22 March 2011

Lipumba awavaa viongozi CHADEMA

Na Benedict Kaguo, Pangani

MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakina nia thabiti ya
kupambana na ufisadi kutokana kuchochea mgawanyiko wa Watanzania.

Alisema chama chochote cha siasa kilichoshindwa kuthamini matakwa ya wananchi wake hakina nia ya dhati ya kuwaletea ukombozi wa kweli wanaouhitaji Watanzania kwa sasa.

Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Pangani katika mwendelezo wa mikutano ya chama hicho 'kuwazindua Watanzania katika kujenga demokrasia ya kweli hapa nchi'.

Alisema wafanyabiashara wa Chadema hawawezi kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi kwa kuwa tayari wako katika mazingira ya kukumbatia rushwa, hivyo ni vigumu wao kuongoza mapambano hayo kama wanavyodai.

“Ndugu zangu wafanyabiashara na wapiga disko wa Chadema wanataka kuwang'oa mapapa ya ufisadi wa CCM ili wao manyangumi ya ufisadi waweze kuingia madarakani, hawana nia thabiti ya kupambana na rushwa,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema aliingia kwenye siasa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania sio kutafuta sifa kama walivyo baadhi ya wanasiasa wa Chadema.

"Sikuingia kwenye siasa kutafuta sifa, nimeingia kutumia elimu yangu kuwatafutia ukombozi Watanzania wenzangu, sasa hawa Chadema hawawezi kuiondoa CCM kwa kuwa wanachochea mgawanyiko mkubwa ndani ya nchi kwa kuwatukana Wanzanzibari waliokubali Serikali ya Umoja wa Kitaifa,” alisema Profesa Lipumba.

Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema taifa linaangamia kwa kukosekana uongozi ulio madhubuti sasa ni wakati wa Watanzania kuzinduka ili uchaguzi mkuu ujao waweze kukipa ridhaa chama makini cha CUF.

“Maisha yamekuwa ya kubabaisha huduma za afya hospitalini mama zangu mnatakiwa mwende na nyembe mnapotaka kujifungua, serikali inashindwa kununua wembe lakini wakati wa uchaguzi inaweza kununua kitenge kwa kila mwanamke Tanzania nzima,” alisema Bw. Mtatiro.

Alisema wakati wa mabadiliko ndio huu na wananchi hawana budi kukiunga mkono chama hicho ili kiweze kuongoza mapambano dhidi ya rushwa, matumizi mabaya ya fedha za umma ili kuwakomboa wananchi.

41 comments:

  1. Lipumba elimu yako haijakusaidia wewe na wala waTanzania. Kauli za kashfa na zisizo na heshima hazistahili kutoka kinywani mwa Profesa, labda awe profesa feki na aliyechoka kama wewe.

    Siasa zimekushinda, na sasa unpigia debe ndoa yenu CUF na CCM. Unajinadi kuwa wewe hukuingia kwenye siasa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania, kivipi? Mbona unaonekana kushindwa kazi hiyo kabla hujaianza? Jiulize, siasa za CUF za 1995 - 2004 ndizo hizi za sasa? Kwa nini mumegeukia kuikumbatia CCM ili mpate huruma yao? Upinzani unaujua kweli Lipumba?
    Pisha weye kuitakia nchi hii mema wafanye kazi. Wivu wa maendeleo ya kiuchumi ya mtu binafsi ndiyo yanayokuuumiza wewe na viongozi wenzako wa CUF. Watch-out!!!! Ninyi ni vibaraka wa CCM!!!

    ReplyDelete
  2. Lipumba ulipaswa uje na hoja zenye nguvu dhidi ya hiyo CCM unayotaka kuing'oa madarakani si kuwaita watu wapiga DISCO wakati wewe hatuoni hata chembe ya uprofesa wako ndani ya kauli zako. Achana na CHADEMA. Ganga yako na CCM yako mliyokumbatiana

    ReplyDelete
  3. Lipumba huna point huna sera siasa imekushinda acha majungu nenda vyuoni ukafundishe utaleta mchango mkubwa sana na wa maendeleo, hizo kauli zinakupunguzia hadhi na heshma yako.

