzi wa tatizo badala ya kutumia nguvu nyingi kuyazima na kusababisha madhara.

“Naipongeza Serikali kwa kujenga barabara ambazo awali hazikupitika kirahisi, naomba uboreshaji wa miundombinu uendelee katika kipindi cha miaka 50 mingine ili kuharakisha maendeleo ya sekta mbalimbali,” alisema Askofu Laizer.

Mbunge wa Siha, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Bw. Agrey Mwanri, ambaye alikuwepo katika harambee hiyo, alisema Tanzania imepiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.

“Ni jambo la kumshukuru Mungu kutufikisha hapa tulipo, nchi yetu inashirikiana vizuri na mataifa mbalimbali duniani, raia wa nchi hizo wamekimbilia nchini kwa sababu ya amani tuliyonayo,” alisema.

Kwa upande wake, Bw.Mbowe alisema ujasiri wa kweli ni ule wa kukaa chini na kusikiliza wenzako kile wanachosema ili matatizo yaliyopo nchini yaweze kushughulikiwa.

29 comments:

  1. Ukweli wa udini unaanza kujitokeza kiuwazi kabisa ingawa mwanzo walikuwa wanahubiri kimafumbo na kichichini,na kukataa kabisa lakini sasa wameamuwa kujitangaza kwa uwazi,lengo ni kuchangisha mfuko wa kanisa iweje leo Laiser atamke waziwazi kuwa Chadema kinaumaarufu tena kwa maana ingine kuwa kura waliibiwa na tume ya uchaguzi, huu ni mwanzo tusubiri kati halafu mwisho!!!Ya kaisari tumuachie kaisari na ya Mungu ni ya Mungu karibuni sana

    ReplyDelete
  2. "Kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza matokeo na kukubaliwa hata kama hayana ukweli binafsi sikubaliani nacho, naomba tujirekebishe katika kipindi kingine cha miaka 50, tusipofanya hivyo amani tuliyonayo itatoweka" When the clergy people takes line in politics, Tanzania is probably moving toward undefined direction

    ReplyDelete
  3. Nadhani wewe mchangiaji hapo juu una ufinyu wa kuwaza. Askofu ni Raia mwenye haki kama wewe na mimi. Kwa nini ukweli usisemwe bila kujali itikadi, dini au jinsia? Viongozi wa dini bila kujali mkristo, mwiislamu au mpagani ni watanzania wanayo haki pia ya kutoa mawazo yao kama watu wengine wowote. Suala la kuingiza udini ni wewe umetafsiri kwa uduni wa mawazo yako. Jirekebishe ndugu yangu. Kama huna la kuchangia acha kupotosha.

    ReplyDelete
  4. Mimi nadhani tufike mahali watanzania tuache kushupalia mambo ya udini na ukabila.Mimi sioni mch.Laizer wapi ameonyesha udini au ametamka isipokuwa ameliasa taifa kutokana na hali halisi. Halafu huyo mwandishi kweli ni mfinyu wa mawazo yaani harambee kusherekewa na chadema basi imekuwa chama cha udini? Mbona mzee mengi pia alikuwepo hapo unajua yeye ni chama gani? haya agrey mwamri naye alikuwepo siyo wa ccm? acha kuchonganisha wewe tafakari kabla ya kusema.Tume ya uchaguzi ni madudu matupu kwa taarifa yako, na huo ndiyo ukweli CDM ina umaarufu mkubwa nchini na nje ya nchi angalia agenda zote inazoibua ccm mwishowe hukubaliana nao japo inapojaribu kuzipoka hoja na kuzitekeleza kinashindwa kwa sababu ya kutokuwa na utashi.Bravo askofu laizer.

    ReplyDelete
  5. mtoa maoni hapo juu hajakosea, ni wazi kuwa haki huleta na kudumisha amani, hivyo haki isipotendeka amani inaweza toweka, hasa kama walio nyimwa haki hawata kuwa wavumilivu. kwa wale waliotoa maoni ya kwanza hapo juu, ni haki yao lakini wameshindwa kuelewa kuwa kila mtu anahaki ya msingi yakutoa maoni yake, hivyo askofu kama mwananchi yeyote ametoa maoni yake, hivyo ni wazi kuwa ukandamizaji wa haki za msingi za wananchi zinaweza leta maafa hapo mbeleni.

    ReplyDelete
  6. Ni muda muafaka askofu Laizer akagombee uongozi wa CHADEMA ili aizungumzie vizuri badala ya kutumia madhabahu.

    ReplyDelete
  7. CCM changa la macho, watoto wa mafisadi wasiitetee? Wanakula, wanakunywa, wanasoma nje ya nchi bure. Pesa zipo za kutanulia na wanawake, wanashida gani haooo!!. Bravoo!! Bishop Laizer.

    ReplyDelete
  8. Heko Baba Askofu kwa kuwapa CCM na Serikali wamejisahau sana.Rushwa imekuwa Agenda ya CCM kila uchaguzi.Hata huyo aliepinga hotuba ni kada wa CCM na kama sio kada wa CCM basi ni Mtoto wa Kada wa CCM.
    Mtu mwenye busara hawezi kupinga hotuba ya Ba.Askofu aliosema hivi karibuni kwenye sherehe za jubilee katika Kanisa la Kkkt Ishara

    ReplyDelete
  9. @mchangiaji wa juu,mbowe ndo mtoto wa fisadi uliza historia yake,chadema ni chama cha kidini waislam hawana nafasi sana humo wala umuhimu mbona cuf ilipokua juu hawakusema haya kina laozer

    ReplyDelete
  10. Siku zote watu walioishiwa kifikra hushindwa kutmia akili zao katika kupambanua hoja zinazotolewa kwa maslahi ya taifa! Mimi siyo mchagaa, lakini sioni mantiki ya huyu mwehu kumhusisha Mbowe na ufisadi; kwani kafisidi nini na wapi? Je, Zito Kabwe na mbunge wa Sumbawanga mjini, anyekaimu uenyekiti wa CDM siyo waislamu? Mbona matukio yaliyojitokeza katika uchaguzi wa mwaka jana hukukemea pale Makamba mkubwa alipowahadaa na hatimaye kuwakashifu maaskofu akiwataka wakavue majoho ili wapambane, kauli iliyorudiwa na Nape na yule aliyepeleka Arusha kutotulia, yaani mary chitanda? Na ni akina nani waliobainika kutumia dini fulani kule Igunga wakiwahamasisha wadanganyika kutokichagua chama fulani? Nadhani huyu bwana hapo juu katokana na uzao wa posho, uzao wa wadanganyika wasiofikiri vyema, hata mijadala yenye tija kwa taifa wao hupotosha na kupotosha; karne hii ya ishirini na moja haina nafasi kwa wavivu wa kufikiri, CDM inawakilisha walipa kodi bwana!!

    ReplyDelete
  11. MASHEIKH.NAFIKIRI WAKATI UMEFIKA NANYI KUONYESHA MKO CHAMA GANI,MAANA YAKE SIYO SIRI TENA KUWA CHADEMA NI CHAMA CHA KIDINI.

    ReplyDelete
  12. mimi nasubiri nione wanaodai kuwa siasa ya Tanzania haina udini, wakati Gadaffi aliuawa na nchi za magharibi kwa msingi wa udini.uwazi ni kwamba demokrasia unaotoka magharibi umejaa udini,wanapalilia ukristo bandia duniani kwa kuleta siasa ya umwagaji damu.eti walioko madarakani ni wababe mbona Kipindi cha Mkapa(mkristo) hamkuja juu kiasi hicho wakati ndio rasilimali nyingi ya nchi ziliuzwa.maaskofu wasitudanganye wawe wazi, wasijifiche kwenye dini huku wakituletea sera za Illuminaty ya wasiomfahamu Mungu.

