18 February 2011

Wabunge wahofu siasa, hujuma jeshini

Na Waandishi Wetu

BAADHI ya wabunge wameonesha wasiwasi wao kuhusu ulipukaji wa mabomu na kusema kwamba ni uzembe wa serikali hujuma na huenda
siasa zimeingia ndani ya jeshi.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti waliyasema hayo wakihojiana na Majira baada ya Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda kuahirisha Kikao cha Bunge akisema kwamba hali inatisha, Watanzania wote wako katika hofu hawajui familia zao ziko wapi, hivyo hawawezi kuendelea na shughuli za bungeni.

Mbunge wa Arusha Mjini, Bw. Godbles Lema (CHADEMA) akitoa maoni yake kuhusu janga hilo alisema kuwa kutokea kwa milipuko ya mabomu mara kwa mara katika kambi za kijeshi ni uzembe wa serikali na inaonesha kuwa ndani yake kuna masuala ya kisiasa.

Alisema kuwa suala hilo linaonesha kuwa kuna mtu anayetafutwa ndani ya uongozi ili aweze kuangushwa na kubainisha kuwa siasa za nchi hii zimeenda ndani zaidi hadi kufikia jeshini.

"Ukifuatilia zaidi unaweza kukuta walinzi wa maghala hayo ya silaha hawajafa au kujeruhiwa na kama itakuwa hivyo, basi kuna walakini kwa sababu walitakiwa kuwa wa kwanza kufa," alisema Bw. Lema ambaye pia ni waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.

Alisema kuwa kumekuwa na tatizo kwa nchi hii pindi inapotokea matukio kama haya serikali inakimbilia kuunda tume na kusema kuwa basi tume hiyo itakayoundwa ichunguze kwa makini zaidi na kubaini kilichotokea.

Naye Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya TLP, Bw. Augstino Mrema kwa upande wake alisema kuwa rais achukue jukumu la kuwawajibisha baadhi ya viongozi wanaosimamia masuala ya kijeshi kwani wameonesha kutowajibika kikamilifu katika kusimamia usalama wa maisha ya wananchi.

Alisema kuwa wananchi walidhani kuwa Serikali ilijifunza kitu kwa tukio la Mbagala la kulipuka kwa mabomu ambayo yaliua watu wengi  lakini inaonesha haikujifunza kitu hivyo wahusika lazima wawajibike.

Alisema kuwa Tanzania ijifunze kwa nchi zingine zilizoendelea kuwa ikitokea hali kama hiyo basi wahusika huwajibika kutokana na matukio kama hayo.

Naye Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Bw. Rashid Mohamed alisema kuwa inaonesha kuwa Tanzania haina uwezo mzuri wa kudhibiti silaha.

Alisema kuwa ipo haja kwa serikali kuchukua hatua za dharura kuangalia hali hiyo kwani inaonesha kuwa nchi haiko katika hali nzuri.

"Serikali ambayo ina amani kwanini inakuwa na silaha kama hizo ambazo ni nzito, utunzanji wake unaonesha kuwa si mzuri na umekuwa ukihatarisha maisha ya watu, iliangalie hilo na kujifunza kitu kutokana na matukio," alisema.

Hata hivyo, alisema wananchi walijua serikali ilifanya tathmini na utafiti wa kutosha kwa tukio la Mbagala mwaka juzi na kujifunza kitu ili hali hiyo isijitokeze tena lakini inashangaza kuona kuwa tukio kama hilo linajitokeza tena kwa mara nyingine tena na kupoteza maisha.

Awali Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda akitoa taarifa ya maafa hayo alisema mlipuko ulianza saa mbili usiku katika maghala ya Jeshi la Ulinzi ambapo maghala 23 yameteketea yakiwa na silaha pamoja na mchanganyiko wa mabomu.

Alisema juhudi zilifanyika na viongozi wa jeshi baada ya milipuko kupungua na kubaini mabweni mawili ya jeshi hilo yaliharibiwa vibaya, magari mawili yaliteketea na watu zaidi ya 17 walifariki dunia.