    ReplyDelete
  4. lipumba kwani kufanya biashara halali kama kupiga disko na kulipa kodi kwa maendeleo ya watanzania ni kero kwako? mbona uprofesa wako wa uchumi haukusaidii kujua vitu vidogo kama hiyo? ina maana wewe ukiwa rais kumbi zote za disko utazifunga? mbona kodi inayotokana na hao wapiga disko hujaikataa?
    fanya siasa, sio uprofesa taahira

    ReplyDelete
  5. Ukweli wa Prof. mwongo umejidhihirisha sasa. Ninamshauri Lipumba asome alama za nyakati. Umeshachoka Prof. wangu siku zako sasa zinahesabika. Jiulize kwa nini CUF ya 1995 sio hii ya sasa? Tanzania Bara uchaguzi uliopita 2010 umefanikiwa kupata wabunge wangapi? Kwa nini chama kimeshuka ghafla na kukosa umaarufu hivyo. Ni wakati wa Prof. Lipumba kung'atuka aachie vijana kukiendesha chama. Mbona vikongwe vya CCM vinasemwa ni vipi CUF mnasahau kuvisema hivi vikongwe vyenu. Mawazo ya Lipumba ni machovu sana jamani amebakia kuipigia debe CCM kama Augustino Mrema wa TLP. Tunashindwa kumwelewa Prof. Lipumba ni mpinzani kweli au pandikizi la CCM? Chama chako kinaisha umaarufu polepole badala ya kubuni mbinu za kukijenga upya unabaki kuwatukana CHADEMA huoni unapoteza muda? CHADEMA KIMEFANIKIWA kutwaa majimbo mengi uchaguzi uliopita na hiyo ndio sababu wapinzani wengine wana wivu mkubwa. Jengeni vyama vyenu achaneni na CHADEMA au wivu ni hiyo ruzuku? Wananchi wanawashangaeni sana mnavyopiga vita wapinzani wenzenu. Ninamshauri Ndugu Mtatiro asimame imara maana yeye bado damu changa usifuate nyayo za huyo mchovu Lipumba huyo ni sawa na Prof. wa miti shamba elimu yake mbona haimsaidii hata kidogo? Nakushauri ustaafu siasa usije ua chama cha CUF.

    ReplyDelete
  6. Mimi nadhani profesa siasi zimeshakushinda kwasababu huwezi kupanda jukwaani na kuwakashifu wapinzani wanzako badala ya kutangaza sera na uzuri wa CUF kama unauona upo, na kuacha kuwatukana wenzako kuwa ni manyangumi ya ufisadi ili hali kila mtu anajua kuwa mapapa na manyangumi ya ufisadi yako kwenye chama kinachotawala nchi hii kama kweli chama chako ni kizuri kiasi hicho mbona una mbunge mmoja tu bara? au umeridhika na posho ya visiwani kwakuwa kuna wawakilishi wengi kule? ukitaka watanzania wakukubali kama hao wapiga disco wanavyokubalika nao tangaza sera sidhani wapiga disco kama unavyowaita hawakuwa na sera nzuri ndio maana wakachaguliwa na wananchi la hasha sera zao zinauzika baba, nenda ukagombee ubunge kwenu uone kama utapita wenzako mrema, cheyo na mbowe ameenda kwao na anauzika sijui wewe kama unauzika nyumbani kwako

    ReplyDelete
  7. Sasa tunaanza kuelewa nini maana ya CHADEMA kukataa kuungana na CUF; Kumbe ni kwa sababu ya ndoa ya kweli ambayo sasa unaitumikia ili kuilinda kwa kuchafua wengine? Lazima watanzania tuwakatae vibaraka kama Prof. Lipumba na wenzake maana hawana nia ya kweli ya kuleta mageuzi zaidi ya kupigania maslahi yao binafsi. Sasa hatuogopi kusema CUF ni CCM B hasa kwa kauli na vitendo vya CUF na viongozi wake. CHADEMA ndiyo chama tawala mpaka unakishambulia? Huna hoja...ni wajinga wenzako watakaokusupport kwenye hili

    ReplyDelete
  8. Swali langu kwa Prof. Lipumba, Je hao MAPAPA ya ufisadi wako tu TANZANIA bara? Au hata huko ZANZIBAR wapo ambapo CUF ni sehemu ya serikali?

