Na Esther Macha, Chunya
VIONGOZI wa vijiji katika Kata ya Kanga, Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya, wametakiwa kuwaeleza wananchi misaada na vifaa vinavyotolewa na mbunge wa Jimbo
Songwe Bw. Philipo Mulugo ili kusaidia ujenzi wa shule za sekondari na msingi.
Bw. Mulugo aliyasema hayo juzi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Tete, jimboni humo baada ya kuwauliza kuwauliza wananchi kama wameelezwa juu ya msaada aliotoa wa mifuko 50 ya safuji ili kusaidia ujenzi wa Shule ya Msingi Kanga.
Alisema kitendo cha wananchi kutopewa taarifa za misaada anayotoa ni kutengeneza maneno ambayo mwisho wa siku, matokeo yake hayawezi kuwa mazuri.
“Mimi kama mbunge wenu, wananchi watajisikiaje kama nimehaidi jambo alafu nimeshindwa kulitekeleza kama viongozi mtaendelea kukaa kimya bila kuwaeleza misaada ninayotoa.
“Hii inajenga picha mbaya, tubadilike ndugu zangu, tabia hii sijaipenda kabisa, mkifanya mikutano yenu waelezeni wananchi nini nimefanya siyo kukaa kimnya jamani,” alisema.
Bw. Mulugo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, alimtaka Mwenyekiti wa Kijiji hicho kufanya mikutano ya hadhara mara kwa mara na kuwaeleza wananchi misaada au vifaa vinavyotolewa na mbunge badala ya kukaa kimya.
“Mheshimiwa diwani, mimi na wewe sote tunachaguliwa na wananchi hivyo ni vema ukawa unatoa taarifa kwa wananchi ili siku ikifika, tusiambiwe hatujatekeleza ahadi tulizotoa,” alisema.
Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Vicent Mpanzo, alisema taarifa ya msaada huo alitoa katika mahafali ya darasa la saba shuleni hapo.
Wahariri wa Habari
ReplyDeleteJaribuni Kupitia taarifa kabla haziaandikwa
angalia hapo juu
ineandikwa "alafu" Badala ya Halafu
makosa madogo kama haya huwa yanajitokeza mara kwa mara na kuwapotosha wasomaji wachanga (wanafunzi wanaojifunza)