15 December 2011

Aangukiwa na tawi la Mbuyu, afariki dunia

Na Zena Mohamed

WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti Jijini Dar es Salaam likiwemo la Bi. Justa Fidelis (29), kuangukiwa na tawi mti wa Mbuyu.
Akizungunza na wandishi wa habari Dar es Salaam Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Faustine Shilogile, alisema tukio hilo lilitokea Ukonga Mzambarauni.

Alisema marehemu alikuwa amekaa na wenzake chini ya mti wakijikinga mvua iliyokuwa inanyesha na kwamba ghafla tawi la mti wa Mbuyu lilimuangukia na kufa papo hapo.

Kamanda Shilogile alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana.

Katika tukio lingine dereva wa pikipiki ya miguu mitatu maarufu kama bajaji Bw. Iddi Poli, anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka (35-40) amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondini, Charles Kenyela, alisema, tukio hilo lilitokea Tegeta Darajani baada na kutaja gari iliyohusika kuwa ni aina ya Toyota Hiace namba T 428 BLJ.

“Gari hii ilikuwa ikiendeshwa na Bw. Athumani miaka mwenye umri kati ya miaka (25-30), akitokea Njia Panda ya Kunduchi kwenda Tegeta, pikipiki ilikuwa na namba T 265 BTT, aina ya Tifan,” alisema Kamanda Kenyela.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwanyanyamala.
  

No comments:

Post a Comment