19 October 2011

Simba vitani tena leo

Na Zahoro Mlanzi

VINARA wa Ligi Kuu Bara, timu ya Simba leo itakuwa katika mtihani mwingine itakapoumana na Ruvu Shooting ya Pwani kwa kutaka
kuendeza azima yao ya kushinda mechi tano, zilizobaki katika mzunguko wa kwanza.

McNa Zahoro Mlanzi

VINARA wa Ligi Kuu Bara, timu ya Simba leo itakuwa katika mtihani mwingine itakapoumana na Ruvu Shooting ya Pwani kwa kutaka kuendeza azima yao ya kushinda mechi tano, zilizobaki katika mzunguko wa kwanza.

Mchezo huo utapigwa Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ukiwa ni mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

Simba katika mechi ilizojiwekea kushinda ni pamoja na ile dhidi ya African Lyon, ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Timu hiyo kwa sasa ndiyo inayoongoza ligi, ikiwa na pointi 21 ikifuatiwa na JKT Oljoro yenye pointi 19, Azam FC ina pointi 18 na Yanga katika nafasi ya nne kwa pointi 15.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Mkuu wa Simba, Mosses Basena alisema mpango wao wa kushinda mechi tano, upo pale pale na kwamba tayari moja wameshashinda na wana imani mechi ya leo watashinda pia.

"Timu inaendelea na mazoezi kama kawaida Bamba Beach, ipo katika morali ya juu na kwamba nitazidi kuwapa mbinu zaidi ili kufanya vizuri," alisema Basena.

Akizungumzia kiwango cha kiungo wake Shomari Kapombe, alisema ni mchezaji mzuri, anayejituma na kwamba kama ataendeleza kucheza katika kiwango kile, hana shaka atakuwa hazina ya taifa kwa baadaye.

Naye Ofisa Habari wa timu ya Ruvu, Masau Bwire akizungumzia mchezo huo alisema watahakikisha wanatibua rekodi ya Simba ya kutofungwa.

Alisema mbali na rekodi hiyo, pia watahakikisha kampeni yao ya kushinda mechi tano, inaingia doa kutokana na kufanya maandalizi ya nguvu.

"Timu yetu baada ya mapumziko mafupi kupisha timu ya taifa (Taifa Stars), tuliingia kambini kujiandaa na michezo iliyobaki na tumejiwekea kwamba lazima tuhakikishe tunaifunga Simba," alisema Bwire.
hezo huo utapigwa Uwanja wa Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ukiwa ni mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

No comments:

Post a Comment