Bw. Pinda alisema maiti waliofikishwa Hospitali ya Amana ni 13, Muhimbili wawili na Temeke wawili na kati ya maiti hizo tatu waliyoka Kitunda.

Alisema majeruhi 145 hadi asubuhi lakini upo uwezekano wa kuongezeka marehemu na majeruhi baada ya kufanya ukaguzi katika maeneo ambayo usiku hayakufikika.

Waziri alisema zaidi ya watu 4,000 wamehifadhiwa Uwanja wa Uhuru, wakazi waliojirani na maeneo ya matukio wanatakiwa kupisha ukaguzi kujua hali ilivyo.

Alisema kuna mabomu yaliangukia Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius, walipendekeza uwanja ufungwe kwa muda na ndege zilihadharishwa kutotumia uwanja huo.

"Rais ameitisha kikao cha dharura cha Ulinzi na Usalama wa Taifa na jeshi liunde tume ya kuchunguza tatizo hilo ili kubaini chanzo na hatua stahiki zianze kuchukuliwa," alisema na kuwapa pole wote kutokana na mtikisiko huo.

18 comments:

  1. Ni kweli,Rashid umenena.Kwa nini tukae na mabomu kama nchi yetu ni amani?????
    Tunaomba viongozi wenye nafasi hizo wajihuzuru mapema bila kulazimishwa.Nasikia tuna usalama wa taifa lakini mimi naona wanakula tu mshahara lakini hawafanyi kazi yoyote.Tunashuhudia mambo kadhaa ambayo nilidhani usalama watadhibiti kabla hayajatokea lakini wanashindwa.Nchi yetu haina ulinzi,watu wananenepa tu na kufungua biashara mtaani badala ya kuwalinda wananchi.

    ReplyDelete
  2. jamani tunawataka viongozi wawajibike kwani hii serikali yetu imetushosha kila kitun kinaenda hovyohovyo lakini ndio vijitu vimeng'ang'ania madaraka pamoja na kuwa vimechoka!!!!!!!!!!!!!!!!!!sasa unategemea shimbo ana mpya? unategemea mwinyi ana jipya? au makamba wa ccm ana jipya? au kikwete anaegoma kumtaja rostam kama mmiliki wa dowans ana jipya?

    WATANZANIA TUMEKWISHA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!KHANGA NA FULANA INCLUDING KOFIA ZIMETUMALIZA JUZI WAMETOKA KUUA ARUSHA,IKAFATA MBARALI,IKAFATA HIFADHI YA WANYAMA NA LEO GONGOLAMBOTO....WATANZANIA TUSITAFUTE MCHAWI TUKO NAE HAPAHAPA HATA MALOW MWANAMUZIKI ALIHAMASISHA SANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Manenoyanayosemwa ni mengi lakini technically lazima tujiulize kwa nini mabomu yanalipuka!!

    1. Je ni kwa sababu muda wake umekwisha hivyo yalihitaji kuharibiwa?

    2. Ni kwa sababu hayakutunzwa vizuri kwa maaana ya unfavarorable temperatures, etc?

    3. Je aina ya mabomu tuliyotunza hayakuwa na kiwango kizuri cha utengenezaji, na hivyo kulipuka bila wanajeshi wetu kujua ( manufactures default?

    4. Au kuna tensions kati ya jeshi na serikali kuhusu kuyateketeza hayo mabovu; kwa maaana ya budget

    6. Suala la neighourhood si la msingi sana kwa sasa kwa maana hata kama kambi ingekuwa kilometres elfu ngapi mbali na makazi ya wanaichi; bado mabomu hayatakiwi kulipuka tu kwani kuna wanajeshi wanatakiwa wawepo eneo hilo

