*Aliyeuawa Igunga kufanyiwa Dar hitma leo
Na Charles Mwakipesile, Mbeya
WABUNGE na madiwani wenzao wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana walisusa na kutoka nje ya kikao cha
Baraza la Madiwani kwa madai ya kutosikilizwa wakati wakihoji kubadilishwa kwa muhtasari wa kikao uliotakiwa kujadiliwa badala yake ukapelekwa uliojadiliwa mwaka jana.
Awali wakizungumza kabla ya kuanza kwa kikao baada ya kupewa nafasi na Meya wa Jiji, Bw. Athanas Kapunga, Diwani wa Kata ya Sinde, Bw. Fanuel Kyanula (CHADEMA) alitaka mwenyekiti huyo kuzingatia maombi yao ya kutokuwa na imani na kikao hicho kutokana na kutolewa kwa muhtasari wa mwaka huu, kuanzia Julay kama ilivyotakiwa.
Pamoja na hoja hiyo iliyoungwa mkono na madiwani wengine wa chama hicho, mwenyekiti wa kikao alimpa nafasi Mkurugenzi wa Jiji, Bw. Juma Idd ambaye alifafanua kwa kutumia vifungu vya sheria jinsi ya uendeshaji wa vikao na namna ya uwasilishaji wa mihtasari ya vikao kwa ajili ya kujadiliwa katika kikao cha baraza hilo.
Bw. Idd alisema kuwa kimsingi ajenda zote zinazoletwa katika kikao cha baraza hupitishwa katika vikao vya kamati mbalimbali ikiwa ni vikao vya vyama mbalimbali ambapo kwa jiji hilo ni pamoja na CCM, CHADEMA, NCCR na TLP ambapo alisema kuwa katika kikao hicho huletwa mambo yaliyokwisha jadiliwa.
Hata hivyo, alisema kuwa diwani anaruhusiwa kuwasilisha ajenda mapema kabla ya kikao, ili kutoa muda wa kuandaliwa majibu na watalaamu na kisha kuletwa katika kikao hicho ambacho ndicho cha mwisho kwa mujibu wa kanuni.
Pia alisema kamati zinao uwezo wa kupitisha mambao yake na kisha kuanza utekelezaji bila ya kufikisha kwenye baraza hilo.
Baada ya ufafanuzi huo ndipo Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji na Mazingira, Bw. Boyd Mwabulanga aliposimama na kutaka kupewa nafasi ya kuchangia mjadala huo lakini hakupewa nafasi, ila mwenyekiti aliamua jambo hilo kwa kupiga kura ambapo madiwani wa CCM, NCCR walisimama, na kufanya wa CHADEMA kutoka nje wakiongozwa na wabunge wa chama hicho.
Nje ya ukumbi, Mbunge wa Mbeya Mjini, Bw. Joseph Mbilinyi na mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Naomi Kairuki Mwakyoma wakizungumzia walisema wanasikitika kuona haki ya wananachi wa Mbeya inanyakuliwa kwa misingi ya kisiasa.
Bw. Mbilinyi alisema kuwa wameamua kutoka ili kuunganisha nguvu ya umma na kujiepusha kuwa sehemu ya maamuzi mabovu yanayoweza kuamualiwa kutokana na mihtasari feki waliyoletewa, ambayo katika kikao chao cha chama walikubaliana kuikataa.
Alisema kuwa baada ya kutoka, madiwani wa CCM wakiamua kupitisha ajenda hizo, wao watatumia nguvu ya umma kwa kwenda kwa wananchi kuwaeleza kila kitu kilichojificha ili hatimaye waamue yupi ana haki waliokataa kushiriki au wale waliobaki kupitisha mambo yasiyofaa.
Mbunge huyo aliyeonesha kuchukizwa na kitendo hicho, alisema kuwa anamuomba Waziri Mkuu kuunda tume kuchunguza uendeshaji wa kisiasa huku akimrushia kombora Meya Kapunga kuwa anandesha halmashauri kama afanyavyo kwa wadhifa wake wa Katibu Mwenezi wa CCM.
Naye Mbunge Mwakyoma alisema kuwa hatua waliyoichukua ndiyo inayochukuliwa na nchi zote zilizoendelea ambapo alisema kuwa ni ya kuonesha mshikamano na kutotaka kuburuzwa katika mambo ambayo ni haki yao ya kimsingi.
Meya Kapunga baada ya madiwani hao kutoka alisema kuwa kikao hicho kwa mujibu wa kanuni na kwa kuwa hajawafukuza kinaendelea kama kawaida kwa kuwa anachoamini yeye ni kuwa wametoka kwa mambo yao.
Diwani Mwabulanga wa Kata ya Forest ambaye ndiye alianza kushawishi wenzake kutoka, alisema kuwa yako mambo ya msingi likiwemo la kuungua kwa Soko la Sido, kugawiwa kwa Mlima wa Nonde Itiji kwa watu wanaoharibu mazingira kwa maslahi ya kisiasa na Kamati ya Fedha kutumia mamilioni ya fedha za Jiji kwa kinachoelezwa ni kuwachunguza madiwani CHADEMA.
Aliyeuawa kufanyiwa hitma
Naye Tumaini Makene anaripoti kuwa wakati CHADEMA kimeanza kuhoji maswali juu ya utata na mazingira ya kifo cha kada wake, Bw. Mbwana
Masoud, ambaye maiti yake iliokotwa katika pori la magereza,
Igunga, leo mchana kimeandaa hitma kumwombea.
Hitma hiyo ambayo kimesema itakuwa ya kitaifa itafanyika saa saba mchana nyumbani kwao marehemu eneo la Kwa Njongo, Magomeni Makurumula na kuhudhuriwa na viongozi wakuu, akiwemo Katibu Mkuu,
Dkt. Willbroad Slaa.
Akizungumza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mafunzo na Oganaizesheni ya CHADEMA, Bw. Benson Kigaila alisema kuwa chama hicho kinauchukulia msiba huo kuwa ni wa kitaifa kutokana na kada huyo kufa akiwa katika uwanja wa mapambano akipigania haki, hivyo ni pigo kwa wapenda demokrasia wote nchi nzima.
Naye Mkurugenzi wa Uenezi na Habari, Bw. Erasto Tumbo alisema wanataka taarifa ya uchunguzi uliofanywa kwa mwili Bw. Masoud itolewe wazi ili kila mwananchi aje kilichobainika.
hakiki tumepokea msiba huu kwa masiKitiko makubwa pole kwa familia na kwa chama cha chadema na watanzania wapenda Demokrasi DAMU YAKE ITAWALILIWA DAIMA .
ReplyDeleteziku zote harakati za ukombozi zina gharama,ipo siku ukombozi utatimia
ReplyDeletePOLENI WAPENDA MAGEUZI YA KWELI KWA KUMPOTEZA MPAMBANAJI.KAZI NDIO KWANZA IMEANZA .
ReplyDelete