Na Gabriel Moses
BAADHI ya watumishi wa Makahama ya Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam, wameiomba serikali iwajengee jengo lao tofauti na ilivyo sasa ili kuboresha utendaji kazi na kuongeza hadhi ya chombo hicho.
Wakizungunza na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutotajwa kwa hofu ya kushughulikiwa, wafanyakazi hao walisema licha ya serikali kutumia mamilioni ya fedha kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa nchi hadi sasa mahakama hiyo inatumia jengo la kupanga.
Walisema Mahakama hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo miundombinu mibovu hivyo kuwakatisha tamaa kufanya kazi kwa moyo.
“Makahama hii ipo katikati ya jiji lakini ipo katika hali mbaya, pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala kukusanya kodi nyingi, hakuna dalili za kuiboresha ili ionekane ya kisasa.
Awali Mahakama hii ilijulikana kama Samora kwa sababu ya kutumia kwa muda mrefu Jengo la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya hapo tulihamia hapa Lumumba,” alisema mfanyakazi mwingine mrundikano wa watu eneo hilo.
Katika hatua nyingine, watumishi wa Mahakama hiyo wameiomba serikali kuharakisha mfumo mpya wa utunzaji kumbukumbu hususan majalada ili kupunguza mrundikano wa kesi.
Wamesema mfumo uliopo sasa umepitwa na wakati hivyo serikali haina budi kuhakikisha teknolojia za kisasa zinatumika katika mahakama zake mbalimbali.
No comments:
Post a Comment