    ReplyDelete
  13. nafikiri ni vizuri tukafungua vichwa vyeti ili vifikiri,tusijaribu kuwa vipofu na viziwi wa akili.hakuna aliyezaliwa na dini siku ya kwanza wakati tunatoka matumboni mwa mama zetu lakini kila mtu alizaliwa na haki ya kuishi maisha ya utu.ukijua hayo yote unatambua kwamba hata dini ipo ili maisha ya utu yathaminiwe na dini ni mtumishi wa maisha ya utu. maisha ya utu muhimili wake ni haki. ikizingatia ukweli huu unagundua kwamba askafu na mtu mwingine yeyote bila kujali dini wanawajibika kusema ukweli bila kuhofia chochote. dini zisitumike kufunika maovu ili mradi tu watu wasiseme dini fulani ni sehemu ya siasa.Dini zote zinawajibika kutetea haki na kutumikia maisha ya utu.namalizia kwa kusema hakuna chama kilichodhihilsha kutumia udini kama CCM MFANO MZURI NI IGUNGA wakuu wa dini ya kiislam walisimama kidete kutetea maovu ili mradi tu kuitetea CCM Ishinde hii ni aibu pale viongozi wa dini wanaposahau kutimiza wajibu wao wa kuhakikisha kuwa haki inatendeka na badala yake wanakuwa mawakala wa kutenda maovu kwa maslahi yao mbinafsi .siku ya mwisho watamjibu nini aliyewatuma.
    sijaona hata dhehebu moja likisimama kuwabeba chadema zaidi ya uvumi tu. uchaguzi wa mwaka 2010 ubunge sumbawanga mjini kilitokea kioja nacho ni kama ifuatavyo:Mgombea wa CCM muislam kwa imani alishinda ubunge badala ya kuwashukuru watu yeye na wafuasi wake wakaandaa sherehe na kuweka msalaba ndani ya jeneza wakidai wameshinda nguvu ya kanisa?jiuliza sumbawanga una waislam wangapi mpaka ushinde nguvu ya kanisa.badala ya kukubali ukweli kwamba waliomchagua ni waislam na wakristo yeye na chama chake kwa kuwa wanaamini adui wao ni ukristo basi wakafikiri wameushinda ukirsto. tubadilike tufikirie kwa mapana nami naamini tanzania hakuna udini na wale wanaofikili upo waende mtaani watu hawana habari na hicho kitu. lakini pia yeyote anaetumia nguvu kupandikiza udini kama CCM asubili kuumia.

    ReplyDelete
  14. ikiwa hatukuchukua hatua za haraka watu wataumizana kwa mambo ya kidini.Kwa mtazamo unavyoonekana baadhi ya dini zimepewa nguvu kuikemea serikali au kufanya chochote na serikali imekaa kimya , hata ktk baadhi ya kambi za kijeshi kuna sehemu zimetengwa kwa ajili ya watu wa dini fulani, tunaiomba serikali iachane na hawa watu wa aina za dini zote , si vyema kwa baadhi ya watu kuona dini zao tukufu kushinda nyengine. Maaskofu kaeni pembeni muhubiri kwenye makanisa, mbona hatuwaoni mashekhe kuisema serikali ? na wakijaribu basi mara wameekwa mahabusu kwa kuipinga serikali , lazima upatikane uwiano ndugu zangu watanzania , nchi yetu ni ya dini nyingi , isiwe serikali inaegemea upande mmoja kama ilivyo sasa, mtasababisha maafa makubwa , Nd Kikwete , Nd Pinda jamani hamuoni?... wana macho lakini hawaoni....

