Na Amina Athumani
TIMU nane za mpira wa kikapu zimeanza zinakaribia kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), kwa
kuongoza katika makundi yao.
Katika kundi A, timu zinazoongoza ni ABC yenye pointi saba ikifuatiwa na Chui yenye pointi saba na Hopolife yenye pointi saba, huku zote zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa, wakati JKT ikiwa na pointi sita.
Kundi B, linaongozwa na Pazi ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Tanzania Prisons yenye pointi sita, Savio pointi sita na Vijana pointi sita, huku zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa mashindano hayo ya RBA, Zabron Manase, alisema timu zitakazokata tiketi hiyo, zitatangazwa baada ya kumalizika kwa michezo yote ya makundi.
"Tunasubiri hatua ya makundi imalizike ili tujue timu zilizotinga hatua ya robo fainali," alisema.
Alisema baadhi ya timu zimefungana pointi, wakati nyingine hazijamaliza michezo yao ya hatua ya makundi, hivyo hawataweza kuzitangaza kwa sasa.
Manase alisema ligi hiyo bado ni ngumu, hasa baada ya bingwa mtetezi, Savio kuzidiwa na wengine wa Kundi B.
No comments:
Post a Comment