14 February 2011

St. Aggrey kutimua wanafunzi watakaofeli

Na Charles Mwakipesile Mbeya

TAASISI ya St.Agrey inayomiliki Shule za  Sekondari na Chuo cha Ualimu katika Mikoa ya 
Mbeya na Rukwa Juzi ilitangaza mkakati wa
kuinua kiwango cha elimu katika shule hizo kwa kupiga marufuku mtindo wa kupokea wanafunzi wasio na uwezo na kutimua baadhi walipo katika shule hiyo.

Msimamo huo ulitangazwa katika mahafali ya kidato cha sita na Mkuu wa Chuo cha Ualimu cha taasisi hiyo, Bw. Stewatt Danda

Alisema kuwa uongozi wa taasisi hiyo umechukuwa umuzi huo kwa faida kwa ukuaji wa elimu nchini.

Alisema kuwa  kuanzia sasa hakuna mwanafunzi atakayeruhusiwa kuingia kidato kingine bila ya kufanya vizuri katika masomo yake

Bw. Danda alisema kuwa awali watu walieneza sifa mbaya kwa shule hizo kwa kusema kuwa inapokea  wanafunzi walioshindikana katika shule nyingine hali ambayo aliipinga

Aliutaka umma wa Watanzania ujue kuwa   walizoamua kukifanya kwa ajili ya maendeleo ya ukuaji wa elimu.

Alisema utaratibu huo tayari umeanza  kwa kidato cha tatu ambapo hawataruhusiwa kwenda kidato cha nne kama mwanafunzi hatakuwa na  wastani unaotakiwa.

Hata hiyo Mgeni rasmi huyo alitamba kuwa wana uhakika na wanafunzi hao kutokana na jinsi walivyowandaa na hivyo  watatapata mafanikio makubwa yatakayoweza kuwafikisha katika ndoto yao ya kuwa wasomi wakubwa nchini.

Naye Mhasibu Mkuu wa taasisi hiyo, Bi.Neema  Mwambusi akitoa nasaha zake alisema kuwa lengo la muasisi wa shule hizo hayati Sir Agrey   Mwambusi ilikuwa ni kuhakikisha  anatengeneza kituo bora cha kutengeneza wa wasomi watakaoisaidia nchi kupiga hatua.

3 comments:

  1. Kufukuza ni kushindwa kazi. Kama kweli mmedhamiria, swala muhimu ni kuhakikisha kwamba kila mmoja wa wanafunzi wenu anakuwa na uelewa mpana wa masomo anayofundishwa. Itakuwaje mwanafunzi afike hadi kidato cha tatu halafu ashindwe kuelewa, au ashindwe kufaulu hata mitihani ya hapohapo shuleni? Hamuoni kwamba kumfukuza mtakuwa hamjamtendea haki mlezi wake aliyemlipia kwa muda wote huo mpaka kumfikisha hapo alipo? Inatia moyo kwamba mmeweka dhamira safi, lakini pamoja na dhamira hiyo kwa wanafunzi, iwepo pia kwa walimu ambao masomo yao watoto watafeli.

    ReplyDelete
  2. JAMAN SIR AGGREY MWAMBUS IMETOKA WAPI TENA? ALIPATA LINI CHEO HICHO? KWA LIPI? ETI SIR

    ReplyDelete
  3. Kwa hili st Aggrey mmenena kama kweli mnataka kiwango cha elimu kukua,lakini wasiwasi wangu ni kweli utekelezaji utakuwa asilimia mia?maana kwa maneno tunawakubali implementation zero anyway yetu macho tungoje tuone.Halafu hili lisiishie kwa st Aggrey tu liende mbele wizarani kuleta mfumo mpya wa kila mwanafunzi kupata mchujo kila anapo ingia darasa jipya kwa kufanya hivyo Tanzania tunaweza kupiga hatua vingivyo ni hadidhi za abunuasi na mwisho wa siku tunapata wasomi vilaza na wataalam wa kuchakachua nahivyo kuiingiza nchi gizani.

    ReplyDelete