    Jeshi linatakiwa lijibu maswali haya kikamilifu

    ReplyDelete
  4. SERIKALI IMECHEMKA. TUME NDIO WIMBO WA KILA SIKU.WATU WANAKULA POSHO.WANAOMBA WAKIMALIZA HICHO WANACHOKIITA UCHUNGUZI , WANAPIGA JALAMBA KUSUBIRI JANGA LINGINE LITOKEE WACHAGULIWE TENA KWENYE TUME NYINGINE. " EWE MWENYEZI MUNGU FUNGUA FAHAMU ZA HAWA VIONGOZI WETU WEKA UPENDO NA UZALENDO WA KWELI NDANI YA MIOYO YAO, ILI MAMBO WANAYOYAPANGA WAYATEKELEZE , YASIISHIE KWELNYE MAFAILI TU, TUNAHITAJI KUONA KUWA WANATUJALI, NA SIYO KUTUUPUZA NA HUKU WAO WAKINEEMEKA, JINSI WALIVYO NI WEWE MUNGU ULIWAJALIA WAWE HIVYO WASIJE WAKAJIVUNA NA KUONA KUWA WAO WAMESOMA SANA. EWE MUNGU , UTUSIKIE, AMANI ULIYOTUJALIA TUIIHIFADHI KWA JINSI INAVYOPASWA, NA VIONGOZI KUSIMAMA KATIKA NAFASI ZAO SAWASAWA.AMINA." VILE WANAPASWA KUFANYA.ZIRI JIUZULU.

    ReplyDelete
  5. well,
    kwa muda watanzania watazungumzia mambo ya mabomu na kusahau mengine.. mi sisemi sana. but i know it is conspiracy

    ReplyDelete
  6. Mungu kakasirika baada ya Maaskofu kubariki dhambi za Slaa kuchukua mke wa mtu na wao badala ya kukemea wanasema ni masuala binafsi,sasa hii ni adhabu na zingine zinakuja,mnaua maalbino kutafuta pesa,mnadhulumu masikini na mahakama hazitoi haki,ole wenu tubuni kwa Mungu.

    ReplyDelete
  7. Nimejua sasa kuwa hata wabunge wetu uwezo wao wa kufikiri bado ni mdogo, Mbunge mkongwe na anayetegemewa anasema kwa nini tuwe na silaha nzito (makombora) wakati Tanzania kuna amani, nani alikwambia makombora ni kwa ajili ya Usalama wa ndani? Kama hamjui mambo ni bora muulize ili mfahamishwe. Mnadhani siku zote Tanzania itakuwa na majirani wema????? rafiki wa leo ni adui wa kesho. We must avoid hasty conclusions.

    ReplyDelete
  8. Kwa kweli kauli ya Mbumge mmoja kuwa walinzi wa maghala ya silaha ilikuwa wafe wao imenitia hofu sana juu ya uwezo wake wa kufikiri. Hivi hajui kuwa walinzi wale wanajua mbinu zote za kujiokoa kama kutatokea milipuko yoyote? Kwa kweli upeo wa mheshimiwa huyu ni mdogo sana. Pia naomba ieleweke kuwa hii sio hujuma bali ni ajali kama ajali zingine ila tuanze kuwa makini juu ya matukio haya. Pia sheria za makazi zitumike sawa sawa ili kuzuia wananchi kujenga nyumba za makazi karibu na makambi ya jeshi.

    ReplyDelete
  9. Mimi ni yule yule Hafidh kutoka Zanzibar,kwanza kabisa napenda kutoa pole kwa wahanga wote waliopatwa na kadhia ya mabomu - Gongolamboto. Mwenyezi Mungu awaponye haraka na wale waliotangulia basi Mungu akawaeke mahala pema peponi-Amin.
    Pili napenda kutoa mchango wangu kwanza kwa mbunge Hamad Rashid mawazo aliyoyatoa sikubaliani nae hata kidogo hata kama sote tuna itikadi moja ya kisiasa. Unaposema eti Tanzania ina amani na majirani zetu tunaishi nao kwa amani na upendo na hakuna haja ya kua na silaha nzito Tanzania ! hapo umechemka au ndio umelewa na fikra potofu. Hoja yake haina msingi kwa sababu adui yako si lazima awe karibu yako tu , kuna nchi ngapi duniani zinavamiwa na adui kutoka mbali ?!! kama hiyo haitoshi kua na rafiki yako mzuri haina maana atakua mzuri milele !! nanukuu msemo wa Robert Nesta Marley - anasema rafiki yako mpenzi anaweza kua adui yako na adui yako anaweza kua rafiki yako mzuri. so huwezi jua nini kinaweza kutokea badae, kujiweka tayari kwa kila kitu ni busara zaidi. usisubiri kushambuliwa ndio unaanza kutafuta silaha wakati adui yako anakushambulia kwa silaha za kisasa na nzito. waheshimiwa kueni makini na mnayosema.

