*Kila mmoja apewa dk 10 kueleza mafanikio, mikakati
*Pinda atamba na makusanyo ya bil. 400/- kwa mwezi
Na Kulwa Mzee, Dodoma
MAWAZIRI wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, wakiongozwa na
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda juzi walihitimisha mjadala wa hotuba ya bosi wao kwa aina yake, kwa kila mmoja kupewa dakika 10 kueleza mafanikio na mikakati ya wizara zao na serikali kwa ujumla.
Hotuba hizo zilizovuta zilihitimishwa na Bw. Pinda ambaye alisema Rais Kikwete katika uongozi wake amefanya mambo makubwa, ikiwamo kuiwezesha nchi kupata mapato ya ndani sh. bilioni 400 kila mwezi.
Alisema serikali itaendelea kukuza uchumi kwani kwa miaka mitano Rais ameweza kuiingizia nchi mapato ya sh. bilioni 400 kila mwezi, ambalo ni ongezeko la sh. bilioni 200 katika kipindi hicho.
"Serikali imefanya mengi, sina sababu ya kueleza sekta zote, leo tunalaumiwa kwa kushindwa kukuza sekta ya maji, tuulizane mkoloni aliacha visima vingapi," alisema na kuongeza kwamba tumeongezeka kwa idadi ndio sababu na matumizi ya maji yameongezeka, hata hivyo kuna mikakati mingi ya kuboresha sekta hiyo.
Akizungumzia migomo na maandamano ya vyuo vikuu alisema ufumbuzi unatafutwa ili kuimaliza lakini pia kuna upungufu katika suala zima la utoaji mikopo ambao utafanyiwa kazi na tume hiyo iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete.
Alisema kisheria migogoro hairuhusiwi vyuoni, wanafunzi wakigoma siku tatu mkuu wa chuo anaruhusiwa kuwafukuza chuo.
"Kudai haki kwa migomo na maandamano si utaratibu mzuri, watumie njia ya majadiliano ili kufikia muafaka," alisema.
Alitoa mwito kwa wabunge kujiepusha na jambo lolote la kurudisha nyuma juhudi za serikali kwa lengo la kushika madaraka.
Alisema si busara wabunge kubeza shughuli zao zilizowafanya kuwafikisha hapo walipo, na kuhusu suala la Muungano, aliwaomba wanapojadili mabadiliko yaliyofanyika Zanzibar yawe ya kukuza Muungano badala ya kuuvunja.
Waziri Mkuu aliungana na wale wanaosema Muungano hautetereki ni imara na mabadiliko ya katiba Zanzibar yamehamasisha hisia za umoja, upendo, mshikamano na kuvumiliana.
Akizungumzia hoja zilizotolewa na wabunge alisema mjadala umesaidia kuirahisishai serikali kufanya kazi yake.
Wasira na suala la udini
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Bw. Stephen Wasira aliwashambuliwa wale wanaosema nchi haitawaliki wakati wao wanataka madaraka ya kutawala.
Alisema suala la uhuru na umoja halina chama, akitokea mtu anataka kuuza uhuru watakataa kwa gharama yoyote.
Waziri huyo alisema wanasiasa wanawafuatafata viongozi wa dini wanapoona hawawezi kuchaguliwa bila wao, jambo ambalo hata viongozi hao hawalitaki na wamewataka kuacha kufanya hivyo.
Alisema alikutana na viongozi 70 wa dini mjini Dodoma walililalamikia suala hilo na kuahidi kuimarisha umoja.
"Nimewaambia wakiona mtu kachachamaa sana sababu hajazoea kushindwa, wamwite kanisani au msikitini wamwombee," alisema na kuongeza kwamba wanaounga mkono masuala ya udini ni wale wanaotaka madaraka.
Aliwashauri wabunge kuendeleza misingi waliyoiacha wanasiasa waliowatangulia kwani wangekuwa wachoyo na wadini nchi isingefika hapo ilipo.
Aliendelea kuwashauri wapinzania kwamba sifa ya upinzani ni hoja, wakiamua kutoka katika vipindi vya Bunge, wananchi watawazoea watafika wakati hawatoki wataulizwa mbona hawatoki.
Magufuli na barabara za lami
Ilipofika zamu yake, Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli alitoa hutoba ya kuvutia akitaja barabara zinazojengwa, maeneo zilipo na urefu wake bila kusoma mahali popote, na kutoa ahadi kuwa kzatika miaka minne ijayo barabara zote zitapitika na hakutakuwa na barabara ya changarawe.
Alisema serikali imefanya vizuri katika miradi mikubwa ya barabara, kuna miradi iliyo katika utekelezaji, upembuzi yakinifu na mingine inasubiri kupatikana kwa mkandarasi ili ujenzi uanze.
Bw. Magufuli alisema mtu anaweza kwenda mahali kokote ikiwemo hata kutoka Mtwara kwenda Morogoro kwa kutumia bajaji.
Aliwataka wananchi kuheshimu sheria namba 13 ya mwaka 2007 inayohusu hifadhi ya barabara, waliondani ya hifadhi hawatalipwa fidia wakibolewa kwa mujibu wa sheria hiyo.
"Katika masuala ya barabara hakuna siasa, hakuna CCM, hakuna CUF, hakuna CHADEMA wala chama gani, waliojenga nje ya barabara lazima walipwe kwa mujibu wa sheria, hatakiwi mtu yoyote kuvamia eneo la hifadhi ya barabara," alisema.
Tibaijuna na kero za ardhi
Akichangia kwa upande wa Wizara ya Ardhi, Prof Anna Tibaijuka alisema kuna vipaumbele walivyojiwekea ikiwemo kujadiliana serikali kuweka sera ya kuhakikisha wawekezaji wanazingatia haki za wananchi na ardhi inalindwa.Aliwaomba wabunge na wadiwani kushiriki vikao husika vinavyogawa ardhi kwa wawekezaji kwani wanatambua sheria za ardhi zina upungufu.
Prof. Tibaijuka alisema kero katika ardhi ni nyingi lakini habari njema ni kwamba walishaanza kuzifanyia kazi wamejipanga kwa umakini wanaomba msaada kutoka kwa wananchi na wabunge ili kufanikisha azma yao.
"Watendaji ardhi kama mlikuwa mapumziko yamekwisha, kupanga mji kunataka kujitoa na kufuata sheria kwa maslahi ya Watanzania wote,"alisema.
Nundu kupanua bandari Tanga, Dar
Kwa upande wake Waziri wa Uchukuzi, Bw. Omar Nundu akizungumzia wizara yake alisema sh. bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kuipanua bandari ya Tanga kufanya kazi ili kusaidia kukuza uchumi.
Alisema bandari ya Dar es Salaam ikiongezwa uchumi pia utaongezeka, wamepanga kuongeza gati namba 13 na 14, bandari itaongezwa na kuchukua sehemu ya Vijibweni na Kisarawe.
Kwa upande wa reli wanatarajia kuboresha usafiri wa abiria na mizigo ni mpango wa mwaka, kwa miaka miwili wanategemea kuwa na treni inayokwenda Mwanza kila siku.Kwa upande wa viwanja vya ndege ujenzi wa terminal three unatarajiwa kuanza mwaka 2011-2012 na uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya utakamilika Agosti mwaka huu.
Nahodha na udogo wa Zanzibar
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha yeye alionesha kukerwa na kauli kwamba Zanzibar ni ndogo, akifafanua kuwa kama ongozi anaangalia ukubwa wa jimbo au wingi wa wapiga kura, John Mnyika, Mbunge wa Ubungo angekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzania Bungeni kwa kuwa na wapiga kura wengi.
Hoja hiyo imetokana na wabunge wa upinzania hasa CHADEMA kuzungumzia bungeni kwamba Zanzibar ina watu wachache, hoja ambayo iliwakera wachangiaji mbalimbali, waliokuwa wakiitolewa maelezo na kuonya kila walipokuwa wanachangia.
"Leo Mnyika anaongoza watu zaidi ya 450,000 kama ni kuangalia ukubwa basi angekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzania Bungeni," alisema.Alisema siku moja wabunge wa bara wataangalia wenzao wa Zanzibar si kwa udogo wa majimbo bali kwa hoja na mchango wao bungeni.
Waziri Nahodha akizungumzia kuboresha maslahi ya polisi alisema hatua zinachukuliwa kuboresha utendaji kazi wao, kuwapa vifaa na makazi mazuri ili kukidhi ari na motisha.
Pia alisema watawapa mafunzo ya upelelezi ndani na nje ya nchi ili kuzisaidia mahakama kuendesha kesi haraka kwani waliojaa magerezaji asilimia 50 ni mahabusu.
Alisema wanadhamiria kujenga vituo vya polisi kila kata na alikiri kwamba Tanzania ina amani na usalama japo baadhi ya maeneo kuna vitendo na matukio ya uhalifu yanayoweza kuhatarisha usalama.
Waziri alimalizia kwa kusema kwamba watashirikiana na Watanzania kuimarisha amani ya nchi, alisema hata mataifa tajiri yana changamoto za usalama kama zilizopo nchini.
JAMANI HAWA MAWAZIRI NI WAONGO SANA MBONA HAWATWAMBII WHY UCHUMI WETU UMESHUKA SANA HADI KUGARAGAZWA NA BURUNDI,RWANDA NA KENYA!!!!!!!HUKU WAKIJISIFIA KWENYE MAJUKWAA ETI TUNA AMANI TANGU UHURU NA WANAKIKASHFU HIZO NCHI KWA VITA!!!!!
ReplyDeleteWATANZANIA TULISHAWAJUA VIONGOZI WA TZ KUWA WANATUMIA UJINGA WA WATANZANIA KUWARUBUNI KWA KISINGIZIO CHA AMANI ILI HALI WAKIPORA RASILIMALI ZETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!SASA TUNAWAMULIKA NA MACHO MAWILI BORA AMANI ITOWEKE KWA MUDA ILI BAADAE TUHESHIMIANE NI SI KUBAKI NA AMANI NA UMASKINI TELEEEEEEEEEEEEEEE!
Mchangiaji hapo juu unachemsha, na bado una mtazamo wa kitoto kuhusiana na amani ya nchi.
ReplyDeleteWATUAMBIE NI KWA NINI WATANZANIA WENGI WANAKOSA HATA KUPATA MLO WA SIKU ILHALI NI WAAJIRIWA NA WAFANYAKAZI. WATUAMBIE NI KWA VIPI MIAKA HAMSINI BAADA YA UHURU BADO TUNAISHI GIZANI ILHALI TUPO MIJINI. WATUAMBIE NI KWA NINI UFAULU MASHULENI UMESHUKA NA ELIMU IKO KATIKA VIWANGO VYA CHINI KULIKO WAKATI WOWOTE. WASEME NI KWA NINI HAKUNA MADAWA YA KUTOSHA HOSPITALINI NA KWA NINI VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO HAVIPUNGUI BALI VINAONGEZEKA. WATUAMBIE PIA, NI KWA NINI WAO NA WATOTO WAO WANAZIDI KUTAJIRIKA, WAKATI SISI NA WATOTO WETU TUNAZIDI KUWA MASIKINI. NA WAINUKE WASEME JUU YA HAYA PIA TUWASIKIE.....
ReplyDeletemkome si simliwashabikia akina makamaba na kucheza ngoma zote na meno nnje hamkuelewa mnapumbazwa akili,haya miaka mitano mtuvumilie tutarudi kuwa danganyatena mkisahau, sahizi mtakula mabomu ya mchozi sikumoja moja ya moto maisha bora kwa kila mtanzania ,tanzania bila utajiri ina wezekana.
ReplyDeleteAcha kuchemsha. Wamekuwa madarakani mwaka haujaisha wewe unaongelea miaka 50.
ReplyDeleteSiku zote mawaziri wa Kikwete ni wale wanaofikiria hapa tulipo tu. hawataki kwenda mbele na kufikiri kuwa kesho itakuwaje? Ni jambo la ajabu mtu kuimba amani utafikiri wao ndio walioieleta wakati polisi wao wanaua watu. Huyu anayesema udini ndio kabisa amefilisika mzee huyu Wasira. masikini Wasira hata baba wa Taifa alisema kiongozi anayeanza kuyaja udini ujue huyo kafilisika. Najua tu wanampiga vijembe Dr. Slaa, kumbukeni mwaka 2005 kikwete alikuwa chaguo la mungu lakini wasira hakumsema wala kulalamika leo hii kwa kuwa Slaa anataka urais na ni mkristo basi imekuwa nongwa. Mbona huko CCM yenu Rais, makamu wake na Rais wa zanziba wote ni waislamu hili nalo Wasira anasema nini? juzi hapa Rais ameteua wabunge watatu wote ni waislamu hili hujaliona wewe kipofu wa uwaziri wasira? usiwachefue watanzania na hoja zako za kijinga huu si wakati wake, mambo hayo hayafai kuzungumzwa bungeni maana wengine mnawatia vidonda kama sio majeraha.
ReplyDeleteBarabara ndio imekuwa wimbo eti kwa miaka 5 ijayo hakutakuwa na barabara ya changarawe! Hizi ni ndoto za mchana kwa nchi ya ufisadi kama Tanzania. Labda hiyo inawezekana kama kwa wanaokariri kemia kama huyu Magufuli. alianza na kutamba kuwa watu watatoka Bukoba hadi mtwara kwa teksi ikashindikana leo anakuja na kibajaji. Usanii huu. Pinda elekeza nguvu kwenye kilimo ili watanzania waweze kukuchangia vizuri pensheni yako. Huu ujinga wa 400b kwa mwezi acheni mnaeza kupata nyingizaidi kama sio ufisadi mnaoufanya.
MUNGU ATAWABARIKI KWA MATENDO YENU MEMA NA ATAWAAANI KA UFISADI NA WIZI WENU
Bila kugeuza mnazi mmoja tahrir square mmekwisha! Wamejipanga bungeni ili 2015 wafunge Kazi!
ReplyDelete