LONDON,England
KOCHA wa Chelsea,Carlo Ancelotti amesema kwamba mafanikio kwa timu hiyo katika michuano ya Klabu Bingwa Ulaya ndiyo yatakaikoa baada ya
kushindwa kutwaa kwa mara ta tatu ubingwa wa Kombe la FA.
Timu hiyo iliondolewa katika michuano hiyo na Everton kwa mikwaju ya penalti 4-3 juzi baada ya timu hizo kufungana bao 1-1 katika mechi ya marudiano ya raundi ya nne iliyofanyika kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Wakati Chelsea kwa sasa ikiwa nyuma kwa pointi 12 dhidi ya vinara wa Ligi Kuu, Manchester United na ambayo haina uhakika wa kumaliza ikiwa katika nafasi nne za juu,inatakiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ili isimalize msimu huu bila ubingwa.
Ikiwa wiki hii inakabiliana na timu ya FC Copenhagen katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora mechi itakayofanyika nchini Denmark,kocha Ancelotti bado anaamini kuwa msimu huu bado upo mbali kumalizika.
"Kwa sasa tunaangalia kuzitumia siku zijazo ili kuweza kujiweka sawa kwa ajili ya mechi ijayo ya Klabu Bingwa Ulaya ,"alisema.
"Nafikiri tuna muda.Siyo kazi rahisi lakini tuna muda,inatubidi kwa haraka kuzinduka kutoka katika kipigo hiki,tuna mechi muhimu katika kipindi kijacho inatupasa kwa haraka kuzinduka kiakili,"alisema.
Aliongeza kwamba kila wakati timu inaposhindwa kupata matokeo mazuri mara zote kocha ndiye anayekuwa kwenye shinikizo lakini cha kushangaza anapata msaada kutoka kwa klabu,wachezaji na kwa pamoja watasonga mbele.
No comments:
Post a Comment