    Mungu ibariki Tanzania ,Mungu ibariki Zanzibar na watu wake.

    ReplyDelete
  10. Kwanza napenda kutoa RAMBIRAMBI zangu kwa ndugu wote waliofiwa na jamaa zao katika msiba ulio sababishwa na wapotevu wa USALAMA wa wananchi.Pia nawaombea majeruhi wote Mungu awaafu na awaepushe na mabaya. Huu ni msiba wa pili kutokea baada ya muda mchache tu kupita toka ulipotokea ule wa kwanza 2009 na bila kuchukua hatua yoyote ya kulinda USALAMA wa watu na maisha yao.Naomba BUNGE la Taifa lichukuwe hatua ya makini sana kuchunguza jambo hili ambalo sio la kawaida, mambo kutokea kila mara na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa kuepukana na msiba kama huu.Msisahau kuwa wanaohitaji silaha za magendo wanawazunguka pande zote kwa hiyo mbinu za kila aina hufanyika ili kuuza silaha na hii ni moja wapo ya kufunika pengo la silaha zilizo kosekana au zilizo toweka kutoka katika HIFADHI ya Jeshi (WAREHOUSE).Mimi ni profesa wa upelelezi na ninahisi kuwa kuna mchezo umefanyika wa madhara kwa Taifa la Tanzania.Mimi sio mkazi wa hapo lakini Roho huniuma ikitokea kitu cha madhara kwa wananchi au kwa Taifa.Tanzania ni nchi yangu ya pili na nitaitetea mpaka kufa kwangu kwa sababu sisahau fadhila za Elimu nilizopata kutoka huko.(Hilali Masudi Aljabri-Muscat Oman.email:hilights@omantel.net.om

    ReplyDelete
  11. me i wonder hivi huko bongo wabunge pia wanavuta bangi, eti mbunge asema siasa zimeingia jeshini ! ina maana wanasiasa kazi yao ni kuuwa watu na daz why sometime anasema yuko tayari kupigwa risasi oh nchi haitatawalika huyo anafaa akawe mbunge rwanda coz i think atapata doze kwa mzee Kagame and I DEDICATE DA SONG BY THE LEGEND OF RAP 2pac hit 'em all coz he deserve dat pwaaaaaaaa to devil less lema

    ReplyDelete
  12. mimi naamini siasa imeingia jeshini maana hata jenarali A .shimbo aliingia kwenye siasa alipoahidi kuwaua wapinzani kama watakataa matokeo ya kupanga katika uchaguzi mkuu 2010 KUKIPA CCM USHINDI.

    Huyu anaefanananisha Tanzania na Rwanda kaishiwa fikra maana Rwanda sasa hivi ni peponi zaidi ya tanzania. Miundombinu ya rwanda iko juu,usafi wa miji upo juu,uchumi upo juu sana 27 kwa sh 1 ya rwanda,Hakuna rushwa wala ufisadi na wananchi wana heshima na utu.Hivyo si vema kulinganisha tanzania nchi iliyojaa uchafu wa kila aina chini ya utawala wa ccm!

    ReplyDelete
  13. Ni kweli why hata mmoja asijeruhiwe? mbona mbagala walikufa kama wanajua kujihami?

