*Anayetajwa kuimiliki ajitokeza Dar
*Akiri kumpa Rostam nguvu ya kisheria
Na Mwandishi Wetu
MFANYABIASHARA wa Oman anayetajwa kuwa ndiye mmiliki wa Kampuni ya Dowans Holdings SA na Dowans Tanzania Limited, Brigedia Jenerali
(Mstaafu), Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi amejitokeza na kukiri kumiliki kampuni hiyo huku akiweka wazi kuwa iko tayari kwa na mazungumzo na serikali.
Al Adawi aliyezungumza na baadhi ya wahariri wa magazeti jijini Dar es Salaam kwa sharti la kutopigwa picha wala kurekodiwa na kamera za televisheni, alisema ameamua kujitokeza kutokana kuondoa kiwingu kilichokuwa kinaizunguka kampuni hiyo hasa kuhusu umiliki wake na akakiri kwamba alimpa Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz nguvu ya kisheria kuisimamia nchini.
"Mimi ndio mwenye hisa nyingi katika kampuni ya Dowans Holdings SA na kampuni yake tanzu ya Dowans Tanzania Limited...Nimekuja nchini kuweka sawa habari za upotoshaji kuhusu Dowans na kufahamu kama uwezekano wa kupata suluhisho la hali iliyopo," alisema.
Mfanyabiashara huyo aliambatana Bw. John Miles, aliyetambulishwa kama mwanasheria maarufu wa kimataifa ambaye amekuwa akiiwakilisha kampuni hiyo tangu ilipoingia katika mgogoro na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Bw. Stanly Munai aliyetajwa kama Mkurugenzi wa Fedha wa Dowans Tanzania Limited, ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa kampuni hiyo waliotajwa na Waziri William Ngeleja Januari mwaka huu.
Mbali na Brigedia Jenerali Al Adawi, wengine waliotajwa ni Andrew James Tice kutoka Canada, Gopalakrishnam Balachandran wa India, Hon Sung Woo wa Malaysia, Guy Arthur Picard kutoka nchini Canada pamoja na Stanley Munai wa nchini Kenya.
Brigedia Jenerali Al Adawi alisema tangu kampuni hiyo ilipoanzishwa mwaka 2005 alikuwa amenuia kuwekeza katika mkongo wa mawasiliano katika nchi za Afrika Mashariki, lakini kwa kuwa yeye anaishi Muscat, Oman, alihitaji mtu wa kumwakilisha kufanikisha mpango wake, ndipo alipomchagua rafiki wake wa siku nyingi Bw. Rostam Aziz.
"Ili Bw. Aziz awe na mamlaka ya kutosha kusimamia kampuni yangu, mwaka huo wa 2005 nilimpa nguvu ya kisheria," alisema na kufafanua kuwa mpango huo ulibadilika baada ya kutokea mpango mpya wa mitambo ya kuzalisha umeme mwaka uliofuata.
Alisema Baada ya kampuni ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme, Septemba 2006, Bw. Aziz aliwasiliana naye akimwelezea tatizo la umeme akimshawishi awekeze kwenye umeme, akiamini kuwa mwekezaji anayetakiwa ni mwenye uwezo na anayeweza kufanya shughuli hiyo haraka.
"Mtakumbuka kuwa TANESCO iliomba kupitia kwenye vyombo vya habari mwekezaji mwenye uwezo wa kuzalisha kuanzia megawati 1 kuwasiliana nayo kuzalisha umeme wa dharura. Gridi ya taifa ilikuwa inaishiwa umeme kabisa.
"Hatimaye, Dowans ilifikia makubaliano na Richmond, kuwa kama TANESCO ingekubali kampuni yake ingechukua nafasi ya Richmond kuchukua mkataba wa kuzalisha umeme. Tuliamini kuwa Dowans ingepokewa vizuri na TANESCO, serikali na umma kama shujaa, kinachotushangaza haikuwa hivyo.
Alisema Dowans ililipa dola za Marekani milioni 109 (kwa ajili ya mitambo, vifaa vyake na wahandisi na baadaye kuongeza mtaji wa dola milioni 20.
