15 February 2011

Manjia ajiweka pembeni Yanga

Na Elizabeth Mayemba

MDHAMINI Mkuu wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amejiondoa katika klabu hiyo, baada ya kuchoshwa na lawama ambazo amekuwa akitupiwa kila siku na
baadhi ya wanachama wa klabu hiyo,ikiwa na uongozi kushindwa kufanya ukaguzi wa mahesabu na kuweka wazi kwa wanachama.

Pia, mdhamini huyo amesema kwamba, sababu nyingine iliyomwondoa Yanga ni kutokana na klabu hiyo kutokuwa na nguzo ya wanachama, ikiwa uongozi kuwa, wagumu wa kufanya mahesabu ya klabu hiyo.

Habari zilizopatikana Dar es Salaam jana kutoka katika chanzo chetu cha habari, zinadai kwamba, Manji ameondoka Yanga si kwa jazba, bali alikaa na kufikiria hivyo, atabaki kuwa mwanachama wa Yanga na atashiriki shughuli zote za klabu kama kawaida akiwa kama wanachama wengine.

"Manji anasema alikuwa anataka mahesabu yafanyike haraka kwani ana uhakika kabisa kwa upande wake, atakuwa ametapeliwa, na Yanga pia itakuwa imetapeliwa,na ndio maana alikuwa anakazania mahesabu yafanyike ili kila kitu kiwe wazi," kilidai chanzo hicho.

Imedaiwa kuwa, pamoja na mdhamini huyo kuendelea kushikilia msimamo wake wa kutaka ukaguzi huo ufanyike, bado viongozi wanaendelea kumwongopea,jambo lililojitokeza hivi karibuni ni kwamba, uongozi uliomba mdhamimini huyo asaidie kutoa nauli ya wachezaji wakati walipokwenda Songea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara.

Hata hivyo, inadaiwa sababu kubwa ambayo uongozi ulitoa kwa mdhamini huyo, ni kwamba, basi lao lilikuwa limezuiliwa,na hivyo Manji akatoa sh.70,000 kwa kila mchezaji kwenda na kurudi.

"Matokeo yake, nauli walichukua na basi wakaondoka nalo,sababu kama hizi zimemkera sana Manji," kilidai chanzo hicho.

Pia, mdhamini huyo imedaiwa kuwa, amesikitishwa na watu wanaomsema vibaya kutokana na yeye kuukopesha uongozi fedha, na kuhoji kwamba, kwanini wasiulizwe wale waliokuwa wanakopa, waseme walikuwa wanafanyia nini.

Chanzo hicho kinasema Manji alikuwa akiwakopesha Yanga kwa nia nzuri tu, kama alivyokuwa anaombwa,na si kama yeye alikuwa analazimisha viongozi wamkope.

Pia, mdhamini huyo ameishukuru klabu hiyo kwa heshima kubwa waliyompa kwa kipindi cha miaka mitano akiwa kama mfadhili, na kwamba, maamuzi yake ni kuinusuru klabu hiyo na migogoro kwani kuna watu wanataka kugombana naye akiwa ndani ya Yanga, na ili kuepusha hali hiyo, ameona ni vyema akaondoka moja kwa moja.

7 comments:

  1. si uende tu unambwela mbwela nini bana...arghhhh!

    ReplyDelete
  2. Bora akae pembeni tuone hao wanachama wenye mdomo wanaoweza kwenda habari maelezo na kuanza kuropoka wakati hata shs hawatoi kuichangia timu michango yenyewe 12000 kwa mwaka hawatoi..washenzi wamekaa majungu tu hata hawjui timu inaendeshwaje? wachezaji wanalipwaje?..sasa tuone wapewe timu sasa...bora timu apewe mtu aindeshe kuondokana na wanachama wababaishaji..washenzi wamesabaisha timu ifanye vibaya kwa sasa..Kaa pembeni Manji nakuunga mkono ingawa najua unaumia

    ReplyDelete
  3. Mipira nayo kama siasa! nchi hii sijui inaelekea wapi!

    ReplyDelete
  4. TENDA WEMA WENDEZAKO USINGOJE SHUKURANI!1, HIZI KLABU ZA SIMBA NA YANGA CK ZOTE HAZINA SHUKRANI WAO WANACHOTAKA NI USHINDI TUU,LAKINI UKIANZA KUSUASUA HUNA MAANA KWAO, PIA NI WATU WALIOZOEA KUBEMBWA NA KULA PESA ZA DEZO UKIWABANA HAWAKUPENDI,CHA KUFANYA SASA MANJI ANZISHA TIMU YAKO KAMA ALIVYOFANYA DEWJI AKAIUZA KWA MDADA SASA NAWE ANZISHA KAMA VILE AZAM, TANZANIA LYON NK, HAKUNA MTU WA KUKUINGILIA AU KUWAUDHI WATU FIKIRIA HILO UWE NA TIMU PINZANI SAAAFI SANA

    ReplyDelete
  5. manji siyo lazima yanga,tunajua lengo lako mbeleni,na unajua kwamba wajinga ndo waliwao, lakini kumbuka siku moja wataamka kutoka usingizini..sasa yanga wanaanza kuamka baadaya usingizi mnono.. amkeni kumekucha. manji anaondoka kabla ya malengo yake??...mmm'' manji huyu ninaye mfahamu?.. labda mwingine.. YANGA BILA MANJI INAWEZEKANA

    ReplyDelete
  6. TATIZO KUBWA NI TOFAUTI KUBWA YA MALENGO KATI YA YANGA NA MANJI. TATIZO JINGINE NI KUTOKUWA/KUTOHESHIMU MIPAKA YA KIUTENDAJI KATI YA MDHAMINI, MFADHILI NA UONGOZI. MATOKEO YAKE MIGOGORO YA AINA HII HAIWEZI KUEPUKWA.

    ReplyDelete
  7. Manji tatizo lako ulifikiri migogoro ya Yanga itamalizwa kwa kumwaga fedha nyinngi. Umemwaga fedha, umekarabati jengo, umejenga kiwanja - lakini tatizo lipo pale pale.

    Kumbe shida ya Yanga ni nini?- tatizo ni kuifanya wanachama waihodhi club na si wadhamini waendeshe club. Wanachama wajue kwamba yanga ni yao na bila wao hakuna club ya yanga. Manji umekuwa unatoa fedha nyingine ambazo ni kichekesho, mfano wakati wa michezo kati ya yanga na simba utasikia "Manji katoa shs milioni 50 kwa ajili ya kushinda simba, 10 kati ya hizo ni za wazee"- very childish!! mambo kama hayo ndo yanachangia migogoro na kukosa sense of ownership!!

    Sasa umestuka too late approach yako was poor

    ReplyDelete