11 February 2011

Wabunifu kushiriki maonesho ya mavazi ya harusi, mapambo

Na Amina Athumani

WABUNIFU 32 wa vitu mbalimbali vya maharusi wanatarajia kushiriki maonesho ya pili ya mapambo na vitu mbalimbali vya harusi   yatakayofanyika
Machi Mosi hadi 3, katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.

Washiriki hao ni wabunifu wa mavazi waliobobea katika fani hiyo yakiwemomavazi ya harusi na mapambo .

Akizungumza Dar es Salaam jana, mwandaaji na msimamizi wa maonesho hayo, Mustafa Hassanali, alisema mwaka huu yatakuwa makubwa, mazuri na yenye mvuto, zaidi ya mwaka jana.

"Maonesho ya harusi ya mwaka huu, ni maonesho ambayo uboreshaji wake umevuka kutoka siku mbili za maonesho hadi siku tatu, huku likiongezewa na kujumuisha vionjo vingi zaidi," alisema Hassanali.

Alisema maonesho hayo  ambayo hufanyika kila mwaka, huwaleta pamoja wahusika wote wa mambo ya harusi katika kujenga na kutengeneza mtandao wa kimafanikio baina yao.

Maonesho ya mwaka huu yatapambwa na vitu kama keki, maua, wapiga picha na magauni ya harusi.

No comments:

Post a Comment