Al Adawi alisema kuwa watu wasiokuwa taarifa sahihi wamekuwa wakiishutumu kampuni yake wakiita ya mfukoni, lakini yeye anawapa changamoto waoneshe kampuni nyingine ya mfukoni yenye mitambo ya dola za Marekani milioni 109.
Mfanyabiashara huyo alionekana kama anajibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikimtaja Bw. Aziz kuwa mtu mwenye mamlaka na Dowans, alisema wakati anaweka sawa kampuni yake nchini, alimwomba mbunge huyo ambaye ni rafiki yake amsaidie, pia aliwatumia wafanyakazi wa kampuni ya mbunge huyo, Caspian limited, ambao baadaye walikabidhi majukumu kwa wengine walioajiriwa na Dowans limited.
Akijibu maswali ya wahariri, mfanyabiashara huyo alisema kwa sasa ameitwa nchini na serikali kuzungumzia uwezekano wa kutumia mitambo yake kuzalisha umeme kuinusuru nchi na mgawo unaoendelea sasa.
Alipobanwa zaidi ni nani hasa serikali aliyemuita kuzungumza naye, alisema kwa sasa atazungumza na uongozi wa TANESCO kwa kuwa ndiyo inayohitaji umeme, huku akisisitiza kuwa kampuni yake imekuwa ikiuza umeme kwa gharama nafuu ya senti 4.99 kwa uniti moja, jambo ambalo anaweza kufanya hata sasa ikiwa wataelewana.
Kuhusu uwezekano wa kupunguza fidia iliyotolewa kwenye hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICC), alisema ikiwa serikali itazungumza hilo atakuwa tayari kusaidia kwa nia njema.
Alipoulizwa kwa nini ameamua kujitokeza yeye mwenyewe badala ya Bw. Aziz ambaye alishapewa nguvu ya kisheria, Brigedia Jenereli Al Adawi alisema ni kwa sababu kumekuwa na maneno juu ya mmiliki wa kampuni hiyo, hivyo amejitokeza ili kuonekana.
Alipoulizwa kama anataka kuonekana kwa nini hakutaka kupigwa picha za magazeti wala televisheni, alisema yeye ni mfanyabiashara asiyetaka kufahamika kwa kuwa si vizuri kufanya hivyo kwa mtu kama yeye anayemiliki mali nyingi, akitolea mfano India anakomiliki mitambo ya mabilioni lakini picha yake haijawahi kutokea kwenye magazeti.
Akizungumzia tuzo ya ICC, Al Adawi alisema baada ya hukumu hiyo, Dowans iliwaandikia TANESCO na serikali ili kufanya mazungumzo kutafuta maelewano kwa njia mbalimbali lakini haijajibiwa.
JAMANI WATANZANIA Wenzangu, ninashindwa kuelewa ni kwa nini serikali ya CCM haikutaka kununua mitambo mipya tangu mjadala wa Richmond ulipoisha takriban miaka 6 iliyopita. Wakati mgao wa umeme ulipoanza ndipo tunaambiwa kuwa Dowans imeshinda kesi. Wakati hali ya umeme iko shwari TANESCO NA SERIKALI hawakutaka kuagiza mitambo yetu. JE NI KWA NINI SERIKALI INATUMIA MAKALI YA MGAO WA UMEME KUTAKA KUHALALISHA UFISADI WA DOWANS? Ni nani amemwita huyu mwarabu jama siyo Mafisa wakati wanajua kuna pingamizi mahakama kuu
ReplyDeleteIKIWA TUMESHAPATA HASARA CHUNGU MZIMA TOKEA DESEMBA MPK SASA,TANESCO IMEKOSA MALIPO TOKA KWA WATEJA KWA UZEMBE NA PIA TUMESHATESEKA KUKAA KIZA KWA MIEZI HII YOTE NA PIA TUMESHAPATA HASARA ZISIZO LIPWA ZA KUTUUNGUZIA VIFAA VYA MAJUMBANI, NA KUHARIBIKA BIDHAA MADUKANI NA MAJUMBANI NI BORA TUENDELEE KUSUBIRI KUDRA YA MUNGU KULETA MVUA, WAKATI ZIMESHAANZA NI BORA TUZIDI KUTESEKA KULIKO KUTOA MWANYA KWA MAFISADI,HUYO RICHMOND KAWEZA KUAGIZA MITAMBO NA KIUILETA NCHINI KWA NDANI YA MIEZI3,IWEJE KWA SERIKALI ETI KUAGIZIA HIYO MITAMBO ICHUKUWE MIEZI 12?!! KULIKONI? HAPO KUNA NJAMA NA MWAKA 2008/9 WALISEMA NI BORA KUAGIZA MITAMBO YETU KULIKO KUNUNUWA HIYO YA DOWANS SASA NI MIAKA MITATU HUU NI WIZI MTUPU ,
ReplyDeleteMungu awalaani Wale wote wanaochezea akili zetu. Wanatufanya tutende dhambi kuwa na chuki kila tunaposoma magazeti na kusoma udanganyifu kama huu wa kifisadi kama wa DOWANS.
