18 July 2011

SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA

Viongozi wa dini sasa wajisalimisha
*Wakiri kufanya biashara hiyo muda mrefu
*Watoa ushuhuda mbele ya kamati ya maadili

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi, Zanzibar

VIONGOZI sita wa madhehebu ya dini ambao wanajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa
Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.

Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amesema baada ya viongozi hao kuhojiwa, waliiomba kamati hiyo kutowataja hadharani au madhebebu yao wakihofia kubezwa.

Akizungumza mwishoni mwa ziara yao visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, alisema orodha hiyo na wengine 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wanasiasa ambao wanajihusisha na biashara hiyo, itafikishwa kwa Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya nchi.

Mchungaji Mwamalanga alisema ongezeko la dawa za kulevya nchini pia linazihusu nchi mbalimbali duniani ambapo kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kuzungumzia ufumbuzi wa tatizo hilo.

“Mkutano huu pia utapendekeza wabunge wa nchi hizo na Bunge la Afrika ya Mashariki, kutunga sheria za kuwafilisi wale wote waliojilimbikizia mali kutokana na biashara ya dawa za kulevya kwa nchi wanachama,” alisema Mchungaji Mwamalanga na kupongeza juhudi za Jeshi la Polisi kukabiliana na ongezeko la dawa hizo.

Akizungumzia kero ya dawa za kulevya visiwani hapa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Aziz Juma Mohammed, alisema kuwa jeshi hilo limekuwa likiwakamata wafanyabiashara na watumiaji wa dawa hizo na kuwafikisha mahakamani.

Kamanda Mohammed ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali wa usalama, kusaidiana na jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wale wanaojihusisha na mtandao wa dawa hizo.

Wiki iliyopita watu wawili wakazi wa Dar es Salaam, walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa nyakati tofauti wakitokea nchini Brazil ambapo kila mmoja alipatikana na kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya aina ya Cocaine.

14 comments:

  1. Kwa hiyo JK alikuwa sahihi.

    ReplyDelete
  2. jamani wote watajwe tu hakuna haja ya kuwaficha wakati waumini wanaamini wachungaji kumbe sio ni wauza unga wanawaharibia watoto wao plz tajeni hao wachungaji.

    ReplyDelete
  3. Kama ni kweli wapo basi na watajwe!!!! hadharani kweupe kabisa bila kuficha chochote! Hii itasaidia kujua kama ni kweli au serikari inaleta saisa ktk jamob hili. naomba sana serikari ifanye kazi yake kama kawaida bila kuficha! asante. Mwl sendoro.

    ReplyDelete
  4. Zote ni porojo tu,hakuna mfanyabiashara wa hiyo kitu atakiri bila kuwa amekamatwa,nyinyi viongozi wa dini uchwara acheni longolongo na kujiingiza kwenye politiki msizozijua.

    ReplyDelete
  5. Hii ni ajabu, leo hii serikali inafanya siri ya majina ya watu wanaoangamiza taifa letu kwa madawa y akulevya. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya ........ Mimi kwa nguvu zangu zote nasema haya majina hayapo! na huu ni usanii wa hii serikali yetu. Hivi mharifu anaweza kufanywa siri wakati amejitokeza mwenyewe!!!! yale yale ya EPA!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. Nyie polisi mnashangaza sana, iwapo mtu kakili mwenyewe mnasubili nini kumfikisha mahakamani? au na hao wana kinga kama vigogo wengine?

    ReplyDelete
  7. JK wake up please!! hawa ni wananchi kama sisi ne wanaua watoto wetu!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. Hakuna viongozi wa dini zinazotambulika Tz wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya. Kama wangekuwepo wangetajwa. Kusema wapo lakini wanabakia anonymous maana yake HAWAPO. Hiyo ni siasa tu ili kuhalalisha alichosema rais. Tangu lini mharifu akakiri makosa yake halafu akafichwa jina lake, eti "wakihofia kubezwa"???

    Tzs wake up and stand up for the truth!

    ReplyDelete
  9. wapo wahalifu wengi wanaokiri makosa yao. wanaobisha waende kwa kakobe. kule wamejaa kibaao. hii haipo tanzania tu. wapo hata marekani. wengi wanatimia miamvuli ya uongozi wa dini kufanya madudu yao. wengine ni wafi_raji

    ReplyDelete
  10. Iwapo wao ni viongozi wa madhehebu yalioanzishwa hivi karibuni, inawakilisha nia ya adhma ya madhebu hayo! hii ina maana kwamba lengo sio kueneza imani kama ilivyotarajiwa. Sasa basi, ni vema kwanza madhebu yao yakafungiwa! Pili, watajwe hadharani kwa kuwa tayari wameshirikiana na viongozi wa nchi kwa maana ya wanasisa na pengine wanaohusika na kusajili madhebu haya. Na tatu, wachukuliwe hatua kali kwani wamekiri! lkn pia, wamechangia sehemu kubwa sana ya kudhoofisha uchumi wa nchi yetu kwa kuharibu vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa la sasa.

    ReplyDelete
  11. haya ni maajabu !!! kuogopwa kubezwa , wao mbona hawakuopgopa kuwaharibu akili vijana wetu? walipwe kwa kadri ya matendo yao, watajwe tu .

    ReplyDelete
  12. Watajeni, kama ni kweli. Twataka kuwajua hao mafisi waliovalia ngozi ya kondoo

    ReplyDelete
  13. kama hao viongozi ni waharibu kihivyo,watajwa watu wazoee yaishe,wengine wajifunze.kukaa kimya ni dhana potofu ya kuogopana.mbona mafisadi wa nchii tena watu wakubwa walitajwa live,na watu wamezoea yamekwisha.bila kuwataja ni makosa makubwa.hili walijue.wanalea ujinga.ndo kujivua gamba,ni pamoja na kuwa mwazi kwa pale penye makosa kupakosoa.

    ReplyDelete
  14. MALI ZAO ZITAIFISHWE YAPEWE MASHIRIKA YANAYOHUDUMIA WENYE MATATIZO YALIYOSABABISHWA NA MADAWA YA KULEVYA PIA ZISAIDIE MITAJI YA VIJANA KUANZISHA MIRADI YA KUJIENDELEZA HASA WALE WASIO NA KAZI.

    ReplyDelete