SAINT-DENIS, Ufaransa
MSHAMBULIAJI Karim Benzema amefunga bao katika mechi yake ya tatu ya mafanikio ya timu ya Taifa, ambalo limeiwezesha Ufaransa kuibuka na
ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brazili.
Ushindi huo, umeonesha kuwa, timu hiyo ya Ufaransa kiwango chake kimeongezeka kupanda ikiwa chini ya Kocha mpya, Laurent Blanc.
Mchezaji huyo wa timu ya Real Madrid, alipachika bao hilo usiku wa kuamkia jana, dakika ya 54, baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Jeremy Menez, aliyepanda na mpira kutoka nyuma na kummegea pasi mfungaji.
Hata hivyo, mchezaji huyo angeweza kufunga zaidi ya mabao matano, lakini mlinda mlango wa timu ya taifa ya Brazil, Julio Cesar, alipangua mashuti mawili ya Benzema, likiwemo moja ambalo lilikuwa likielekea kimiani.
Ushindi huo wa mara tano mfululizo kwa Ufaransa, unaashiria kuwa, kikosi hicho kwa sasa kimeimarika chini ya kocha Blanc, ambaye alikabidhiwa mikoba ya ya Raymond Domenech, baada ya timu hiyo kuvurunda mwaka jana katika fainali za Kombe la Dunia.
Ushindi dhidi England na Brazil ni lazima utufanye tujiamini zaidi,¦ alisema Blanc. Matumaini yetu tutaweza kuutumia ushindi huu katika mechi zijazo za kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya 2012," aliongeza.
Kabla ya kufunga bao hilo, Benzema alipachika bao katika mchezo ulioikutanisha timu hiyo na England, na timu hivyo kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo huo uliofanyika mjini Luxembourg mwishoni mwa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment