LONDON, Uingereza
Manchester United, itapambana dhidi ya Arsenal katika robo fainali ya michuano ya Kombe la FA, iwapo Gunners itaifunga Leyton Orient katika mechi
nyingine ya marudiano, baada ya juzi kutoka sare ya bao 1-1.
Kama Gunners itavuka katika mzunguko wa tano kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Leyton Orient, watasafiri kwenda Old Trafford kukutana na timu ya kocha Sir Alex Ferguson.
Manchester City ambayo jana iliifunga mabao 5-1, Notts County itapambana na Everton-Reading, wakati Stoke watakuwa nyumbani kuchuana na West Ham au Burnley.
Bolton itasafiri kwenda Birmingham kupambana na wenyeji wako. Mechi za robo fainalia zitafanyika Machi 12 na 13, mwaka huu.
Vinara wa Ligi Kuu England, Manchester United walisonga mbele kwa ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya timu ndogo ya Crawley katika mzunguko wa tano.
Mara ya mwisho United, ilikutana na Arsenal katika Kombe la FA mwaka 2008 ambapo Mashetani Wekundu, waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 wakati timu ya Arsene Wenger iliishinda United mwaka 2005 katika fainali kwa penalti.
Mabingwa watetezi, Chelsea wametolewa katika mashindano hayo dhidi ya Everton.
No comments:
Post a Comment