    The case of the kettle calling a pot BLACK

    ReplyDelete
  9. prof LIPUMBAVU, kweli we pumba
    unakumbuka haya maneno ya smz kuhusu cuf enzi hizo wakati wewe ni mpinzani wa kweli?
    leo na wewe unaongea kama wao kuhusu wapinzani wa kweli.

    SMZ yakiita CUF- Chama cha Uchochezi na Fujo

    lYatamba: China, India, Libya,Iran, Misri na Japan zinaisaidia

    Arnold Victor

    SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzabar (SMZ) imedai kuwa sera za "Jino kwa Jino" zinazotangazwa na CUF zinaonyesha kuwa chama hicho si chama cha wananchi kama kinavyoitwa bali ni chama cha uchochezi na fujo. Wakiongea na waandishi wa habari jijini katikati ya wiki, mawaziri wa Zanzibar, walisema hawana imani na mwafaka waliowekeana na CUF kwa vile chama hicho kimekuwa kikitoa kauli zinazotishia amani tangu kuanzishwa kwake.

    Waziri anayeshughulikia masuala ya nchi za nje wa SMZ, Balozi Isaack Sepetu, alidai katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) jijini kuwa chama cha CUF kiliwahi kutamka hadharani kuwa kitakomesha utawala wa mtu mweusi Tanzania Visiwani, jambo ambalo linaashiria ubaguzi wa hali ya juu wa rangi na ambao unaonekana kuwa kiini kikubwa cha kukwama kwa usuluhishi wa mvutano wa kisiasa visiwani humo.

    Alidai pia kuwa CUF kimewahi kutangaza kuwa wanawake wa visiwani wajiandae kuishi kizuka(bila waume) kwa vile kuna hatari kuwa waume zao wote watakufa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

    Kauli kama hizo, alisema Sepeku zinaonyesha kuwa CUF si chama kinachowatakia Watanzania mema.

    Hata hivyo, SMZ na CCM wamekuwa wakishutumiwa kwa kuvunja haki za binadamu na kukandamiza demokrasia, kiasi cha kukatiwa misaada na nchi mbali mbali hususan zile za Nordic.

    Hali hiyo imelifanya jina la Zanzibar kuwa chafu katika Jumuiaya ya kimataifa.

    Serikali hiyo imesema kuwa haijali sana kukatiwa misaada kwa vile nchi nyingine kama China,India,Iran, Libya, Misri na Japan zimekuwa zikiisaidia.

    ReplyDelete
  10. weweeeee!!!! hureeeee!!! TANGAZO!! D.I.S.C.O wapi: Bills au ARS,MZA,SHY,sasa tunakuja MBY. kweli wewe Lipumba sasa umekomaa kisiasa unaelewa pumba, makapi na mchele. yaliyokuwa yanasemwa hizo pesa walizopewa na wenyewe watalizilipaje kwakuwa ahadi ya kukamata dola umeota mbawa. rudisheni jamani hiyo pesa yao, matokeo yake mnazunguka nchi nzima kuleta shida taabu na maneno lukuki Jamani tunachotaka sasa ni maendeleo siyo maneno, uchochezi na giriba hizo potofu. tumeamua CCM miaka Gwala (5) subirini 2015 tena, lakini kishindo cha CCM itakiweza wanajipanga tena hata hayo machache yatarudi tumekwishaona wapiga Disco hawana lolote, hatutarudia tena kujaribu ni bora tulijaribu kwa Wabunge na Madiwani siyo Urais kweli sijui Tungeharishia wapi sasa hivyo 23 tu imekuwa Nongwa. CHADEMA TUMEKWISHA WACHOKA. Lipumba wape ukweli wao wasuke wanyoe au ..........

