Na Mwajuma Juma, Zanzibar
MASHINDANO ya Kombe la Muungano kwa vijana wenye umri chini ya miaka 14, yameanza kutimua vumbi juzi katika Uwanja wa Mao mjini hapa, kwa kuzikutanisha timu za Kisk Academy na
New Boys ya Tabata, Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo iliyopigwa saa 4 asubuhi wenyeji Kisk Academy ilinyukwa mabao 4-1.
Mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka, husimamiwa na Kamati ya Central Wilaya ya Mjini ambayo mwaka huu yanaendeshwa na Kamati ya Central Taifa.
Jumla ya timu nane, zinashiriki mashindano hayo ambapo timu tano zinatoka Zanzibar na tatu kutoka Tanzania Bara.
Timu zinazoshiriki ni Kisk Academy, Chriss, Azam Zanzibar, Shangani, Barcelona, New Boys, Mwenge na TESA.
No comments:
Post a Comment