ReplyDeleteYaani huu udanganyifu wa kipuuzi unawafanya wa Tanzania wote kama watu wa porini (Bushmen) yaani hakuna aliyeenda shule ila hao Dowans na washirika wao. Alikuwa wapi huyu Mwarabu, ni ujanja na mtego, limelipuka, Rostam kamuagiza aje nchini kutudanganya. Hivi hawa Waarabu na wote waliomo humu wa nje wanafikiri Tanzania iko kwenye utumwa wa kupigwa, kuchukuliwa utumwani kama zamani au vipi? Huyu mwarabu kwa jina la Yesu nikikutana naye naua, nitamuua haki ya Mungu, simpendi hata kumuona, wala Rostam pia simpendi, yaani wote siwapendi, Raisi yuko wapi na idara za uhamiaji kumuingiza nchini huyu zimwi la mtu, mtoeni hadharani mimi nitamchoma mkuki naapa kwa uchungu wa kukaa gizani na watoto wangu hawafanyi homework, yeye ana jileta hapa kufanya nini. Kwao wanapiga mawe na kuua na sisi tumfanyeje< Hivi nani kamruhusu kuja hapa kama siyo dharau ya hali ya juu ili kutuongoezea hasira. Ndiyo maana watu wanaua, hawana hatia kuna maudhi ndani yake hadi mtu unafikiria kuua. NIna hasira ya kufa mtu na hawa watu. Mungu na ustaarabu naweka pembeni, sitaki umungu wala usomi wala ustaarabu, nakaribisha ubaya kwa hawa watu, wanastahili kuuawa.
ReplyDeleteNINAKUMBUKA NGAREJA ALIWATAJA WAMILIKI WA DOWANS NA KIKWETE AKASEMA HAWAJUI. KIPINDI HIKI CHOTE AZIZ HAJATWAMBIA CHOCHOTE. MMILIKI ALITEJITOKEZA YUKO TAYARI KUFANYA MAJADILIANO YA KUPUNGUZA KIASI CHA FIDIA SASA MBONA TUNASHUPALIA KULIPA HARAKA. HIVI ONGEZEKO LA BEI YA UMEME SIO KWAMBA TUMEANZA KULIPA HIYO FIDIA?
ReplyDeletesuala la msingi siyo jazba za kisiasa kama mmiliki amejitokeza Tanesco wakae naye na kuweka mambo sawa. Cha muhimu ni taifa kupata umeme na huenda hata hiyo fidia anayodai akaisamehe. Tusiingize siasa kila mahali
ReplyDeleteIna maana Tanzania ni maskini kiasi cha kuonewa huruma na huyu jamaa?
ReplyDeleteKweli Tanzania haiwezi kununua mitambo yake yenyewe au kukoka kunakoeleweka? Hii ni aibu, watanzania mil 40 tunakuwa watumwa wa watu mtu mmoja. Utumwa ambao babu zetu waliukataa, tunaukubali kirahisi hivi?
Tuliuzwa kwa waarabu, tukatawaliwa na wazungu, sasa tunarudi kutawaliwa na waarabu? Halafu baadaye na wachina au na wazungu tena?
ngoja tuone hoja ya sultan wa oman,wakae tumsikie,labda anafuta deni,au kaitwa kisanii ili deni lilipwe wakagawane mbelekwambele,si unajua tena mjini shule?mwarabu ns mwarabu mwenzake,rostam kaona maji shingoni kaona bora aje patner wake labda atakata mzizi wa fitna,hiyo italipwa juu kwa juu mjadala unakatika tuendelee na maombolezo ya mabomu,akili za watu ziko na mabomu,dowans ishaisha tena.acha wakagawane vizuri dowans yao!!!
ReplyDeleteMchangiaji mmoja amesema tuache siasa za kukurupuka.
ReplyDelete1. Amekuja, amekirikiri yeye ndiye mmiliki ( swali moja limejibika)
2.Pili, position ya Rostam Aziz imekuwa clear ( swala la pili la umiliki limejibika)
3. Anasema yupo tayari kwa mazungumzo na serikali ( tumweleze yoooote tuliyonayo na kwa nini hatutaki kulipa) - swala la kulipa au la litazungumzia na kujibika
5. swala la kuwasha mitambo kwa mkataba mpya kutuepusha na mgao wa umeme linaweza kuzungumziwa
Mimi nafikiti this is a right route to this issue. Yupo kwetu lazima tumbane kiswasawa.
3. Yupo tayari kwa mazungumzo ni serikali
naungana na mchangiaji aliye ainisha mambo 5 hapo juu. hayo ndiyo mambo ya msingi.tuache majungu na fitina zinazotokana na ubinasfi wetu. leo tunaanza kujua ukweli. kama mtu anachuki binafsi na waarabu hasituletee katika mambo ya msingi yanayohusu maslahi ya nchi.binadamu wote ni sawa.serikali/tanesco ikae na jamaa waone jinsi gani wataweza kumaliza ili suala kwa busara zaidi. kulipa hizo pesa ni nyingi sana , na kusamehewa deni na mwarabu siyo dhambi,cha msingi ni umeme upatikane ili maisha yarejee kama kawaida. tuache chuki binasfi.
ReplyDeleteMAFISADI SASA YAMEITANA BAADA YA HOJA YA JANUARY MAKAMBA KUKODISHA MITAMBO,NYIE ACHENI KUTUCHEZEA AKILI WATANZANIA KUNA SIKU JESHI LITACHOKA NA KUPINDUA NCHI!!!!!!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHuu ni ushenzi, upumbavu na ujinga. Waarabu kwao hakukaliki kwahiyo wanakimbilia shamba la bibi Tanzania na sisi tunakubaliana huu ni utumwa wa haliyajuu na isitoshe kwa vile kesi watanzania watashinda basi dangaja toto hiyo yaja huu ni usanii ambao hautokei mahali pengine ila ni Tanzania. Rostam watanzania hatukutaki rudi kwenu mwehu wewe.
ReplyDeleteili kuwa tuende sawa wale wote waliongopa kwa wawekwe ndani harafu ndiyo tuwaagalie nini kifanyike.
ReplyDeletewametuongopea vya kutosha na bado wanaletana tu kuja kutuongopea zaidi.
sisi siyo wapumbafu wa kupindukia.
Tumechoka elimu ya ujinga na nidhamu ya uhoga,
kuibiwa,tuibiwe na tabu tupewe hivi sawa dunia hii wameumbiwa wao basi hata bongo iwe yao! no hata kidogo, tumechoka
msasa lazima upite ili tuweke sawa mambo
C.C.M wanajua wanapotupeleka,heri hizo prsa zinge saidia walemavu ktk elimu,kuliko kumpatia tajiri.
ReplyDeleteUkisikia utapeli wa kimataifa ndio huu. Sasa watanzania tuamke na tuwe makini katika hili. Hapa ndio patamu na pa kujua mbivu na mbichi katika sakata hili. Watanzania wenzangu nina maswali kadhaa ambayo tuyatafakari:-
ReplyDelete1. Hivi umewahi kusikia wapi mwekezaji safi katika moyo wake (Adilifu) na mwenye nia njema katika biashara zake kukataa kuonana na viongozi wa serikali, kukataa kupigwa picha, kukataa kurekodiwa katika vyombo vya habari? Kwangu mie huyu ni mwizi na ni tapeli mzoefu, mbabaishaji na ni mtu wa kutunga umiliki wake wa kampuni.
2. Taarifa ya kamati ya bunge chini ya Uenyekiti wa Mh. Mwakyembe ilibainisha kuwa kampuni hii haijawahi kuwepo katika rekodi zozote; na hasa Costa Rica, Tanzania wala Canada. Sasa iweje leo ajitokeze kuja kuelezea umiliki na uwepo wa kampuni ya Dowans duniani na kwamba yeye ndiye mwenye hisa nyingi??
3. Katika kikao na waandishi wa habari (wakati anafafanua juu ya mafisadi nyangumi na papa), Mh. Rostam Aziz alikana kuhusika kwake na kampuni zote mbili za umeme na kwamba hahusiki hata kidogo katika umiliki huo achilia mbali kujitokeza hivi karibuni. Je uongozi wake kama mbunge hauna shaka? Je uaminifu wake katika nchi yetu uko wapi? Je anafaa kuendelea kuitwa kiongozi wa watu kama aliwaficha/ aliwakana wawekezaji hapo awali? Mbunge aliyeapa kuitetea katiba?
4. Tapeli Adawi aliwahi kuhojiwa na kamati ya Mwakyembe juu ya umiliki wake wa Dowans akakana. Huku akijuwa fika kuwa kamati ile ni ya wabunge akadiriki kuwadanganya na kukana kumiliki kampuni. Leo anajitokeza na kutaka kutuaminisha kuwa ni mmiliki halali wa kampuni ya Dowans. Hivi huu si ni ujinga na utapeli wa hali ya juu?
5. Kwa kukataa kuonana na viongozi wa serikali, hatuoni kuwa kuna walakini hapa!! Kwanini mwekezaji halali wa kampuni aogope kuongea na viongozi? Ama atuambie ana watu wanaoshirikiana nao pale TANESCO au ni tapeli tu!! Kukataa kuonana na viongozi wa serikali si ni udhalilishaji na taifa? Je ni halali mwekezaji kuweka masharti ya kutokuonana na viongozi ambao hiyo TANESCO inakuwepo kutokana nao? Yaani hata Waziri wa Nishati ambaye alikuwa anatetea kulipa deni naye ni adui wake?? Hapana hapa kuna jambo. Hivi Usalama wa taifa mko wapi na kwanini hamumshughulikii huyu jamaa ambaye anadhalilisha viongozi wetu?? Zoka upo au unajua kuwadhibiti wapinzani tu?
ReplyDelete6. Katika hotuba yake siku ya maadhimisho ya CCM, Mh. Rais Kikwete alisema hawafahamu wamiliki wa Dowans na kwamba haungi mkono kuwalipa Dowans. Imani yangu inaniambia kuwa Kikwete ni "baba" yetu (Nyumba ya Tanzania) na akisema deni, lisilipwe maana yake ni kuwa halitalipwa. Nilifikiri Adawi angesema anahitaji busara ya Rais ili alipwe badala yake anasema hataki kuonana nao. Huu ni ubabe wa aina yake ndugu zangu na haupaswi kuachiwa kiuzembe namna hiyo. Kikwete unavumilia tu, Diplomacy?? No, No, No! Kila kitu kina ukomo wake kaka; Acha uzoba!!