    ReplyDelete
  11. oh!!!!!!!! watanzania wenzangu ni wapi tunakwenda kwa hali hii sijui hata kiongozi mkubwa kama lipumba anadiriki kuongea pumba kama hizi nikweli kuliko unyimwe akili au hekima ni bora unyimwe makalio ya kukaa hapa inaonyesha elimu ya huyo anayejiita profesa ni bure poleni sana mnaoongozwa na huyo profesa

    ReplyDelete
  12. Ahsante sana Professa. Sijui nikuone wapi nikupe mkono wangu. Haya maoni ya hao mamluki waliokodishwa na hao wafanyabiashara kukaa kwenye internet kujibu kila hoja inayokwenda na mawazo yao yasikushughulishe,tunakataa wafanya biashara katika ccm kutokana na yaliyoikumba nchi halafu tuwaingize hawa nyamaume wa kichaga hapo,loo Mungu apushe mbali nchi hii,hivi wewe Mbowe una lipi katka siasa? au Ndasamburo au Mtei. WELL DONE PROFESSA KEEP IT WAPASHE HAO TUNATAKA UKOMBOZI WA KWELI HATUTAKI MATAJIRI NA WAFANYABIASHARA KUONGOZA NCHI HAWAWEZI KUTENGANISHA BIASHARA ZAO NA MASLAHI BINAFSI KAMA ILIVYO KWA CCM SASA. TUANGALIE VIONGOZI TUNAOWACHAGUA NA STAILI YAO YA MAISHA WANAOISHI NA FAMILIA ZAO KAMA KWELI WANATUFAA,KUWAPELEKA WATU LOLIONDO KWA BABU SI KIPIMO CHA KUMCHAGUA KIONGOZI

    ReplyDelete
  13. Huyo hajiiti Professa ni professa kweli na sio wa kusomea ukubwani. Mchango wake unatambulika kimataifa

    ReplyDelete
  14. Lipumba yuko sahihi! Mimi CHADEMA nainasibisha na CHAMA cha Kanisa, hivi sasa wanatekeleza yale yaliyokuwa kwanye waraka ambayo deadline tarehe 30 November 2011

    ReplyDelete
  15. professor L'pumba' mbona haiingii hakilini kwa mtu ambaye tunafahamu mwenye elimu kama yako kuongea hayo uliyo sema,unatutia wasiwasi uenda hata uwezo wa kufundisha hauna ndiyo maana umeamua kujibana kwenye siasa.Siasa ya sasa inataka watu wenye upeo mkubwa sio kama wewe ambaye hata Itataro amekuzidi busara. Ila atushangai sana kwa kuwa tunajua kwa cuf kuwa nyumba ndogo ya ccm,hiyvo uanahaki ya kumtetea bwana anaye kufanya uweze kuishi mjini.niaibu tupu kwa CUF sasa ni wazi kaburi lenu litachimbwa siku moja na la CCM.

    ReplyDelete
  16. Yale yale Mbwa wa Slaa na wafanyabiashara wa kichaga tayari wanabweka,wamewekwa hawa kwenye internet makusudi kulinda maslahi ya hao jamaa. Professa endelea kusema,mbona wao wanasema mpaka wanazulia watu vifo hawa mbwa wao hawalaumi?

    ReplyDelete
  17. lipumba sema baba professa wa ukweli,ulijitoa sadaka katika nchi hii, yaliyokupata mbagala wanayajua chadema kuwa wewe sio mwanasiasa njaa kama mbowe,slaa na wengine katika chadema,hebu jiulize mwenyewe uchaga uliopo ndani ya chadema nchi hii ikaenda wakashinda kweli tunaweza kuishi kwa amani iliopo hivi sasa,mchaga ni jini wa pesa chadema wote ni wachaga,wataibiana,na nchi haitataaliwa,

    ReplyDelete
  18. maandamano ya kuitoa serkali ilichaguliwa kihalali hio ni jinai,mbowe na chadema yako yenu jifunzeni siasa kwanza musihadae watu na kuwadanganya hao maskini na kuwatia barabarani kwa maslahi yanu,siasa sio biashara ya disco nchi hii sio yenu wachaga,mwalimu nyerere alisema nchi kumpa mchaga ni sawa na kumpa mbwa atawale,nendeni mkasomee siasa kwanza sio kudanganya watu kwa kuwatia barabarani kwa kisingizio cha misri,na tunisia ...