    ReplyDelete
  15. Haya mambo ya dini kuwa na nguvu serikalini yalianzishwa na Mwl Nyerere , lakini yakifanyika chini chini kama mwongo angalieni uwiano wa watu wa dini tofauti katika serikali, mawizara , mashirika , vyombo vya sheria mahakama , jeshi / polisi,vyombo vya habari nk, tusilaumu akina JK yeye anaendeleza aliyoyarithi.

    ReplyDelete
  16. nyie acheni aibu kwanza mshukuruni nyerere kama angeliacha mambo kama alivyo yakuta nyie mnaosema ninajua ni waislam mgekuwa wachache sana serikalini kwani hamkuwa na kisomo na hamkuwa na mahala pa kusoma shule zote zilikuwa za wakiristo. muheshimuni yule mzee ametangulia mbele ya haki.kama angekuwa na kinyongo na hiyo dini yenu mungetokea wapi? mambo yote ni shule nyie mlipo mmekaria bao na majungu mtabaki nyuma daima .someni acheni majungu;shule zenu usimamizi mbovu watoto wanafeli tu halafu leo mnataka vyeo huenda mpeane kwa upendeleo.

    ReplyDelete
  17. KWELI MFUMO KRISTO UNATISHA. HIVI ASKOFU HUYU MAKENGEZA HAONI AIBU?

    WAISLAMU WASHAWAJUA NYIE NYOTE. LEMA NI MLOKOLE, MSIKA MCHUNGAJI, HAPO PADRI SLAA BEKI TANO WA KANISA, MCHUNGAJI TUNDU LISU, HALIMA MDEE BIBI WA KANISA, MNYIKA KIJANA WA CHURCH, MBOWE NDOO USISEME.

    ReplyDelete
  18. Siku zote hata ukiuficha ukweli,utajitokeza tu.Mwenye akili na afikiri, Mwenye macho na atazame, Mwenye mdomo na aongee.Enzi hizo ilikuwa usichanganye dini na siasa.Lakini hivi sasa ni ruksa.Ok, wenye macho tumeona na wenye akili tumeanza kujiuliza.Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa kila mtu na lake moyoni na si mdomoni.Kila mwenye uwezo na atetee upande wake.Lakini mwisho wa safari ni......???????Tuache ushabiki.Tuanze kupima maneno ya viongozi wetu, faida zake na hasara zake.

    ReplyDelete
  19. Ni kweli hayo wadau?

    ReplyDelete
  20. Naamini wanaosema hakuna UDINI hawajitambui. Tujiulize uchaguzi wa mwaka 2005 wakati huyu JK anaingia ilikuwaje?, Magazeti yoooote yalikuwa yakiripoti JK chaguo la Mungu, hayo ni maneno kutoka kwa viongozi wa dini. Mashekhe, Mapadre maaskofu wote walimsifu Jk. Tujiulize kulikuwa na msukumo gani hadi hawa viongozi wa Dini wakamsifu? Kipi walikiona? inawezekana kwa kuwa wao ni watumishi wa mungu watueleze. Na ilipofika 2010 mambo yakaja yakabadilika, wakaja na Walaka wa Uchaguzi, wakielekeza kiongozi gani wamchague waumini wao. Hapo ndipo ulipo anza kujitokeza udini,walianza Wakristo wakaja waislam wote wakiwa na walaka wao wakitoa maelekezo kwa kiongozi atakaye wafaa. Hivi kwa nini mwaka 1995 haikuwepo hiyo? Wakati Kigoma Malima alipokuja na chama chake wakamtangaza mdini na anaungwa mkono na Waislam, akaitwa mbele ya haki.CUF wakati ipo juu kwenye medani ya SIASA kikaitwa chama cha Waislam,tena wakasema wanapandisha Bendera hadi Mskitini, msiwachague hao. Lakini tumeshindwa kutambua kuwa ule ni uhuru wa mtu wa kuchagua kama mnavyodai hapo juu.Baba Askofu anavyosema, wakati CUF ipo juu maandamano yalikuwa kama leo hii Chadema wanavyofanya. Wakaitwa wakorofi vilungu kama kawaida kuanzia Manzese hadi Jangwani. Ila leo hii CHADEMA wanaonewa hawatendewi haki Maaskofu kila kukicha wanalaani, lakini hawakupata kulaani mauwaji ya January 2001 kule Pemba zaidi ya kusema CUF ni wakorofi.Angalia hapa '' Maaskofu wa Makanisa ya Kipentekoste jijini Dar es salaam, Jumanne Oktoba 7, 2008 na Maaskofu wa Jumuia ya Kikristo Tanzania (CCT) Jumamosi, Oktoba 24, 2008 walitoa matamko yao yaliyoitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iachane na mchakato wa kutaka kujiunga na OIC.Maaskofu tangu miaka ya 60 walitangaza wazi maadui wa Kanisa ni wawili "Ukomunisti na Uislamu" (Tazama Dr. John Sivalon, Kanisa Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara). Ukomunisti ulishajifia kifo cha mende, umebaki Uislamu. Maaskofu wana hofu na Uislamu (Islamaphorbia) kiasi cha kutoona boriti lililo katika macho yao bali kibanzi kilicho katika jicho la wengine.