7. Kuna baadhi ya wachangiaji wanashauri mwekezaji akae na TANESCO ili waone jinsi ya kupunguza au kusamehe deni. Hili ni jambo jema kabisa; lakini kwanini Taifa linyanyaswe na kudharauliwa hivyo? Mtu hataki kuonana na viongozi wetu (Hata kama walipatikana kwa kuchakachua), anawadhalilisha na kuwabeza. Hii sio haki na haihitaji kunyamaziwa hata kidogo. National Sovereignity has its space in here, we need to be a bit more serious than this, otherwise we are welcoming Neo Neo Neo Colonialism in our country!!. Jambo la busara hapa ni kuitaifisha mitambo, kumtia adabu huyu mdharau viongozi wetu na tapeli wa kimataifa anayejitokeza siku za mwisho baada ya jambo hili kushika kasi.
8. Sakata hili limedumu kwa zaidi ya miaka sita. Siku zote limewasumbua watanzania; viongozi na wanataaluma ndani na nje ya nchi. Hivi haiwezekani kuwa Rostam na wengine wamehusika kumshawishi huyu Adawi kujitokeza kuwa mmiliki halali ili malipo haya yaende kwake na wagawane na wamiliki uchwara?? Tukumbuke kuwa wote walikana kuhusika na kampuni hii; na kumbukumbu tunazo kupitia vyombo vya habari. Ikumbukwe pia matapeli huwa ni wajanja na wana mbinu mbalimbali za kutafuta fedha. Hivyo, sishangai kujitokeza kwa Adawi kuja kudai malipo hayo na ikizingatiwa udhaifu wa kisheria tuliouonyesha hadi sasa. Inawezekana kabisa kuwa hata viongozi wetu wamehusika kumwita huyu FISADI wa kimataifa maana watapata share yao. Ni wakati wa viongozi wetu kuonyesha misuli yao kiuongozi na kisheria. Kikwete usikubali kudhalilishwa. Huu ni mchezo mchafu na haufai hata kidogo; unless nawe unahusika. Mkamateni na ashughulikiwe. "Hakuna Mjomba atakayetoka nje kuja kuwasaidia watanzania, kama yupo naomba mniambie/ mnitajie....." Mwl. Nyerere!!. Tafakari na chukua hatua ndugu yangu Mtanzania.
"Inawezekana kabisa kuwa hata viongozi wetu wamehusika kumwita huyu FISADI wa kimataifa maana watapata share yao".
ReplyDeleteUmenena vema mchangia mawazo hapo juu. Lakini si kwamba INAWEZEKANA tu, hapana, ila WAMEMWITA.
Huu ni wakati wa kusafishana ndugu yangu ili mtu aingie Ikulu. Njia hii inawekwa wazi kwa Lowassa ili baada ya kuwa Rais waendelee na Rostam wake kuyala mema ya nchi hii. Lowassa atamwekea kinga Kikwete ya kuadibishwa kwa lo lote alilotenda ovu kwa Tanzania kama naye JK alivyomkingia kifua Mkapa. Upo hapo? Hii ni cheni ya utawala.
Malalamiko ya kwamba Adawi ametudhalilisha yaelekezwe kwa Kikwete aliyekaa na Lowassa na Rostam kubuni mpango mzima huu wa kumwita huyu mwarabu kuja nchini kutuonesha ubabe wake wa fedha.
Baada ya siku mbili tatu utamskia JK akijisifu kuwa ameweza kumshawishi huyu bwana afikirie matatizo ya nchi yetu na kutupunguzia deni. Hivi huu utumwa hadi lini? Kikwete ameshindwa uongozi jamani. Badala ya kulinda uhai wa watu wake, anawaua kwa mabomu ili kuelekeza fikra za wananchi kwenye janga, na kusahau Katiba Mpya na Dowans. Baada ya mabomu, akaibuka huyu mwarabu mpuuzi.
Tuendelee kumvumilia Kikwete hadi lini? Kwanza hakushinda uchaguzi, ripoti za waangalizi ndiyo zinafichua siri sasa. Aondolewe kama marais wa Tunisia na Misri. TUMECHOKA-A-A-A-A-A-A-A-A-A-!!!!!