18 July 2011

Maaskofu wamkataa mchungaji wa 'ajabu'

Na Masau Bwire, Kibaha

BARAZA la Maaskofu wa Makanisa ya Pentecoste (PCT) Mkoa wa Pwani limeiomba Serikali kulifunga kanisa la Kiristo lililopo Maili Moja, Kibaha mkoani hapa na
kumchukulia hatua kali za kisheria mchungaji Joseph Bagule, kwa kupandikiza waumini wake imani potofu.

PCT mkoa wa Pwani kupitia kwa katibu wake, Askofu Gelvas Masanja,ilitoa tamko kupinga na kulaani ibada inayotolewa na mchungaji huyo, na kuita kanisa hilo kuwa la shetani na ya kitapeli.

Waliomba Serikali ichukue hatua za haraka kumshughulikia mchungaji huyo na kanisa lake, kabla hajaleta maafa makubwa kwa Watanzania.

Mchungaji Bagule anadaiwa kuwakataza waumini wake kwenda hospitali na kutumia dawa ya aina yoyote wanapougua akidai kwa kufanya hivyo ni kumkufuru Mungu wao mwenye kutibu kila aina ya ugonjwa.

Mchungaji huyo pia anadaiwa  anadaiwa kufarakanisha familia kwa kuwazuia waumini wake kukaribiana wala kushirikiana na ndugu yeyote ambaye si muumini wa kanisa hilo.

Askofu Masanja alisema kitendo cha mchungaji huyo kuzuia waumini wake kutibiwa hospitalini ni cha mauaji na kukifananisha na mtu anayeweza kumchinja mwenzake mithiri ya kuku.

Askofu Masanja alisema PCT ina uhakika dhehebu hilo halina usajili na halijaandikishwa kisheria na kwamba, dhehebu hilo halipo katika umoja wa baraza lolote la makanisa linalotambuliwa ikiwa ni pamoja na CCT na TEC, hivyo kuiomba serikali kulifunga dhehebu hilo haraka iwezekanavyo.

Alisema  PCT mkoa wa Pwani itahakikisha dhehebu hilo linafutika Pwani na kuzuia imani nyingine potofu kuwepo mkoani humo.

Askofu Masanja alisema, imani ya mchungaji Bagule ni sawa na bomu lililotegwa ambalo wakati wake ukifika iwe isiwe lazima lilipuke. Aliwataka  waumini wa mchungaji huyo kuikana imani hiyo kwa kuwa si ya Mungu bali ya shetani.

Jeshi la polisi mkoani Pwani tayari limechukua hatua kwa kumkamata na kumhoji mchungaji Bagule kuhusu tuhuma zinazomkabili ikiwa ni pamoja na kutaka kujua kama kanisa hilo limesajiliwa ama la.

Mwisho.
9999999

5TH:
CUF wafurahia kujiuzulu Rostam
Na Rabia Bakari

CHAMA cha Wananchi (CUF), kimefurahishwa na taarifa za kujiuzuru aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Igunga, mkoani Tabora, Bw. Rostam Azizi (CCM) na kusema uamuzi huo, utakiyumbisha chama hicho mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, alisema kuyumba kwa CCM mkoani humo ni nafuu kwa  CUF.

“Bw. Azizi ndio alikuwa nguzo nguzo kuu ya CCM hivyo kuondoka kwake tunaamini CCM itayumba, aliathiri upinzani mjini Tabora kwa kiasi kikubwa kwani alikuwa akikubalika na wengi,” alisema Prof. Lipumba.

Alisema Bw. Aziz anapaswa kufahamu kuwa, biashara na siasa ni vitu viwili tofauti hivyo kama ameamua kuacha siasa hapaswi kujiiingiza katika malumbano ya yoyote ya kisiasa.


Akizungumzia uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo hilo, Prof. Lipumba alisema CUF ina uhakika wa kuchukua jimbo hilo kwa sababu wanakubalika na wapiga kura.

Aliongeza kuwa, katika uchaguzi mkuu mwaka 2010, hakuna chama chochote cha upinzani kilichothubutu kupambana na Bw. Aziz katika jimbo hilo isipokuwa CUF lakini walishindwa baada ya kuzidiwa kifedha na mgombea huyo.

“Pamoja na mgombea wetu kufanya kampeni kwa baiskeli, bado alipata kura za kutosha, hali inayoonesha kuwa anakubalika hivyo basi hatuna wasiwasi katika uchaguzi mdogo, tutafanya vizuri kama hapatakuwa na uchakachuaji wa kura,” alisema.

2 comments:

  1. poa , cuf tafuteni mgombea makini na mumsaide . lakini chadema mjue watawaingilia na kujifanya wao ndo wanajua , matokea yake wote mtalikosa hilo jimbo hivihivi.

    ReplyDelete
  2. Napenda kuipongeza chama cha CUF kwa mwongozo na maendeleo bora na kufatilia shida za wananchi kwa ujumla. Zingatieni mwenendo huo na fursa iko mbele ya macho ya wananchi. Achene porojo za kisiasa na upakaji mafuta kwa ajili ya manufaa yenu hiyo ni njia fupi haifikishi mbali na punde ikibainika itakuwa dowa jeusi katika maendeleo yenu. Ukweli na ukhalisi wa maneno na vitendo ni ufunguo wa miyoyo ya wananchi. Hakuna mtu anayependa ulaghae wa maneno kila binadamu anapenda ukweli na mwongozo wa halali bila upendeleo.

    Asanteni Mungu awafungulie kila la kheri nawaombea Mwongozo mwema wa nchi Takatifu ya Tanzania. Ndugu yenu Hilal Masaud Aljabri(hilights@omantel.net.om)

    ReplyDelete