    ReplyDelete
  21. huyo askofu na ajiunge tu na chadema ili aweze kusema kero zake si kutupotosha sisi wakristo tumenda kusali na si kufanya siasa. mbona yeye mwenyewe analalamikiwa na kanisa la kkkt kwa kuwaibia mabilioni ya fedha kwa nini asijiudhuli. askofu chungu kondoo wa mbwana mshika mawili moja humponyoka acha kanisa la bwana liendelee hauko peke yako

    ReplyDelete
  22. haya masuala yanachangiwa na vyombo vya habari ambavyo huwapa sauti maaskofu kuikemea serikali , ni vyema kwa vyombo vya habari kuacha kutumika kama vyombo vya kanisa , na hasa IPPMEDIA inaongoza kwa hilo.

    ReplyDelete
  23. Kama CHADEMA in chama cha kidini kama hao watu hapo juu wanavyo dai, basi usijiunge and CHADEMA, tuone kama kita kufa kwasababu wewe mtu mmoja una lalamika vitu ambavyo havitabadilisha msingi ya chadema. kumbuka, CHADAME INA SAJILI WATU 1000 KILA WIKI INCHINI. NENDA MAKO MAKUU UKAULEZE WATU WANGAPI WAMEJIUNGA NA CHADEMA WIKI HII TUU. NDIO UTAJUA KAMA CHADEMA NANI? LAKINI USIONGEE TUU VITU KUCHOCHE MAMBO YA KIPUUZI

    ReplyDelete
  24. SUALA KUBWA NI KUWA LAIZER ANATHIBITISHA WAZI ULE WARAKA ULIOTOLEWA MAKANISANI ARUSHA YA KUWATAKA WAKIRISTO WAIPIGIE CHADEMA KURA NI WA KWELI NA NDIO MAANA WAKATI WATU WAKISHAMALIZA MISA WALIKUWA WAKISALIMIANA KWA ISHARA YA VIDOLE VIWILI. MSITUHARIBIE NCHI KWA MABO YENU YA SIRISIRI. UNAFIKI WAKO LAIZER SASA MUNGU KAUFICHUA NA KUONYESHA WAZI HUFAI KUWA KIONGOZI WA DINI NA TUNAKUOMBA TAFADHALI SANA NENDA CHADEMA KAGOMBE NAFASI ZA SIASA NA DINI UWAACHIE WAUMINI WA KWELI.