    ReplyDelete
  19. nakushangaa unaedai kuwa watu wako internet kwa ajili ya kulinda maslai ya watu fulani, unasasu na wewe umetoa mchengo wako kupitia internet, Je wewe unalinda maslahi ya nani?

    ReplyDelete
  20. Ama kweli twaafwa kama siasa ndo hizi? kweli hakuna jipya chini ya jua. hata lipumba tulietegemea kuwa ndiyo mpinzani mahili umeanza kuchoka kama mrema. au kuna siri nyuma ya pazia kuwa kila mpinzani aisifiaye ccm kuna malipo makubwa anapatiwa? yarabi tufike salama katika harakati ya kuiondoa ccm, na kwa mapenzi ya mungu tutafanikiwa subiri siku yaja.

    ReplyDelete
  21. Ki ukweli Lipumbavu sina uhakika kama ni Profeaor kweli au unajitia tu,inaonekana umeishiwa;nakushauri ukatafute issue nyingine unaweza kufanikiwa kwenye siasa huna MVUTO hjashtukia? hao madisco DJ walivyofanikiwa:WASOMI WA UKWELI HATUDANGNYIKI KWENU WALA KWA MUME WENU CCM.

    ReplyDelete
  22. Aya lipumba unajitahdi kiduchu bt ushachoka mzee na hako ka mrema yan cjui2 au mshakunywa maji ya bendera ya ccm(mume enu?)cz mnavo mtetea utafikir kawanyima unyumba yan?bt nany mnao iponda chadema eti chama cha kidini,chama cha wachaga endeleen kutoa hayo mawazo mgando enu cz 1day mtakua majembe bna?

    ReplyDelete
  23. CHAMA CHA UPINZANI TANGANYIKA NI CHADEMA WENGINE WOTE NI WAGANGA NJAA KWA MAFISADI. LIPUMBA TUACHIE NCHI YETU UENDE KATIKA NCHI YAKO YA ZANZIBAR.

    SITAKI MUUNGANO

    ReplyDelete
  24. Hivi huyo jamaa aliyeandika kuwa eti hatutaki wafanyabishara kwenye siasa kwa kigezo cha kumtetea Lipumba na hata kutetea CCM anajua Tanzania hii au? ni chama gani cha siasa viongozi wake wamejitita kwenye biasahara kama hao wapendwa wetu wa CCM? Angalia miradi mikubwa uliuliza ni jamaa tena kiongozi wa CCM katia nguvu pale! Mjengo wa vijana unajengwa utadhani mnara wa babeli ni wa akina nani? si hao hao? tena ndio wananyumbisha nchi? watu hawapumui kwa sababu yao! Hivyo kama ni biashara hao wamejikita zaidi na tena za kifisadi? Waachaeni kuwalaumu hao Chadema! waacheni wafanye kazi yao ili mradi inasaidia serikali kujirekebisha!

    ReplyDelete
  25. semeni yote mmalize yote kwa yote mboe na slaa nchi hiyo hamuipati mnajidanganya bureeeeee baba yako mboe ndio mkurugrnzi wa kwanza nchi nafasi aliopewa na mwalimu jk kubinafsisha mashirika ya umma chini ya rafiki yake kipenzi samueli sita akiwa waziri wa sheria wadanganyeni hao wakuja wasiojua kitu hasa hao wanafunzi wa udsm watoto wa mikoani mtoto wa bongo anadanganywa?

    ReplyDelete
  26. Lipumba elimu yako haijakusaidia wewe na wala waTanzania. Kauli za kashfa na zisizo na heshima hazistahili kutoka kinywani mwa Profesa, labda awe profesa feki na aliyechoka kama wewe.

    Siasa zimekushinda, na sasa unpigia debe ndoa yenu CUF na CCM. Unajinadi kuwa wewe hukuingia kwenye siasa kwa lengo la kuwasaidia Watanzania, kivipi? Mbona unaonekana kushindwa kazi hiyo kabla hujaianza? Jiulize, siasa za CUF za 1995 - 2004 ndizo hizi za sasa? Kwa nini mumegeukia kuikumbatia CCM ili mpate huruma yao? Upinzani unaujua kweli Lipumba?
    Pisha weye kuitakia nchi hii mema wafanye kazi. Wivu wa maendeleo ya kiuchumi ya mtu binafsi ndiyo yanayokuuumiza wewe na viongozi wenzako wa CUF. Watch-out!!!! Ninyi ni vibaraka wa CCM!!!

    ReplyDelete
  27. Hah hah haaaa siasa ndo hii bwana watu wakiwapinga hao wahuni wanaambiwa rudi shule, kwamba hawajasoma ila wao wamesoma. Na sasa wasomi wanaongea! Hivi kashfa gani kaongea kuhusu Chadema? Au hawajihusishi na biashara, muziki. Its about time for these hooligans to stop thinking like they are class one tanzania, behaving like they are the ones deciding the ultimete of this country because they are simply loosers. Wonderful enough wakiongea upuuzi wao utaambiwa haki 'ya kutoa maoni'. Nadhani hiyo haki ni ya Chadema tu. I just cant wait to see vile raiamwema wataandika wiki hii na ndugu zao mwananchi wa Chadema. Watapapatika sana, ni 2011 hii ujinga wao umeanza kuongelewa na watu wenye akili zao, maprofesa wa ukweli mpaka ifike 2015 Chadema will be in grave na tutabakia na siasa safi za amani, asili yetu, hola...

    ReplyDelete
  28. Jamani Prof kasema Ccm mafisadi papa halafu Chadema ni mafisadi nyangumi. Kuna watu wana akili zaidi humu wanasema anawatetea Ccm kulinda ndoa yao, najisikia kuaminiamini tatizo hawana hoja hata moja hawa wasomi, walete hoja...

    ReplyDelete
  29. nawaonea huruma cuf ya bara hawana kitu tena na lipumba anategemea serikari ya mseto bara hapati huo umakamu aliopata seif sharifu endelea kuwasaidia ccm.WANACHAMA WA CUF LIPUMBA AMEISHA ANZA KUWADHARAU NYEE WANACHAMA ANAONA UPROFESA WAKE NYIE NI MATAHIRI MTIMUENI.NA TAARIFA CUF NI ZANZIBAR

    ReplyDelete
  30. CUF MMEKWISHA, HICHO KIFO KITAKATIFU. LIPUMBA KESHAONA MAJI MAZITO. NIMEWASIKIA KAULI ZAO NA HAMADI SIO NZURI KAMA WANATAFUTA VITA VILE. YETU MACHO TUNAANGALIA TU.

    ReplyDelete
  31. Hamadi na kiherehere chake ndiyo wa kwanza anaechochea na kusema muungano uvunjwe lakini tunamsikia anaendesha mikutano huku bara Zanzibar kumemshinda. Hatutaki atuletee mambo yake ya kigaidi. Wazanzibar tulionao kwenye serikali wanatosha wao wakajenge muungano wao wa kitaifa watuachie Tanganyika yetu

    ReplyDelete
  32. kama maprofesa wa Tanzania ndio hawa basi hii nchi mwisho wake umefika, Lipumba ni kiongozi mnafiki na huyu anafaa kuimba taarabu ndio zinamfaa na siyo siasa kabisaaa, acha kutukana wenzio maana Chadema wanahoja iweje CUF ufunge ndoa na CCM wakati huo unasema unataka kuwang'oa CCM ya kweli hayo profesa? wewe choka mbaya kalala kwanza nashangaa CUF wanasubiri nini kukutimua kila siku wewe tu kugombea urais wakati hata uenyekiti kijijini kwenu uliko zaliwa huwezi kupata?

    ReplyDelete
  33. eti profesa,ujinga mtupu,sasa anaposema CHADEMA ni wanamuziki na wafanyabiashara,mbona yeye wa kwake ni wacheza taarab!!!!!!!!!!!!!!! ni kweli huyo ni LIPUMBAVU eti profesa,profesa maji marefu nini!!!mchawi mkubwa wewe,siasa zimekushinda,tangu 1995 unagombea tu,kwa nini usirudi darasani,huupati uraisi ng`ooooooooo,UTAZEEKEA KUPIGA KAMPENI KILA BAADA YA MIAKA MITANO.

    ReplyDelete
  34. na huyo kuku mtatiro ni lijingaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,domo kubwa chapati hakunji

    ReplyDelete
  35. tulizani upo kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania leo umekuwa wa kwanza kuwatetea chama tawala?elimu yako ni bure bora ungekuwa unanyamaza tu,sukari juu!nauli juu!maisha yamepanda,thamani ya Tsh inazid kushuka hukuviona vyote hivo umeliona hilo tu?unajiita prof wa uchumi,Uchumi upi huo?

    ReplyDelete
  36. upala kama uwanja wa mpira,pua kama unapuliza moto,fanya kazi ya kutetea nchi acha umbea wa jukwaani,

    ReplyDelete
  37. Professor Lipumba!wewe ni msomi tena uliyebobea,lakini kauli ulizotoa hazina tofauti na za wale maprofesa maji mafupi nk.wewe nilidhani ungekuwa umeshayaona wanayofanya watu wa Chadema kwenye midani za siasa za Tz, na mbali zaidi wewe ni mchumi.
    Je, wanachopigania Chadema ni kibaya kwa nchi hii? Najua utasema si kibaya tukiwa mimi na wewe peke yetu.Mimi nakushauri usijiingize kwenye matusi au kashfa.Porfessor hu analyse mambo na kuyatolea kauli usije ukajidharaulisha kwa kutoa matamshi kama Lumpern!wewe ni PROFESA.Usifikiri kuwaita wenzio wapiga disco ndio umewaponda sana.Mbona akina Komba wako bungeni wanatunga sheria?Disco si tusi ni kazi tu.Tafuta lingine kama unataka kuondoka kwenye u prof na kuwa mwanasiasa mbabaishaji.Matusi huyawezi.

    ReplyDelete
  38. afadhal sasa lipumba amedhihirsha waz kuwa cuf n chama kibaraka cha ccm. profesa huyu anaaibsha kwa kutoa kaul pumba kama jina lake. si kla anayesoma ameelmka na hl n ushahd tosha. chadema songen mbele msitishwe na machangudoa wanaojiuza ccm kama pr lipumba.

    ReplyDelete
  39. CARRY ON PROFESSOR EVEN THE LATE PRESIDENT NYERERE ALISEMA HAWEZI KUACHA NCHI IKAENDA KWA MBWA. HATUTAKI WAFANYABIASHARA KWENYE SIASA. TUNAWAKATAA CCM KWA HILO LEO TUWAPE WAFANYABIASHARA WA KICHAGA TUTAKUWA WENDAWAZIMU,NI SAWA NA KURUKA MKOJO KUKANYAGA MAVI

    ReplyDelete
  40. Ugomvi wa ccm na chadema ni hazina ya nchi,wote wezi wanaoshindana kushika mfuko wa fedha wa taifa hili

    ReplyDelete
  41. angalia posted article hapo juu jinus CUF walivyokuwa wakisemwa ZNZ kabla ya serikali ya mseto= WATANZANIA KWELI WATU WA AJABU SANA, WAMESAHAU HATA CUF WALIPiGWA VITA NA SMZ WAKATI HUO KAMA WANAVYOPIGWA CHADEMA SASA (POLENI SANA KWA KUJA). TATIZO LIPUMBA HAWEZI KUTOA HOJA ZA KISIASA KAMA PROFESA KWA KUWA AMESOMEA UCHUMI NDIO MAANA ANAPOTEA HIVI. ANGALIZO RAFIKI WA ADUI YAKO (CCM + CUF ZNZ) HAWEZI KUWA RAFIKI AU KUKUTAKIA MEMA (CUF KWA CHADEMA) BARA.

    ReplyDelete