Na Amina Athumani
TIMU za Tanzania zimeendelea kunyanyaswa katika mashindano ya mpira wa kikapu ya Kanda ya Tano, yanayofanyika mjini Kigali Rwanda.Jana,
katika michezo yake, Tanzania kwa upande wa wanaume ilipoteza kwa kufungwa pointi 54-51 dhidi ya Kenya na wanawake wakafungwa 55-53 na Ethiopia.
Kwa matokeo hayo, Tanzania imepoteza mechi mbili kwa wanawake dhidi ya Rwanda na wanaume pia dhidi ya Rwanda, ikiwa haijashinda mechi hata mechi moja.
Pamoja na kufungwa, Tanzania kwa upande wa wanaume wanajipa matumaini ya kuifunga Uganda leo kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, kwa upande wa wanaume Rwanda iliifunga Uganda kwa pointi 89-76, kwa wanawake, Kenya iliifunga Uganda pointi 64-32 na Rwanda ikaichapa Burundi pointi 83-53.
Kwa matokeo hayo, wenyeji Rwanda wanaongoza michuano hiyo kwa upande wa wanawake na wanaume, timu zote zikishinda michezo yote mitatu iliyocheza, zikiwa na pointi sita kila moja na kufuatiwa na Kenya.
Tanzania kwa upande wa wanawake, leo itamenyana na Kenya. Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe, alisema mchezo huo kwa upande wa wanawake, utakuwa mgunu kuliko mchezo wa Tanzania na Uganda kwa upande wa wanaume.
No comments:
Post a Comment