19 July 2011

Mhudumu wa ndege amponda Ashley Cole

LONDON, Uingereza

MHUDUMU wa ndege aliyefanya mapenzi na mwanasoka Ashley Cole, amesema kuwa, Cheryl Cole anatakiwa kuachana naye moja kwa moja kwa kuwa si tu ni mtu anayepanda
kufanya mapenzi nje ya ndoa, lakini pia ni goigoi katika nyanja hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Sun, Kerry Meades mwenye miaka 29, aliwahi kula uroda na nyota wa Chelsea  mwenye miaka 30, wakati alipokuwa akimsaliti mkewe muda mfupi kabla ya tabia yake hiyo kuwekwa hadharani.

Lakini, Kerry ameeleza kukerwa na tabia yake ya kuvuta sigara, kutembea uchi na kula kidogo baada  ya kwenda naye katika klabu moja ya usiku mjini Los Angeles.

Kerry amesema hayo baada ya kusikia kuwa, Ashley amejitahidi kumshawishi Cheryl mwenye miaka 28 kurudiana naye, baada ya kuachana.

Kerry alisema: "Ninamsikitikia Cheryl. Nimeachana naye kwa sasa kabla ya kuchelewa."

Rafiki aliendelea: "Mara aamkapo asubuhi, huomba kuvuta sigara. Alisema kwa wastani anavuta sigara kama 30 kwa siku.

"Na anakunywa pombe kali za tequila na vodka.

"Mara chache anaonekana akila na anapokula, basi hula vyakula visivyokuwa na virutubisho. Chakula pekee alichokula mdomoni mwake ilikuwa ni kuku wa kukaangwa baada ya kulewa usiku na kula chakula kidogo asubuhi."

Habari hizo zimekuja baada ya wiki chache tangu Ashley kuwa pamoja na Cheryl usiku, siku chache baada ya kuungana Julai Mosi.

Mfanyakazi wa Virgin Atlantic, Kerry aliyewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Cole mwaka 2004, aliongeza: "Sifikirii kama Ashley ana wazo la kuwa mzuri."

No comments:

Post a Comment