    ReplyDelete
  25. Sidhani kama mtu akitoa maoni yake anapaswa kutukanwa. Kama unaona Laizer kakosea basi sema kosa lake siyo kutumia maneno yasiyofaa. Tanzania imeshauzwa siku nyingi, na wewe pia unaishi kwenye ukoloni mamboleo hujui tu. Nenda shule ndugu yangu usiropoke. Kuweza kusoma na kuandika bado hujaelimika unayemlalamikia Laizer. Tunahitaji watu wanaoweza kusema ukweli kama Bishop huyo. Si watu kama wewe unayefaidi ufisadi wa nchii na hapo unatetea uozo. Wanachi wangapi wanakunywa chai siku hizi? Umeme unakuwepo kwa masaa mangapi kwa wiki? Shilingi ina thamani gani sasa? Kikwete anaongoza asilimia ngapi wa Watanzania? Posho wanazojiongezea hawa wala nchi huzioni wakati wewe unashindia na kulalia uji! Mikataba mingi mibovu, mwekezaji anavuna 100% anaacha Tanzania 3%, jamani tuache uongo na ulimbukeni, tuwe wakweli. Mkizidiwa mnasingizia dini? Sasa Laizer angesemea wapi asiambiwe ni dini? Hata angesemea uwanja wa taifa mngesema ni dini, acheni hayo mtaendelea kuteseka kwa ujinga wenu, amkeni na someni alama za nyakati mnaopinga kijinga.

    ReplyDelete
  26. Hakika Tz imeshauzwa siku nyingi? Sasa tuseme ni Kiongozi muislamu kauza au vipi? Ndilo analosema Mchungaji Laiza! Kwa hiyo kiongozi akikutana na mhalifu kisha baadae akakutana na Askari anae mfuatilia mwizi huyo, Mchungaji akihojiwa na huyo askari aseme wongo kwa kuwa eti hulo litakuwa udini?

    ReplyDelete
  27. INASIKITISHA KUONA JINSI KIZAZI HIKI KILIVYONYIMWA UWEZO WA KUFIKIRI NA KUPAMBANUA MAMBO! SHULE MLIENDA KWA AJILI GANI? INAWEZEKANAJE MTU ANAKUDANGANYA BILA HATA KUTUMIA SAYANSI NAWE UNAKUBALI?

    HIVI UDINI NI NINI? INA MAANA HATA NIKIFUNGUA KAMPUNI MIMI NA MKE WANGU, HIYO KAMPUNI ITAKUWA YA KIKRISTO (IWAPO CC NI WAKRISTO) AU YA KIISLAMU (IWAPO CC NI WAISLAMU?) NDUGU ZANGU UDINI NI ITIKADI INAYOJARIBU KUTOA UPENDELEO MAALUMU KWA WATU WA DINI FULANI - SIYO KWA SABABU MIMI MUISLAMU, BASI HATA NIKITOA MAWAZO YAHUSUYO MWENEDO WA VIONGOZI WANGU BASI NITAKUWA NAZUNGUMZIA UDINI.

    TUNATAKIWA KUANGALIA HOJA, NA KUIPIMA BILA HATA KUANGALIA KAITOA NANI. KAMA HOJA INAPOTOSHA, IMEKAA KIUDINI UDINI , BASI TUSEME HUYU ALIETOA HOJA KAPOTOKA.....

    aH! NIMECHOKA BWANA - NAKASIRIKA NIKIONA UPUUZI UNAOZUNGUMZWA ...NITARUDI BAADAYE

    ReplyDelete
  28. askofu hujaeleweka ,yawezekana vp ktk hotuba ya Askofu usimtaje mungu hata mara moja unataja vyama na kusifia vyama vya siasa.hakika hujaitendea haki madhabahu na hustahili kuwapo hapo

    ReplyDelete
  29. LAIZER KAMA SIO FISADI KKKT AMEIFANYAJE HADI BANK WANATAKA KUFILISI MALI ZA KANISA. AUNGAME NA KUTUBU ILI ASAMEHEWE NA MUNGU. MAMBO YAKE YOTE YATAKUWA HADHARANI

    ReplyDelete