21 February 2011

Messi atamani kucheza na Fabregas Barcelona

BARCELONA,Hispania

MSHAMBULIAJI Lionel Messi ameweka bayana akisema kwamba angependa kucheza na mchezaji, Cesc Fabregas katika timu yake ya
Barcelona.

Mshambuliaji huyo wa timu ya Taifa ya Argentina bado anawazia kipigo cha mabao 2-1 ambacho klabu hiyo ya catalan  ilikiambulia katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, Jumatano usiku kutoka kwa Arsenal.

Alisema wanapaswa kufanya marekebisho  wakati kikosi hicho cha Arsene Wenger kitakjaposafiri hadi kwenye uwanja wa  Nou Camp wakati wa mechi ya marudiano itakayofanyika Machi 8, mwaka huu na akasema kuwa angependa kucheza sambamba na nahodha huyo wa Gunners.

Messi aliwaambia waandishi wa habari: "Cesc Fabregas ni mchezaji muhimu kwa Arsenal na kwa ujumla nataka kucheza naye  Barcelona lakini jambo hilo halitegemea kwangu,"

"Ila mwishowe ataweza kufanya kitu ambacho watu wanakitaka Barcelona.Lakini nafikiri mahali pazuri ni Barcelona na hakuna mahali pengine panapoweza kumfaa,"alisema.

Vilevile Messi alikiri kwamba kipigo walichokipta jijini London kimevunja hali ya moyo katika timu hiyo lakini akasema kuwa wanaimani watalipiza kisasi.

No comments:

Post a Comment