    Mimi naona hii milipuko ilipangwa si bure!SHIMBO ANA LA KUJIBU MAANA AMEINGIZA SIASA JESHINI(JWT)

    ReplyDelete
  14. Mabomu, Majambazi, Ajali za barabarani, Magonjwa yanayotibika, njaa, umasikini vyote hivi na vingine vinamtafuna mtanzania huyuhuyu. Tunaomba sana rerikali ijitahidi kuongeza umri wa kuishi wa Mtanzania maana si kwamba yote haya hayaepukiki,inawezekana kabisa hata yakaisha kabisa.

    ReplyDelete
  15. Watanzania! Lugha ya Taifa letu ni Kiswahili! Na Lugha hii inatosha kabisa kujieleza. Ninasikitika kuona watu wakichanganya na kuingiza lugha nyingine hasa Kiingereza. Kama unachangia jambo kwa lugha basi chagua moja kama unaona unaweza kujieleza vizuri kwa Kiingreza au lugha nyingine fanya hivyo. Wajeruumani hawatumii mchanganyiko wa lugha. Kuchanganya lugha ni umamboleo.

    ReplyDelete
  16. We Anonymous hapo juu, kila mtu anao uhuru wa kujieleza kwa lugha anayotaka na anayoweza kujieleza vizuri. Mbona hujalalamika matahira wa vyombo vya habari wavyochafua Kiswahili kwa maneno kama vile "kuua" "kuchinja" wakiwa na maana ya kushinda mchezo. Mbona hujalalamika kiarabu kinachoingizwa kwenye lugha yetu ya Kiswahili wakati tungeweza kutumia maneno kutoka lugha kutoka makabila yetu hapa nchini? Wee vipi? Kama kimombo kinakushinda nenda shule kajifunze.

    ReplyDelete
  17. Sasa Watanzania wanalalamika nini wakati wakijua obovu na uozo wa ccm na serikali yake? Mlitegemea nini juzi hapo mkiwapigia kura na vigelegele? Huo ndio ushindi wenu. Endeleeni kuikumbatia muone itakapowafikisha. Ni wapi katika serikali hii ambapo hakuna uozo: elimu? afya? nishati na madini? maji? mali asili? serikali za mitaa? mashirika ya uma? mambo ya ndani (na hasa polisi)? mambo ya nje (ambapo mtumishi wa ubalozi anaweza kuvunja sheria za nchi alikotumwa kutuwakilisha na akafanya kosa la jinai la kumwingiza Mtanzania nchini kumsaidia mkewe kuendesha biashara ya "mama ntilie") wakati kwa miaka minne balozi wetu alijua na hakuchukua hatua yoyote hadi mambo yamelipuka! Aibuuuu. Wanaccm mmetuweka pabaya, na nyie wenyewe ndo mnakuwa wa kwanza kulalamika.

    ReplyDelete
  18. Huyo jamaa aliyejibu maoni yangu kuhusu lugha naona hakunielewa vema. Mimi ni Mtanzania na ninafahamu lugha kadhaa na pia kuzimudu sana tena hata kuzifundisha: Nikiwa nyumbani na bibi yangu yaani nyanya huzungumza naye lugha yetu bila kuchanganya lugha nyingine; kama ni Kisukuma au Kisambaa basi nitazungumza naye bila kuchanganya. Mimi nilipotoa wazo hili niliwataja Watanzania na si kundi la watu kadhaa bali nilimaanisha wote, hata kama ni wewe na pia sikusema kuwa mtu asitumie lugha anayoimudu; ila nilisema watu wasichanganye lugha, kama unaweza kujieleza kwa kimombo basi fanya hivyo. Inawezekana huyo jamaa alikwenda shule kufuta ujinga lakini hakuelimika. Kwenda shule si kujua kimombo tu maana zipo nchi nyingine hazikijui. Upo hapo? Unaijua historia ya Kiswahili? kama unaijua basi kumbuka ya kwamba Kiswahili kimetokana na lugha mbali mbali za Kibantu na Kiarabu, Kijerumani, Kireno na hata Kiingereza kwa ajili ya hilo bado tunatumia maneno kama "shati" baisikeli,bakshishi, shule, meza, maji,nk kungàtuka nk. UPO HAPO?

    ReplyDelete